Barua ya wazi kwa Rais Magufuli kuelekea uchumi wa viwanda

MKATA KIU

JF-Expert Member
Nov 22, 2010
2,861
6,219
Habari mh Rais John Pombe Magufuli

Kiukweli sikukupigia kura yangu katika uchaguzi uliopita mwaka 2015 na sababu ya kutokupigia kura nilikuwa siipendi ccm kwa kuirudisha nchi nyuma,, japo nilijua wewe ni tofauti sababu kwa records zako za utendaji lakini sababu ni ccm nilijua wale wale tu hasa ukizingatia ulitambulishwa na mkapa na kikwete na mwinyi jangwani..

Ila nimebadilika sana toka siku ya kwanza za utendaji wako kama rais nikajua nguvu ya soda tu na sarakasi za ccm ila mpaka leo miaka yako miwili ya ikulu nimeamini wewe ni jembe na una vision kali sana ya kuifikisha nchi mbali kwa kuanzia kubadilisha akili za watanzania tuliozoea ujanja ujanja na dezo dezo….

Matajiri wa ulaya na marekani na asia wote wamepata utajiri kwa kugundua kitu kilichoifaidisha dunia,, yaani source za utajiri wao zipo very open and clean ila matajiri wa Tanzania hawawezi tetea hata utajiri wao wakiambiwa waseme walipoupata wanasema walipewa mchango wa shule eti,, au mchango wa harusi million 400.. matajiri wanagawa mpaka pesa ovyo ovyo sababu hawajazitolea jasho kuzipata

Hayo tuyaache, dhumuni la barua hii ni kukupongeza kwa yote unayoyafanya na wazalendo wengi tupo nyuma yako hta kama hatupo ccm, na kuna machache ningependa kukushauri mh Rais kama unaona yanakufaa uyafanyie kazi ili tufike uchumi wa viwanda.

1.Sido na Veta zitumike vizuri

Katika harakati zangu za maisha nimefanikiwa kupita sido na veta na niliona vijana wengi na watu wazima wenye ujuzi tofauti tofauti,,, wanatengeneza mashine ambazo huwezi kuwaza na wengi wao kwa juhudi zao binafsi, magari, usindikaji vyakula, mashine za screen printing, mashine za kutengeneza chaki, mashine za kutreat maji , etc etc hivi vyote wanafanya local kwa jasho lao na mitaji yao… ningependa kushauri ufute safari zote za maofisa za wizara za viwanda na biashara badala yao kuwe na utaratibu wa kuwaomba wenzetu walioendelea wawe wanatoa ruhusa ya hawa jamaa kutembelea viwanda vyao huko duniani na kuwafundisha mbinu bora zaidi za utengenezaji wa mashine zao ili ziweze kuwa za kisasa na kuweza kujiuzia wenyewe nchini na hata kuwauzia nchi jirani na zinginezo kukuza pato la taifa.. nimeomba waende hawa watu wa sido na veta badala ya maofisa au mabosi wa wizara kwa sababu hawa ni wepesi kuelewa watachofundishwa sababu wanakifanya kila siku na wana moyo nacho tofauti na maofisa wao safari wanafata posho tu

2. Elimu ya juu _ vyuo vya uma vyote na hata binafsi vikiongozwa na udsm

Pia mh rais ningependa kushauri vyuo vya uma viongeze vigezo vya upatikanaji wa mwanafunzi bora ( best student), kuwe na mashindano mengi ya ujasiriamali, ugunduzi mfano udsm inawekwa sheria kila mwanafunzi wa udbs lazima aandike wazo la biashara na wanashindanishwa wote mwenye wazo bora anapewa zawadi na mtaji wa kutimiza wazo lake na anasimamiwa na wataalamu pale chuoni kila stage.. hii itaweza kutengeneza ajira nyingi mbeleni na hata kuchangamsha akili za vijana wetu kuwaza tofauti tofauti,,, nina imani udbs ina wanafunzi karibu 1000 kwa mfano kila mtu ana idea yake hapo,, wakiandika wote haiwezi ikakosekana hata moja itakayofaidisha taifa mbeleni,, mambo ya vyeti vya AAAAAAA halafu huna ajira sio sahihi kwa dunia ya sasa..

