txyz
Member
- Apr 3, 2014
- 89
- 48
Mh.Rais wa JMT naomba kukushauri mambo manne yafuatayo.
Mosi ni kuhusu misaada na mahusiano yetu na mataifa ya magharibi.Hivi karibuni tumeshuhudia kunyimwa fedha za MCC na hata wafadhiri wetu wengine wa ulaya kusitisha misaada kwa nchi yetu.Binafsi siamini km tutasimama na kuendelea km taifa kwa kusaidiwa.
Ila nachokiogopa ni kauli tata za mawaziri na makamu wa pili zanzibar,kauli ambazo zina chembechembe ya vita ya maneno dhidi ya wafadhili hao ambao ukweli ni kwamba wametusaidia sana.Kama tutaendelea na kauli hizo ni wazi tutaingia katika ukurasa wa magomvi na wafadhili hawa na bila shaka tutaumia kwani licha ya jitihada zako za kutaka kujenga viwanda na kufufua vilivyopo,zoezi ambalo ni long term process,ukweli ni kwamba bado tunahitaji msaada.Nashauri diplomasia itumike sana kwa wafadhili hao na pale tunapokubali kutokubaliana,tutoe kauli za kidiplomasia kuepuka kujenga maadui.
Pili ni mfumo wetu wa elimu.Hapa nakushauri uunde tume iuchunguze mfumo wetu ili ili na mapendekezo nini kifanyike.Wakati hili linafanyika,nashauri pia wasimamizi wakuu wa elimu ngazi ya mikoa,wilaya,kata na shule wachunguzwe kama wanazo sifa za kiuyendaji.
Haiwezekani wanafunzi 112 wa kidato cha nne wapate sifuri na 89 daraja la nne kati ya wanafunzi 220 wakati shule ina maabara,umeme na walimu wa kutosha halafu huyo mkuu wa shule aendelee na cheo!"jina kapuni
Tatu ni kupunguza mishahara na posho za vigogo.Kwa hili nikupongeze kwa kuguswa nalo.ushauri wangu ni kuwa fedha itakayopatikana isifanye kazi nyingine tofauti na kuwaongezea mishahara wafanyakazi kima cha chini.
Nne ni kuhusu harambee ya kitaifa ya kuchangia pato la taifa. Kwa kuwa moja ya sababu ya watanzania kukwepa kulipa kodi ilikuwa ni pamoja na kodi iliyokuwa anakusanywa kuwanufaisha wakubwa na kwa kuwa watanzania wamekubali kazi yako,nashauri uone namna ya kuendesha harambee ya kitaifa ambayo itakuwa endelevu ambapo watanzania na watu wengine ndani na nje ya nchi tutachangia kupitia mitandao ya simu kwa hiari na hamasa kubwa. Hii pia itasaidia kujenga uzalendo miongoni mwa watanzania.
Mwisho nakuombea amani,ulinzi wa kimbingu,hekima na busara na mibaraka tele.
Mungu ibariki Africa
Mungu ibariki Tanzania
Amina.