Dr Nickname
New Member
- Dec 28, 2017
- 4
- 3
Shalom wana JF
Niungane na waumini wenzangu duiani pote kushukuru kwa uhai nilio nao, coz najua wengi hawajapata fursa ya kua hai hadi sasa yakiwa yamebaki masaa kadhaa kuhitimisha mwaka huu. kwa sababu mbalimbali wengine wapo katika hali zenye maumivu na majonzi mengi, wakati mimi ni mzima wa afya. Jesus thanks.
Neno moja nalijua, fursa hii ina maana moja tu ni kuwa bado unanidai mambo uliyoniumba niyafanye ambayo hakika sijayakamilisha, niseme asante kwa neema hiii na rehema hizi zinazonitaka kuwa mwajibikaji na wala si kingine.
Nikiwa nautazamia kwa shauku mwaka ujao, naomba nikuletee maombi yafuatayo, ambayo ni haja ya moyo wangu in the coming new year:
Its me, your Son Dr. Nickname
Karibuni muongeze prayer points to JESUS

- Awali ya yote, Mwaka mpya nataka nguvu ya kuacha dhambi kabisa, natubu kwa dhambi ile ya kutamani wake za watu wenye chura ya maana, na wale dogodogo ambao huwa nazini nao kwa macho tu ya kuwatamani. pia natubu kwa dhambi ile ya kulalamika vyuma vimekaza na hata kuwaunga mikono waleta nyuzi kama hizo humu Jf, hadi tunamchanganya mkuu wa kaya, anafikia kutangaza hali ya hatari kwa yeyote atakayeleta data za vyuma kukaza. Sitoisahau dhambi ile ya kuwasema vibaya wapakwa mafuta wako, hasa wanaoomba sadaka kwa wingi tena kwa masikini sisi, yeye akiishi maisha ya kifahali, katika hili nisamehe tu kwani imeandikwa " touch not my saints", pengine umesema " tusimzuie kinywa punda apulapo nafaka".
- Pili, utusaidie kusikia maombi ya watanzania, tumekujengea nyumba za ibada kila eneo vijijini na mijini, Ki ukweli mapepo na shetani wanakiona cha mtema kuni. Cha upande mwingine inashangaza, watanzania wengi tunashinda makanisani, ila cha ajabu idadi ya walio magerezani inaongezeka, idadi ya watoa mimba inaongezeka, dada poa mjini idadi yao inazidi wanaofanya kazi serikalini, lakini pia maisha ya watu wako ki uchumi bado hali si njema sana. Eeeh baba tusikie kuomba kwetu na utusaidie kubadilisha hali hizi 2018
- Tatu, naomba utende muujiza, Mh Tundu lisu arejee akiwa salama, plz hata kama atabadirika, please uwezo wake wa kujenga hoja usimuondolee. Mpe ujasiri zaidi kwani umeamua kumbatiza kwa moto na kwa kuwa umemtunza na tragic ile, tafsri tuliyonayo ni kuwa bado una haja naye, tena kubwa tu kwa taifa hili, Thanks Jesus
- Nne, Tusaidie kama taifa tuwe wamoja, siku hizi tumegawanywa kwa hitikadi za kisiasa na hali zetu za uchumi, kuna wanaoitwa watu wa chini, na wapiga dili, ili kundi la wapiga dili hata watumishi wako kama walimu, wafanyakazi wa sekta za afya, kilimo, n.k pia wamo. lakini maisha yao kiukweli nao pia wanaonekana ni wanyonge, plz Jesus, msaidie mkuu asiwajumuishe watumishi wako hawa kwenye kundi la wapiga dili kwani wao ni daraja la muhimu sana katika maisha yetu ya kila siku. pia Jesus , please tusaidie tuwajue wazalendo kweli kweli katika nchi hii, coz siku hizi uzalendo ni kuunga mkono tu kila kitu kinachoanzishwa magogoni.
- Mwisho, dear Jesus, nipe hekima, na macho yangu yafunuliwe nijue kipaji changu na nikitumie kuwasaidia waja wako humu Jf katika mwaka 2018. natamani niwe na free mind na financial freedom. ukweli nimejua ukiwa broke, uwezekano wa kuishi maisha matakatifu ni ngumu sana, coz unakuwa na wivu na tamaa na ulalamishi usioisha. nitoe katika kundi hili ili niwe baraka kwa wengi.
Its me, your Son Dr. Nickname
Karibuni muongeze prayer points to JESUS