Havard inasifiwa sababu ya kina facebook, bill gates, google, ford, wallmart, amazon, ni products zao haisifiwi sababu ya AAAA nyingi za vyeti

3. Michezo

Tukianza na yanga na simba ( japo fifa inazuia serikali kuingilia mpira) ila hizi ni timu za wanachama kuwe na usimamizi mzuri ziongozwe na wa kumilikiwa na wanachama wote wawe na equal share, kina manji, dewji, ndio wanaoziharibu hizi timu, kwa kuzifanya ziwe maskini na njaa ili wazidanganye kwa pesa zao na kuzitawala hizi timu na kuharibu mpira, mfano yanga ina mashabiki million 5,, lakini bado inakosa mshahara wa wachezaji wasiozidi 30 eti,,, na hapo kuna vyanzo vya mapato kibao havitumiki… jezi feki zimejaa kariakoo hakuna mtu anaefatilia ambazo haziiingizii timu hata 100 tu,

La pili kwenye michezo ni kuwe na shule ya ziada ya michezo kila mkoa kama ile jakaya kikwete youth park ambapo watoto watacheza michezo yote kuanzia football, basketball, tenniss, volybal, tracking and field etc.. nimependekeza hili sababu sports industry ni ajira kubwa na ina hela nyingi sana NBA huko watu wanalipwa mabilioni, EPL, Tenniss nazo hivyo hivyo..

Watoto wetu waanze cheza organized sports mapema chini ya usimamizi wa serikali ili mbeleni tuje ongeza pato la taifa.

4. Internet and Media

Mh rais kwa maoni yangu tcra wafungie website zote ambazo hazina manufaa kwa taifa, kama china walivyofanya,, website kama za porn, ni za kufungiwa kabisa kupunguza kizazi kisichojielewa

5. Ufisadi

Mh rais huku ndio kaza sura kabisa.. fisadi mmoja akikamatwa adhabu yake inatakiwa iwe kali iwe fundisho kwa mafisadi 100000 watarajiwa. Mfano mtu wa bot au tra au popote ameshiriki kuibia serikali kwa kutumia cheo chake anapaswa afukuzwe kazi on spot, afilisiwe, afungwe jela miaka 10 kwanza baada ya hapo amaliziwe kwa kunyongwaaa.. hii itatoa fundisho kubwa sana kwa kizazi kijacho..

Maana watu hawana huruma kabisa mtu anagawa milioni 1600 ( 1.6b) kwa shule binafsi iliyo na wateja wengi wanaolipa ada kubwaaa… na huyo huyo mtoa hela hajawai changia hata shule ya kata ya mtaani kwake iliyojaa watoto wa maskini wanaokaa chiniii.. kweli ufisadi umefika pabaya sana hawa watu ni wa kunyongwa kabisa

6. wasomi wetu vyuo vikuu watumike vizuri

Mh rais tengeneza mfumo ma dr na ma prof wasikae tu ofisini kusahisha mitihani waende field na kufanya research kwenye fani zao na kuje kuleta solution za kutusaidia na kusaidia dunia siku za mbele..

Hii itatusaidia tutengeneze na sisi mabomu yetu ya nyuklia tusitegemee silaha za kununua kutoka kwa watu sio salama sababu alietuuzia siku tukipigana nae rahisi kutubonda sababu anajua mbinu za kuzuia silaha aliekuuzia.. silaha ukijitengenezea mwenyewe unakuwa salama sana sababu hakuna mtu anaejua siri za umeitengenezaje na unaizuaije kama korea vile anajiamini sababu nyukilia ni za kwake mwenyewe..

Sio silaha wasomi wagundue vingi tuwe na dawa zetu, ndege zetu, ma proff hawatumiki ipasavyo wanakaa vyuoni tu ofisini wanawaza kukamata wanafunzi au kutongoza wanafunzi wao sababu hawana cha kufanya.

