Barua ya wazi kwa rais jk

mtetemo

New Member
Nov 3, 2011
4
0
Barua ya wazi kwa rais

Sisi wafanyakazi 12 wa Bodi ya Tumbaku Tanzania (TTB) kada ya udereva na wahudumu, tunapenda kuwasilisha kwako kero ya uchakachuliwaji wa mishahara yetu uliofanya kati ya Bodi na Hazina.
Kwa mujibu wa taratibu hazina hutulipa mishara ya kila mwezi kupitia akaunti ya bodi na kisha bodi hutupatia hati ya malipo. Tumebaini kuwa toka mwezi Novemba 2010 mpaka mwezi Julai 2011, Hazina ilikuwa ikitulipa mishara mipya, lakini cha ajabu Bodi ilikata ongezeko jipya la mishara yetu na kuendelea kutulipa mishara ya zamani.
Katika kipindi hicho Bodi imekata Sh 15,232,500 kutoka katika mishahara bila ridhaa yetu, takwimu hizi zinatokana na hati za malipo zilizotolewa na hazina ambazo hata hivyo bodi ilizificha na badala yake ilitupatia hati zingine.
Zaidi ya hapo tumebaini kuwepo kwa mawasiliano kati ya bodi na hazima. Katika barua yenye kumb namba TTB/C/FA/26/VOL.VII/28 ya Desemba 27, 2010 yenye kichwa cha habari ongezeko la mishahara ya kada ya udereva na wahudumu, bodi iliiandikia Hazina ikieleza kuwa ‘Salary Slips’ ilizozipokea mwezi Novemba 2010 imeonekana kuwepo kwa ongezeko la mishara kwa kada za udereva na wahudumu. Kwa mujibu wa barua hiyo bodi ilikuwa ikiomba hazina kutoa ufafanuzi wa ongezeko hilo.
Ikijibu barua hiyo, hazina katika barua yake yenye kumbu namba C/BA.54/13/03/10 ya januari 7, 2011 ilijibu kuwa kwa mujibu wa taarifa za zake hakuna marekebisho ya mishahara yaliyofanyika kwa watumishi wa bodi kwa mwaka 2010 na kusisitiza kuwa inawezekana mabadiliko hayo imesababishwa na mapungufu kwenye komputa za mfumo wa malipo. Hata hivyo hazina ilidai kuwa barua ya TTB inafanyiwa kazi na kwamba matokeo ya uchunguzi huo yatatolewa kwa Bodi.
Bodi ya Tumbaku Februari 7, 2011 ilitoa barua kwa wafanyakazi wote yenye kumbukumbu TTB/C/FA/26/VOL.VII/35 ikiwajulisha juu ya majibu yaliyotolewa na hazina kuhusiana na mabadiliko ya mishahara kwa kada ya udereva na wahudumu.
Aidha Machi 2, 2011, bodi iliiandikia tena Hazina barua yenye kumbu namba TTB/C/FA/26/VOL.VII/41 ikieleza kuwa ni takriban miezi minne sasa toka marekebisho hayo kufanyika pasipo hazina kutoa ufumbuzi wa suala hilo hali ambayo ilidaiwa kusababisha manung’uniko makubwa kutoka kwa wafanyakazi husika na chama cha wafanyakazi dhidi ya menejimenti.
Kutokana na barua hiyo bodi iliendelea kuomba maelekezo zaidi ili kuruhusu malipo hayo kufanyika kama ilivyotolewa na kusisitiza kuwa kama si stahili yao kwa maana kuwa inalipwa kimakosa irudishwe hazina. Kwa upande wake hazina ikijibu barua hiyo kwa barua yenye kumbu namba TYC/T/200/809/34 ya Machi 8,2011 ikieleza kuwa maombi ya TTB yanafanyiwa kazi na kwamba bodi itafahamishwa pundu ufumbuzi utakapo kamilika.
Hatimaye Julai 20, 2011 Hazina iliiandikia barua bodi yenye kumbukumbu namba C/CA.251/548/02/8 ikiifahamisha bodi kuwa imefanya uchunguzi na kubaini kuwa mambo manne ni pamoja na mifumo ya mishahara ya bodi ya tumbaku kwa waendeshaji (TTBOS) inafanana na ile ya Bodi ya Utalii Tanzania kwa waendeshaji (TTBOS).
Mengine ni marekebisho ya nyongeza za mishahara hufanywa kwa kuingiza waraka husika kwenye komputa ya malipo na siyo jina moja moja na kwamba marekebisho ya mwisho ya Bodi ya Tumbaku yalifanyika mwaka 2009 yale ya bodi ya utalii yalifanyika mwaka 2010. Pia barua hiyo imesema kuwa wakati wa kurekebisha mishahara ya Bodi ya utalii mwaka 2010 kwa bahati mbaya komputa ilikokotoa mishahara ya TTBO kwa bodi ya tumbaku wakati haikupaswa kufanya hivyo.
Kwa barua hiyo bodi iliagizwa kutolipa mishahara hiyo na kuijulisha Hazina haraka kiasi kilichozidi ili kirudishwe kwenye mfuko mkuu wa serikali vinginevyo fedha hizo zitakatwa kwenye mishahara ya wafanyakazi hao kwa mwezi wa agosti.
Barua hiyo ilisisitiza kuwa iko haja ya kufanya mazungumzo kati ya TTB idara ya bajeti, idara ya Komputa na msajiri wa Hazina ili kukubaliana jinsi ya kubadilisha vifupisho vya viwango vya mishahara ya bodi ya Tumbaku (TTBO), ili kuondoa utata uliopo na vile vya bodi ya utalii Tanzania (TTBO)
Kutokana na barua hiyo ya hazina bodi ya tumbaku iliwaandikia barua wafanyakazi wake wote wa kada ya udereva na watumishi yenye kumbukumbu namba TTB/C/FA/26/VOL.VII/37 ya Julai 22, 2011 ikiwafahamisha juu ya agizo la Hazina na kudai kuwa mishara tunayopata sasa ndiyo iliyo halali.
Pamoja na ufafanuzi huo, tunauliza iwezekanaje toka mwezi Novemba 2010 mpaka kufikia mwezi Julai 2011 makosa yanayodaiwa kusababishwa na komputa yaendelee? Mheshimiwa rais sisi tunaamini kuwa wafanyakazi waliohusika na mchezo huo ambao unaashilia dalili ya wizi wa fedha za umma wawajibishwe.

Sambamba na hilo tumebaini pia kuwa wako baadhi ya wafanyakazi katika bodi yetu ambao wameajiliwa kinyemela pasipo kufuta taratibu za ajira za kutangaza nafasi na kuwafanyia usaili waombaji. Tunafahamu kuwa baadhi ya wafanyakazi hao walikuwa wakiitwa mmoja mmoja na kupewa ajira .
Kama hilo halitoshi tunatambua pia ya kuwa wako baadhi ya wafanyakazi wanaokaribia 10 ambao wameajiriwa hapa lakini hawalipwi mishahara na hazina badala yake kupata misharaha kutoka OC jambo ambalo si utaratibu wa serikali hivyo kuzifanya shughuli zingine za bodi kushindwa kufanyika kutokana na kutokuwa na fedha.
Kutokana na hilo tunaomba tume ya kuchunguza malalamiko haya, sisi tuko tayari kutoa ushirikiano ili kuthibitisha taarifa hizo.
Sisi wafanyakazi wa TTB.
 
Back
Top Bottom