GARETHBALE
Member
- Dec 22, 2013
- 76
- 333
BARUA YANGU KWA ZITTO.
Kwako Zitto,
Habari za siku tele?Ni miaka tele hatujaonana.Kutokuonana kwetu haikuzuia sisi kuwasiliana,simu na barua pepe zimerahisisha sana mawasiliano yetu.
Mimi ni mzima wa afya.Naendelea na majukumu yangu ya kilimo na ufugaji.Nikipata wasaa nitafika Dar es salaam kuja kukusalimia na kuteta nawe mambo kadhaa yahusuyo siasa za nchi yetu.
Dhumuni la barua hii ni kukueleza ya moyoni. Tafadhali usichoke kuisoma kwakuwa inaweza ikawa ni ndefu sana ila kwako ila yenye tija kwa taifa.Naiandika kwako kwasababu najua wewe ni sauti ya wengi.
Najua fika sauti yako itafika hata kwa wasiopenda kusikiliza wengine.Najua fika sauti yako itafika hata kwa wale ambao kwa namna moja au nyingine wanahitaji kukusikiliza ila wamejaa hofu kuwa sauti yako ina ukakasi kwa wasiopenda demokrasia.
Tuachane na hayo,ngoja nirudi katika dhima yangu.Barua hii ina pande mbili.Moja ni pongezi.Mbili ni ujumbe kwa ajili ya wananchi wote wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Nianze na pongezi.Hongera sana kwa usajili wa mwanasiasa Bernard Kamilius Membe.Najua haikuwa kazi rahisi kwako ukizingatia saini yake ilikuwa ikiwaniwa na vyama mbadala vingi nje ya ACT WAZALENDO.
Na kwa tunaomjua Bernard Kamilius Membe tunafahamu kuwa kumshawishi jambo lolote lazima uwe umejipanga sana.Huwa hakubali jambo kwa hoja nyepesi.Huwa hakubali jambo bila utafiti wa kina.Na huwa hafanyi maamuzi bila kupima matokeo yajayo.
Kwakuwa amekubali kujiunga na ACT WAZALENDO basi tambua kwa Bernard Kamilius Membe hayo yote niliyoyaainisha hapo juu ameyafanya na kajiridhisha pasipo na shaka yoyote kuwa yupo mahali salama.Lakini pia na wewe umedhihirisha kuwa uliyoyasimamia wakati unamshawishi ajiunge na ACT WAZALENDO hayakuwa na mashaka yoyote.
Ile dhana kuwa unatumika na mahasimu wa vyama mbadala imekufa rasmi.Umma ulisubiri kwa hamu dhana hii ife siku nyingi sana ila labda zama zile hazikuwa nyakati sahihi.Hii ya sasa ndio nyakati sahihi.
Nihitimishe barua hii kwa kutoa ujumbe kwa wananchi wote wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Shime kwenu watanzania wenzangu,huu ndio wakati ambao njia ya mabadiliko ni nyeupe sana.Ni lazima tuchukue hatua sasa na sio wakati mwingine tena.Vyama ni itikadi ila MEMBE ni imani.Imani haifi.Imani huambatana na baraka.Twendeni pamoja na MEMBE ili atuvushe salama.Tukimfanya MEMBE kuwa imani na sio itikadi amini kwamba uchaguzi huu watanzania watashinda kwa asilimia kubwa sana.Na kwakuwa sera ya ACT WAZALENDO na maono ya MEMBE ni kuwa na Tanzania moja yenye kuelekea kutibu majeraha na maumivu ya watanzania na kwakuwa vyote hivyo vitaponywa kwasababu ya imani basi tumfanye MEMBE ni imani yetu sote na sio itikadi.Alamsiki!
Ni mimi wako mtiifu,
Johnson Mtivila,
Kalamu kutoka Katavi,
19.07.2020.