7. UJinga na utapeli upigwe vita

Mh rais hapa ndio kaza sura zaidi,, ukitembea mitaani kila hatua unakutana na kibao mganga toka Nigeria, mara mganga anakufanyia mpango hadi unajiunga free mason eti yaani matapeli kibao, mganga anakupa utajiri wakati yeye mwenyewe maskini,, hawa jamaa wanatapeli watu wengi na kufanya ujinga mwingi,, mfano Yule mama airport aliyetembea uchi, kuna wastaafu wanapigwa mafao yao na waganga,,

Na sio waganga tu na hata wachungaji feki wengi wanatapeli watumishi wao kwa njia ya sadaka na fungu la kumi…

Mh rais naomba uweke sheria kali za kuwabana watoa huduma hizi na wote wasajiliwe na wakitapeli mtu nao wanyongwe hadharani kama fundisho

8.Hospitali na afya

Mh rais ningependa kushauri madaktari wote wale wanaofanya surgery sio mabosi waombewe trainings sehem sahihi.. mfano kuna surgery kama zile za kutenganisha walioungana zinazotangazwaga dunia nzima zile ndio sehemu za kuomba ma dr wetu nao waende kwenye surgery room hata wasaidie kushika mikasi nina imani watajifunza kwa kuona na siku ikitokea Tanzania wataweza kufanya na wao.

Ama ile ajali arusha st vicent wale watoto walioenda usa ilibidi na m dr wa Tanzania nao waende nao wakifika kule waone wenzao wanavyotibu watoto ili ujuzi ule waje nao bongo hata siku ikitokea case ingine kama ile wanaifanya wenyewe tu hapa hapa.

Yaani mgonjwa yeyote special case akienda nje aende na mdr wetu wakajifunze kupitia kwake atakavyotibiwa,,

Ama tuwe na utaratibu wa kuinvite madaktari bingwa kama ben carson mhimbili waje watibu wagonjwa hapa hapa huku wanafundisha ma daktari wetu.

9. Michango ya harusi ifutwe na ianzishwe michango ya viwanda vya familia au mitaji

Karibu kila familia Tanzania huwa inachangishana kukiwa na harusi na wanafanya harusi kwa nguvu zote, na pia kila familia ina vijana hawana ajira na hawana mitaji ya kufanyia biashara,, kwa nguvu ile ile inayotumika kuchangishana harusi ndio itumike kuchangiani mitaji nah ii itasaidia kufanya kila familia iwe na kiwanda hata kimoja na mwisho kuwa na viwanda vingi nchi nzima,,

Tatizo la mtaji liondoke kwenye kila familia kwa kuchangishana kama harusi.

10. Mikataba na taarifa zote ziwekwe wazi kama usa.

Mwisho kabisa mheshimiwa rais kuepusha ufisadi kila mkataba uwekwe wazi mitandaoni kila mtu ausomeee, pia vitu kama mishahara wa kila mtu uwekwe wazi kama usa vile, yaani kila kitu kiwe wazi.. mambo ya kuficha ficha haya ndio yanasababisha wiziii na ufisadiii

mheshimwa rais ni hayo tu kama kuna mwenye kuongezea ataandika chini..

Nakutakia afya njema na uendelee na uzalendo huo huo wa kupigania taifa,, ila naomba uongeze spidi kuleta maendeleo naona kama imepungua hiviiii

kwa kumalizia mh rais naomba usitubembeleze wananchi na wala usimbembeleze mtu yeyote kwenye kitu chochote. hakuna nchi iliyoendelea duniani kwa kubembelezana.. nchi za makauzu ndizo zilizoendelea tu.. maendeleo hayaji kwa kubembelezana bembelezana
 
Bora wewe umekuja na wazo zuri. Ila tatizo ninaloliona kwenye hii post yako umejaza mambo mengi na mengine rais hatataka kuyafanyia kazi kwani yanamgusa hata yeye. Kwa mfano hapo uliposema mshahara uwe wazi. Ila pendekezo lako namba moja nimelikubali. Kisha kuna sehemu umechangia kwa mihemko sana. Lakini kwa kuanzia sio mbaya, hongera kwa mawazo yako.
 
