Barua ya wazi kwa Rais Samia Suluhu

EllySkyWilly

JF-Expert Member
Aug 28, 2020
2,204
2,083
Kwako Mhe. Rais wa JMT, MHE. SAMIA SULUHU.

Ombi langu ni kwenye hizi nafasi za kazi za ualimu zinazotangazwa.

Kwakua nafasi zinazotangazwa nichache na wanao omba ni wengi ninakuomba ili kuondoa lawama ni vyema wanaotuma maombi ya kazi waanze kufanya usaili wa kuandika.

Utungwe mtihani kisha wasailiwa wafanye. Wale watakao faulu huo mtihani ndio wapewe ajira.

Kwani wizara ya Tamisemi ikiajiri kwa mfumo inaotumia sasa, watu wataona kama kuna upendeleo unafanyika.

Mimi naona njia ya kufanya mtihani ndio njia bora na ya haki ya kuajiri bila lawama hasa unapoona waombaji wa kazi ni wengi kuliko nafasi zinazotangazwa. Sekretarieti ya ajira wanatumia njia hii na wamefanikiwa sana.

Tamisemi wanaweza kuwaachia kazi ya kuajiri Sekretarieti ya ajira nadhani itasaidia sana kuondoa lawama kwa baadhi ya watu wanaofikiri mfumo wa kuajiri hasa nafasi za kazi za ualimu sio wa haki.

Ahsante sana.
Kazi Iendeleee
 
Hilo ombi lako halitekelezeki. Vijana wangu walio jitolea huenda wakapewa kipaumbele safari hii. Hao wanao kurupuka sasa kuomba, nao nawatakia kila la heri.

Ingawa kiukweli hali ni mbaya mtaani. Na iwapo huo mfumo wa maombi utafunguliwa, basi kutatokea mafuriko ya maombi na mwisho wa siku hao Tamisemi wenyewe, wataishia tu kuchanganyikiwa.
 
Back
Top Bottom