Pole sana ndugu kwa kupandwa na hasira! Kabouru alikimbilia CCM ambako ameenda kumezwa ambapo, leo hii siasa zake zimeshazikwa kabisa. Hata hivyo, hatumtishie Mhe. Zitto kwa yaliyompata Kabouru, bali bila shaka mchangiaji ameleta tu mfano kuonyesha jinsi CCM inavyoweza kuwalubuni wananchama mahiri wa vyama pinzani kwa leo la kuzika siasa zao. Hata hivyo, nani tena atakuamini hata kutoka jamii ya kwenu utokapo kama njia zilizopelekea kuhama kwako zilionyesha usaliti wa hali ya juu?
Kuna mazingira ambayo hata watu wakiona mtu anahama chama, basi ni rahisi kuelezea na mifano ipo (Dr. Slaa alipotoka CCM, John Magale Shibuda pia alivyotoka CCM kwa zengwe la kunyimwa haki yake ya kusimama kama mgombea). Si hili na Mhe. na kijana mwenzangu Zitto. Utarudisha vipi imani ya wananchi kama hata unashindwa kusimamia msimamo ulioamuliwa na wanachama ndani ya kikao halali?
Cha msingi ninachoweza kusema, jaribu kujipa mwanya wewe binafsi wa kujifunza "UONGOZI" maana hakuna anayezaliwa kuwa kiongozi. Chukulia yaliyotokea juzi na jana ni changamoto katika njia zako za kujifunza kuongoza jamii. Lakini pia kumbuka kwamba, kiongozi ni yule anayeweza Ku-influence watu awaongozao kwa kuwafanya waamini njia uipitayo. Kama juzi watu hao walionyesha wasiwasi na njia uliyotaka kuwapitisha, basi jiulize wapi ulikosea na kurekebisha makosa hayo ili safari iendelee. Kujifunza uongozi ni mchakato unaohitaji muda wa kutosha, na hakuna kipindi kitafika utasema umetosha kujifunza uongozi. Kila kuchapo tunajifunza kitu hiki adimu katika jamii zetu. Ukiweza kusimamia kile wengi wakiaminicho, basi wewe utakuwa kiongozi bora na uongozi wako utakuwa na changamoto chache njiani.