Habari mh Rais John pombe magufuli

Kiukweli sikukupigia kura yangu katika uchaguzi uliopita mwaka 2015 na sababu ya kutokupigia kura nilikuwa siipendi ccm kwa kuirudisha nchi nyuma,, japo nilijua wewe ni tofauti sababu kwa records zako za utendaji lakini sababu ni ccm nilijua wale wale tu hasa ukizingatia ulitambulishwa na mkapa na kikwete na mwinyi jangwani..

Ila nimebadilika sana toka siku ya kwanza za utendaji wako kama rais nikajua nguvu ya soda tu na sarakasi za ccm ila mpaka leo miaka yako miwili ya ikulu nimeamini wewe ni jembe na una vision kali sana ya kuifikisha nchi mbali kwa kuanzia kubadilisha akili za watanzania tuliozoea ujanja ujanja na dezo dezo….

Matajiri wa ulaya na marekani na asia wote wamepata utajiri kwa kugundua kitu kilichoifaidisha dunia,, yaani source za utajiri wao zipo very open and clean ila matajiri wa Tanzania hawawezi tetea hata utajiri wao wakiambiwa waseme walipoupata wanasema walipewa mchango wa shule eti,, au mchango wa harusi million 400.. matajiri wanagawa mpaka pesa ovyo ovyo sababu hawajazitolea jasho kuzipata

Hayo tuyaache, dhumuni la barua hii ni kukupongeza kwa yote unayoyafanya na wazalendo wengi tupo nyuma yako hta kama hatupo ccm, na kuna machache ningependa kukushauri mh Rais kama unaona yanakufaa uyafanyie kazi ili tufike uchumi wa viwanda.

1.Sido na Veta zitumike vizuri

Katika harakati zangu za maisha nimefanikiwa kupita sido na veta na niliona vijana wengi na watu wazima wenye ujuzi tofauti tofauti,,, wanatengeneza mashine ambazo huwezi kuwaza na wengi wao kwa juhudi zao binafsi, magari, usindikaji vyakula, mashine za screen printing, mashine za kutengeneza chaki, mashine za kutreat maji , etc etc hivi vyote wanafanya local kwa jasho lao na mitaji yao… ningependa kushauri ufute safari zote za maofisa za wizara za viwanda na biashara badala yao kuwe na utaratibu wa kuwaomba wenzetu walioendelea wawe wanatoa ruhusa ya hawa jamaa kutembelea viwanda vyao huko duniani na kuwafundisha mbinu bora zaidi za utengenezaji wa mashine zao ili ziweze kuwa za kisasa na kuweza kujiuzia wenyewe nchini na hata kuwauzia nchi jirani na zinginezo kukuza pato la taifa.. nimeomba waende hawa watu wa sido na veta badala ya maofisa au mabosi wa wizara kwa sababu hawa ni wepesi kuelewa watachofundishwa sababu wanakifanya kila siku na wana moyo nacho tofauti na maofisa wao safari wanafata posho tu

2. Elimu ya juu _ vyuo vya uma vyote na hata binafsi vikiongozwa na udsm

Pia mh rais ningependa kushauri vyuo vya uma viongeze vigezo vya upatikanaji wa mwanafunzi bora ( best student), kuwe na mashindano mengi ya ujasiriamali, ugunduzi mfano udsm inawekwa sheria kila mwanafunzi wa udbs lazima aandike wazo la biashara na wanashindanishwa wote mwenye wazo bora anapewa zawadi na mtaji wa kutimiza wazo lake na anasimamiwa na wataalamu pale chuoni kila stage.. hii itaweza kutengeneza ajira nyingi mbeleni na hata kuchangamsha akili za vijana wetu kuwaza tofauti tofauti,,, nina imani udbs ina wanafunzi karibu 1000 kwa mfano kila mtu ana idea yake hapo,, wakiandika wote haiwezi ikakosekana hata moja itakayofaidisha taifa mbeleni,, mambo ya vyeti vya AAAAAAA halafu huna ajira sio sahihi kwa dunia ya sasa..

