Barua yenye Kumb. No. MZR/CID/SCR/105/2011/4 kwa katibu wa Bunge kuomba kumkamata Mbunge wa CCM

mumburya

JF-Expert Member
Mar 19, 2012
321
448
Jeshi la Polisi mkoani Mwanza huenda likamkamata Mbunge wa Busega kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Titus Kamani, ili kumhoji kuhusiana na tuhuma za kutaka kumuua aliyekuwa Mbunge jimbo hilo, Dk. Raphael Chegeni.

Tayari Jeshi hilo limekwisha kumwandikia barua Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Thomas Kashillilah, kumtaka mbunge huyo kwenda Mwanza kuhojiwa kuhusiana tuhuma hizo zinazomkabili.

Jeshi hilo limesema kuwa endapo Dk. Kamani ataendelea kukaidi amri ya polisi ya kwenda jijini Mwanza kutoa maelezo, linaweza kutumia nguvu kumkamata kwa mujibu wa sheria.

Mkuu wa Kitengo cha Upelelezi wa Makosa ya Jinai mkoani Mwanza (RCO), Deusdedith Nsimeki, alisema juzi jijini hapa kuwa mtuhumiwa huyo bado hajafika polisi kutoa maelezo yake dhidi ya tuhuma zinazomkabili licha ya polisi kumtaka kufanya hivyo.

Inadaiwa kuwa Mei 31, mwaka huu, Jeshi la Polisi mkoani Mwanza liliiandikia barua katika Ofisi ya Bunge kumtaka Dk. Kamani kwenda Mwanza kwa ajili ya mahojiano maalumu na jeshi hilo dhidi ya tuhuma hizo.

Nsimeki alithibitisha kuwa hadi sasa Dk. Kamani hajafika Mwanza kutoa maelezo kwa Jeshi la Polisi.

Alisema kuwa ikiwa mbunge huyo ataendelea kukaidi amri hiyo halali, wataomba kibali kwa Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI), ili watumie nguvu kumkamata.

Jeshi hilo liliandika barua Mei 31, mwaka huu, yenye Kumbukumbu No. MZR/CID/SCR/105/2011/4 iliyotumwa kwa Katibu wa Bunge ikimkata kumruhusu Dk. Kamani kwenda Mwanza kutoa maelezo polisi katika Jalada No. MW/IR/2607/2011-MR-CC.28/2011 lililofunguliwa kwa kosa la kula njama na kutaka kumuua Dk. Chegeni.

Watuhumiwa wanne tayari wamekwisha kufikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mwanza kujibu tuhuma hizo.

Waliofikishwa mahakamani na sasa wako nje kwa dhamana ni Dismas Zacharia Ndaki, Erasto Kazimili Kombe, Queen Joseph Bogohe na Ellen Joseph Bogohe.

Kesi yao imepangwa kutajwa Julai 6, mwaka huu.
Dk. Chegeni aliangushwa katika kura za maoni na Dk. Kamani kabla ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka jana.
NIPASHE ilipowasiliana na Kaimu Katibu wa Bunge, John Joel, jana jioni, kuhusiana na suala hilo, alisema kuwa wanachofahamu ni kuwa Dk. Kamani alikuwa Mwanza na kuongeza kuwa kama hajafika Polisi ni kitu kingine.

"Sisi hatupendi masuala kama haya yawasumbue wabunge, lakini la kwake (Dk. Kamani) ni gumu kuliingilia," alisema Joel.

Alipoulizwa kama ofisi ya Bunge ilipokea barua kutoka Polisi ikitaka Dk. Kamani kwenda kuhojiwa Mwanza, Joel alisema hana uhakika kwa kuwa wakati huo hakuwepo katika ofisi hiyo na kusisitiza kuwa anachokifahamu ni kuwa mbunge huyo hivi karibuni alikuwa Mwanza.

CHANZO: NIPASHE
 
mbona umesema jeshi liliandika barua mei 31, hapa sijakuelewa mei hii ya mwaka jana au
 
watoto wa mama wa kambo vs watoto wa mama mzazi mungu nae tamko la jana leo. barua. loo
 
Hii ishapitwa na wakati. Ni ya mwaka jana hiyo

Je, toka wakati huo, sheria ya kumkamata Mbunge imebadilika? Naamini maadam uko hapa wewe ni great thinker. Jiulize na ujijibu.
 
Mla Unga anaombwa ajipeleke kutuoni mwenyewe kabla polisi hajamkamata, mbunge wa upinzani anadakwa kama kibaka na kusafirishwa usiku wa manane, mbunge wa chama fulani polisi wanaandika barua ya kuomba kumkamata mbunge wa chama fulani! This is full comedy!
 
