BASATA, Wimbo wa Diamond unahamasisha Kuzuia Kampeni Halali ya Kitaifa Afungiwe

Mnyanyembe wa Mboka

JF-Expert Member
Feb 10, 2017
2,348
3,036
Nimeshangaa sana BASATA kwa kukaa kimya dhidi ya wimbo mpya wa Dai ambo kwa uwazi mapana kabisa ameimba kwa maneno ya uchochezi na kuhamasisha watu kupuuzia kampeni halali ya kitaifa dhidi ya uhakiki wa vyeti vya kugushi kwa watumishi wa umma.

Maneno ya Mwanamuziki huyo Nguli asie kua na upeo wala elimu ya Siasa katika wimbo wake amesema:

"... anashangaa badala ya kutafuta pesa watu wamekalia tu habari za vyeti ..."

Kwa kauli hiyo Dai amepinga kauli ya raisi inayohimiza uhakiki wa vyeti kwa watumishi wa umma, ambayo pia kupitia baraza la mitihani la taifa, lilitoa tangazo kwenye vyombo vya habari kuhamasisha wananchi kutoa taarifa za mtu anae dhaniwa au anae tumia vyeti visivyo halali au vya kugushi.

Ni hatari sana kwa mwanamuziki huyu mwenye umbo la PAKA anaejiita SIMBA, kuihamasisha jamii kinyume na kampeni za kitaifa, jambo linaloweza kuisababishia serikali hasara kubwa, katika juhudi za kuhamasisha mambo mbalimbali ikiwamo kupiga vita mambo yanayoweza kurudisha nyuma maendeleo ya Taifa

Kana kwamba haitoshi Mwanamuziki huyo alie Buma na wimbo wake huo mpya ulio chalala katika medani za kisiasa, pia ameongea kauli za kichochezi kwa kulitukana taifa letu kwa kusema

"... Taifa limeingia Matope ..."

Kwa kauli hii ya Taifa limengia tope inamaana Taifa limechafuka au aidha kunuka kwa sababu hajafafanua ni tope la aina gani na limeingilia wapi,

Hivyo mwanamuziki huyo anaesemekana kuwa analea mtoto wa mwinzie akidhani ni wake, anaonekana kuchochea hali halisi ya Taifa kwa mlengo wa kulipaka tope Taifa kama jinsi yeye alivyopakwa tope na mkewe dhidi ya mtoto anaedhani ni wake.

Pia Mwanamuziki huyo nguli asie na elimu ya kutosha hasa katika somo la Uraia, ambae pia hajui ni nini maana ya maendeleo ya Taifa lake, ameongea uongo katika wimbo huo kwa kusema

"...bifu la Konda na Gwajima linachochewa ba binti mmoja kwenye mitandao ..."

Kwa kauli hii BASATA inapaswa kumchukulia hatua mwana muziki huyo nguli anae lea mtoto wa mwenzie akidhani ni wa kwake, kwa sababu ameongea uongo katika wimbo wake kwa kuudanganya umma kwani bifu la Makonda na Gwajima limechochewa na Makonda mwenyewe kumuorodhesha mchungaji huyo katika orodha ya wauza ngada bila ya kua na ushahidi.

Pia BASATA wanapaswa kumchukulia hatua mwanamuziki huyo nguli anaesemekana kuwa ana mdomo mkubwa kuliko wana muziki wote Afrika, kwa kuitumia picha ya Baba yetu wa taifa kama alama ya maudhui ya wimbo wake wenye maneno ya UONGO, UCHOCHEZI na UASI wa kuihamasisha jamii kuacha kuongelea kampeni ya kitaifa ya kuhakiki vyeti kwa watumishi wa umma, licha ya kua Raisi alisisitiza hilo pia Baraza la Mitihani la Taifa likatoa tangazo kwa umma kutoa taarifa za jambo hilo pale litakapo tokea kwa mtu yeyote

Naamini BASATA wako fasta na wanafanya kazi zao kwa weledi licha ya kurudishwa nyuma na kauli ya Raisi pale walipo mkamata Nay na kufungia wimbo wa wake, na badae Raisi akamwachia kwa kumpongeza na kuruhusu mwimbo upigwe.

BASATA mkimuachia Daia katika hili sinto waelewa,


Mnyamwela wa mboka!!!
Unyanyembeeee!!!
 
Diamond yeye mwenyewe anajijua elimu yake ipoje... haniumizi kichwa..!!!
 
hahahaha bawacha bhana si mliususia huu wimbo kumbe mnasikiliza...hivi ile campaign ya kugomea line za voda imeishia wapi?

Basata hawana uwezo wa kufungia wimbo wa Diamond.

Waache wa chizi Roma wafungie wa Diamond?
Nikweli watafungia wa Roma kwa sababu kachana mistari ya ukweli afu inachoma kama pasi
 
Hata Makongoro kupitia Instagram kapinga picha ya baba yake kutumika kati huo wimbo na amesema ni kinyume na Sheria ya Waasisi wa Taifa ya mwaka 2014.
 
Hili la kulea mtoto wa mwenzie limesemwa kwa muda mrefu sana ni wakati sasa DNA itumike kukata mzizi wa fitina.
 
Spelling za BASATA mbona kama zinaelekeana na BASHITE ? Ahhhh hata usemayo sidhani kama watayasikiliza
 
Rekebisha neno mwanamuziki nguli,kina lady jay dee utawaita wanaochipukia au? Huyo jamaa mwite msanii msaka pedsa
 
Basi mtoa uzi ni matunda,
Hapo sawa na ndio maana ukiumwa hospitali unaambiwa kula sana matunda ...

Mtoto afya ikiregea unambiwa mpe matunda kwa wingi ...

Hii ni kwa sababu MATUNDA ni muhimu kwa afya na tiba kwa wagonjwa upo hapo!!!
 
as long as unamsifia Bashite na baba yake wa kumlea BASATA lazima waufyate
 
Back
Top Bottom