Havard inasifiwa sababu ya kina facebook, bill gates, google, ford, wallmart, amazon, ni products zao haisifiwi sababu ya AAAA nyingi za vyeti

3. Michezo

Tukianza na yanga na samba ( japo fifa inazuia serikali kuingilia mpira) ila hizi ni timu za wanachama kuwe na usimamizi mzuri ziongozwe na wa kumilikiwa na wanachama wote wawe na equal share, kina manji, dewji, ndio wanaoziharibu hizi timu, kwa kuzifanya ziwe maskini na njaa ili wazidanganye kwa pesa zao na kuzitawala hizi timu na kuharibu mpira, mfano yanga ina mashabiki million 5,, lakini bado inakosa mshahara wa wachezaji wasiozidi 30 eti,,, na hapo kuna vyanzo vya mapato kibao havitumiki… jezi feki zimejaa kariakoo hakuna mtu anaefatilia ambazo haziiingizii timu hata 100 tu,

La pili kwenye michezo ni kuwe na shule ya ziada ya michezo kila mkoa kama ile jakaya kikwete youth park ambapo watoto watacheza michezo yote kuanzia football, basketball, tenniss, volybal, tracking and field etc.. nimependekeza hili sababu sports industry ni ajira kubwa na ina hela nyingi sana NBA huko watu wanalipwa mabilioni, EPL, Tenniss nazo hivyo hivyo..

Watoto wetu waanze cheza organized sports mapema chini ya usimamizi wa serikali ili mbeleni tuje ongeza pato la taifa.

4. Internet and Media

Mh rais kwa maoni yangu tcra wafungie website zote ambazo hazina manufaa kwa taifa, kama china walivyofanya,, website kama za porn, ni za kufungiwa kabisa kupunguza kizazi kisichojielewa

5. Ufisadi

Mh rais huku ndio kaza sura kabisa.. fisadi mmoja akikamatwa adhabu yake inatakiwa iwe kali iwe fundisho kwa mafisadi 100000 watarajiwa. Mfano mtu wa bot au tra au popote ameshiriki kuibia serikali kwa kutumia cheo chake anapaswa afukuzwe kazi on spot, afilisiwe, afungwe jela miaka 10 kwanza baada ya hapo amaliziwe kwa kunyongwaaa.. hii itatoa fundisho kubwa sana kwa kizazi kijacho..

Maana watu hawana huruma kabisa mtu anagawa milioni 1600 ( 1.6b) kwa shule binafsi iliyo na wateja wengi wanaolipa ada kubwaaa… na huyo huyo mtoa hela hajawai changia hata shule ya kata ya mtaani kwake iliyojaa watoto wa maskini wanaokaa chiniii.. kweli ufisadi umefika pabaya sana hawa watu ni wa kunyongwa kabisa

6. wasomi wetu vyuo vikuu watumike vizuri

Mh rais tengeneza mfumo ma dr na ma prof wasikae tu ofisini kusahisha mitihani waende field na kufanya research kwenye fani zao na kuje kuleta solution za kutusaidia na kusaidia dunia siku za mbele..

Hii itatusaidia tutengeneze na sisi mabomu yetu ya nyuklia tusitegemee silaha za kununua kutoka kwa watu sio salama sababu alietuuzia siku tukipigana nae rahisi kutubonda sababu anajua mbinu za kuzuia silaha aliekuuzia.. silaha ukijitengenezea mwenyewe unakuwa salama sana sababu hakuna mtu anaejua siri za umeitengenezaje na unaizuaije kama korea vile anajiamini sababu nyukilia ni za kwake mwenyewe..

Sio silaha wasomi wagundue vingi tuwe na dawa zetu, ndege zetu, ma proff hawatumiki ipasavyo wanakaa vyuoni tu ofisini wanawaza kukamata wanafunzi au kutongoza wanafunzi wao sababu hawana cha kufanya.