Jeshi la Polisi mkoani Mwanza huenda likamkamata Mbunge wa Busega kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Titus Kamani, ili kumhoji kuhusiana na tuhuma za kutaka kumuua aliyekuwa Mbunge jimbo hilo, Dk. Raphael Chegeni.
Tayari Jeshi hilo limekwisha kumwandikia barua Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Thomas Kashillilah, kumtaka mbunge huyo kwenda Mwanza kuhojiwa kuhusiana tuhuma hizo zinazomkabili.

Jeshi hilo limesema kuwa endapo Dk. Kamani ataendelea kukaidi amri ya polisi ya kwenda jijini Mwanza kutoa maelezo, linaweza kutumia nguvu kumkamata kwa mujibu wa sheria.

Mkuu wa Kitengo cha Upelelezi wa Makosa ya Jinai mkoani Mwanza (RCO), Deusdedith Nsimeki, alisema juzi jijini hapa kuwa mtuhumiwa huyo bado hajafika polisi kutoa maelezo yake dhidi ya tuhuma zinazomkabili licha ya polisi kumtaka kufanya hivyo.
Inadaiwa kuwa Mei 31, mwaka huu, Jeshi la Polisi mkoani Mwanza liliiandikia barua katika Ofisi ya Bunge kumtaka Dk. Kamani kwenda Mwanza kwa ajili ya mahojiano maalumu na jeshi hilo dhidi ya tuhuma hizo.
Nsimeki alithibitisha kuwa hadi sasa Dk. Kamani hajafika Mwanza kutoa maelezo kwa Jeshi la Polisi.
Alisema kuwa ikiwa mbunge huyo ataendelea kukaidi amri hiyo halali, wataomba kibali kwa Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI), ili watumie nguvu kumkamata.
Jeshi hilo liliandika barua Mei 31, mwaka huu, yenye Kumbukumbu No. MZR/CID/SCR/105/2011/4 iliyotumwa kwa Katibu wa Bunge ikimkata kumruhusu Dk. Kamani kwenda Mwanza kutoa maelezo polisi katika Jalada No. MW/IR/2607/2011-MR-CC.28/2011 lililofunguliwa kwa kosa la kula njama na kutaka kumuua Dk. Chegeni.
Watuhumiwa wanne tayari wamekwisha kufikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mwanza kujibu tuhuma hizo.
Waliofikishwa mahakamani na sasa wako nje kwa dhamana ni Dismas Zacharia Ndaki, Erasto Kazimili Kombe, Queen Joseph Bogohe na Ellen Joseph Bogohe.
Kesi yao imepangwa kutajwa Julai 6, mwaka huu.
Dk. Chegeni aliangushwa katika kura za maoni na Dk. Kamani kabla ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka jana.
NIPASHE ilipowasiliana na Kaimu Katibu wa Bunge, John Joel, jana jioni, kuhusiana na suala hilo, alisema kuwa wanachofahamu ni kuwa Dk. Kamani alikuwa Mwanza na kuongeza kuwa kama hajafika Polisi ni kitu kingine.
"Sisi hatupendi masuala kama haya yawasumbue wabunge, lakini la kwake (Dk. Kamani) ni gumu kuliingilia," alisema Joel.
Alipoulizwa kama ofisi ya Bunge ilipokea barua kutoka Polisi ikitaka Dk. Kamani kwenda kuhojiwa Mwanza, Joel alisema hana uhakika kwa kuwa wakati huo hakuwepo katika ofisi hiyo na kusisitiza kuwa anachokifahamu ni kuwa mbunge huyo hivi karibuni alikuwa Mwanza.
CHANZO: NIPASHE
Lengo lako limefail kabla ya kutimia. Hiyo barua ni ya kufoji na hakuna kitu kama hicho.

Huyo Dr. Kamani sio Mbunge tena wa Busega. Ndio huwa maana sisomagi Gazeti la Nipashe.
 
Mla Unga anaombwa ajipeleke kutuoni mwenyewe kabla polisi hajamkamata, mbunge wa upinzani anadakwa kama kibaka na kusafirishwa usiku wa manane, mbunge wa chama fulani polisi wanaandika barua ya kuomba kumkamata mbunge wa chama fulani! This is full comedy!
halafu wanadai tunakwenda na vifungu vya sheria, hawa jamaa hebu wasitugawe aisee, matabaka yalikuwa yanaanza potea sasa yamerudi tena, time will tell
 
Back
Top Bottom