7. UJinga na utapeli upigwe vita

Mh rais hapa ndio kaza sura zaidi,, ukitembea mitaani kila hatua unakutana na kibao mganga toka Nigeria, mara mganga unajiunga free mason na matapeli kibao,,, hawa jamaa wanatapeli watu wengi na kufanya ujinga mwingi,, mfano Yule mama airport aliyetembea uchi, kuna wastaafu wanapigwa mafao yao na waganga,,

Na sio waganga tu na hata wachungaji feki wengi wanatapeli watumishi wao kwa njia ya sadaka na fungu la kumi…

Mh rais naomba uweke sheria kali za kuwabana watoa huduma hizi na wote wasajiliwe na wakitapeli mtu nao wanyongwe hadharani kama fundisho

8.Hospitali na afya

Mh rais ningependa kushauri madaktari wote wale wanaofanya surgery sio mabosi waombewe trainings sehem sahihi.. mfano kuna surgery kama zile za kutenganisha walioungana zinazotangazwaga dunia nzima zile ndio sehemu za kuomba ma dr wetu nao waende kwenye surgery room hata wasaidie kushika mikasi nina imani watajifunza kwa kuona na siku ikitokea Tanzania wataweza kufanya na wao.

Ama ile ajali arusha st vicent wale watoto walioenda usa ilibidi na m dr wa Tanzania nao waende nao wakifika kule waone wenzao wanavyotibu watoto ili ujuzi ule waje nao bongo hata siku ikitokea case ingine kama ile wanaifanya wenyewe tu hapa hapa.

Yaani mgonjwa yeyote special case akienda nje aende na mdr wetu wakajifunze kupitia kwake atakavyotibiwa,,

Ama tuwe na utaratibu wa kuinvite madaktari bingwa kama ben carson mhimbili waje watibu wagonjwa hapa hapa huku wanafundisha ma daktari wetu.

8. Michango ya harusi ifutwe na ianzishwe michango ya viwanda vya familia au mitaji

Karibu kila familia Tanzania huwa inachangishana kukiwa na harusi na wanafanya harusi kwa nguvu zote, na pia kama familia ina vijana hawana ajira na hawana mitaji ya kufanyia biashara,, kwa nguvu ile ile inayotumika kuchangishana harusi ndio itumike kuchangiani mitaji nah ii itasaidia kufanya kila familia iwe na kiwanda hata kimoja na mwisho kuwa na viwanda vingi nchi nzima,,

Tatizo la mtaji liondoke kwenye kila familia kwa kuchangishana kama harusi.

9. Mikataba na taarifa zote ziwekwe wazi kama usa.

Mwisho kabisa mheshimiwa rais kuepusha ufisadi kila mkataba uwekwe wazi mitandaoni kila mtu ausomeee, pia vitu kama mishahara wa kila mtu uwekwe wazi kama usa vile, yaani kila kitu kiwe wazi.. mambo ya kuficha ficha haya ndio yanasababisha wiziii na ufisadiii

mheshimwa rais ni hayo tu kama kuna mwenye kuongezea ataandika chini..

Nakutakia afya njema na uendelee na uzalendo huo huo wa kupigania taifa,, ila naomba uongeze spidi kuleta maendeleo naona kama imepungua hiviiii
Utakuwa una mke Kufuta michango ya harusi? Umesahau kumwambia katiba mpya itajibu yote hayo uliyo yaandika na mengine mengi ya wadau mbalimbali
 
Pombe yupo busy na kupiga mipasho jukwaani na kupambana na wapinzani mawazo haya atayasoma 2020 during campaign
 
hii bonge ya uzi...point mwanzo mwisho...

kwenye veta na sido umepatia sana..

na hiyo ya udsm wanafunzi walazimishwe kuandika mawazo ya biashara kuwafanya kila mtu kichwa kiwaze mbali...
hata wakiandika kwa kugoogle bado wanakuwa wamechangamsha vichwa vyao na wanagain alot
 
watoto wapewe challenge za kubuni miradi toka wapo vyuoni tujiajiri wengi

Back
Top Bottom