Barua ya wazi kwa Askofu mkuu Yuda Thaddeus Ruwa'ichi

nivoj.sued

JF-Expert Member
Jul 14, 2009
221
190
Barua ya Wazi kwa Askofu Mkuu Yuda Thaddeus Ruwaichi
1566205206865.png

Askofu Mkuu Yuda Thaddeus Ruwaichi-DSM

Mpendwa Askofu Mkuu Yuda Thaddeus Ruwaichi! Kristu!

Sikupenda kabisa kuwasiliana na wewe kwa mfumo huu, lakini kwa vile sina jinsi nimelazimika kufanya hivyo. Nimejitahidi kukutafuta ili tuongee, lakini jitihada zangu zimegonga mwamba!

Ninaomba kukupongeza kwa kuteuliwa na Baba Mtakatifu kuwa Askofu Mkuu wa Jimbo Kuuu la Dar-es-salaam, kuchukua nafasi ya mwalimu wetu wa Teolojia ya maadili Mwadhama Kardinali Pengo. Hongera sana na pongenzi nyingi sana kwa mwalimu wetu kwa kazi ya utumishi aliyoifanya kwa miaka mingi.

Ni imani yangu kwamba kwa kuliongoza Jimbo Kuu la Dar-es-salaam utaongozwa na roho ya kifransiskani. Hayo ni maisha yako na sina cha zaidi kukuelezea. Labda, nikushirikishe kidogo ninayoyajua ya hapa Dar-es-salaam. Ninajua, hutapata wa kukueleza mambo ya Dar-es-salaam kwa uwazi bila unafiki. Lakini sisi tunaofahamiana kutoka huko nyuma, nisipokwambia nitakuwa ninatenda dhambi!

Ningependa nikushirikishe machache ambayo nimeyaona kwa miaka hii ambayo nimeishi hapa Dar-es-salaam na kujaribu kuingia kwenye jumuiya za hapa Dar-es-salaam. Wewe ukiwa Kiongozi wa ngazi ya juu kabisa, na mchugaji mkuu wa Jimbo Kuu la Dar-es-salaam, una nafasi kubwa ya kuleta mabadiliko na kujenga kanisa ambalo ni familia na linakuwa mikononi mwa waumini wenyewe:

1. Bahati mbaya kabisa, hizi Jumuiya Ndogo Ndogo za Jimbo Kuuu la Dar-es-salaam, zimebaki katika ngazi ya kusali pamoja tu, bila kuingia kwa undani kwenye maisha ya mwanajumuiya mmoja mmoja! Maisha ya kumegeana mkate, kujuliana hali, kuchukuliana na kugusana nyoyo [hayapo]. Haya makanisa ya kisasa yanayoibuka, yanapata waumini wengi kwa vile wao wana mfumo wa kumgusa kila muumini. Kanisa Katoliki, bado hatuna mfumo huu, mbali na Jumuiya Ndogo Ndogo. Kuna umuhimu wa kutafuta na kubuni mifumo mipya ya kugusa roho za waumini.

2. Mfumo wa sala za jumuiya ndogo ndogo hauna ubunifu, ni kurudia zile sala za kanisa za asubuhi, mfumo huu unadumaza maendeleo ya imani katika jumuiya zetu.

3. Jumuiya hizi zimeingiliwa na Ukarismatiki, ambao hauna tofauti yoyote ile na Ulokole.

4. Watu bado wanaamini wachawi, mashetani na miujiza. Hivyo sala zote ni za kupambana na wachawi na kusubiri miujiza.

5. Lakini pia kuna tatizo la Mashirika ya kitawa hapa Dar, baadhi ya parokia zinaendeshwa na mashirika haya. Jambo la kushangaza ni kwamba mashirika haya badala ya kueneza Injili, kama walivyofanya wamisionari wa White fathers na wengine, wao wanasambaza maonjo ya roho ya mashirika yao. Unakuta roho ya shirika, sala ni vya mtakatifu wa shirika husika. Mimi nafikiri Jimbo Kuu la Dar-es-salaam, liwe na Mwongozo kwa mashirika haya. Wao washike roho ya mashirika yao, lakini waumini wawe na msimamo mmoja wa Jimbo lao. Hapa, ninaona changamoto kubwa kwako. Wewe ni Mwanashirika. Utaweza kulivusha Jimbo Kuu la Dar-es-salaam kwenye changamoto hii, au utaiongezea zaidi? Ni muhimu jimbo likawa na msimamo wa kichungaji. Mashirika yafanye kazi zake na kuishi “roho” ya mashirika yao, lakini waumini wengine wasilazimishwe kufuata “roho” hizi. Ukishindwa kulifanya hili, na kuambukiza zaidi roho ya shirika lako, ambayo mimi ninaipenda saaaana, utaacha historia itoe hukumu. Ujenge jimbo lenye mshikamano, tofauti za “roho” ziliunganishe jimbo badala ya kulitenganisha.

6. Lakini pia michango inakuwa mingi sana. Badala ya kujenga maisha ya kiroho, tunajenga fedha na miradi. Hili ni la kuangalia sana, vinginevyo tunajenga mashindano ya wenye fedha kwenye makanisa yetu. Sipingi miradi ya kanisa, lakini kuwachangisha waumini kwa mfumo unaoendelea hivi sasa hapa Dar-es-salaam, ni kujenga ufalme wa fedha badala ya Ufalme wa Mungu.

7. Kanisa lianze kutafakari upya mfumo wa utawala wa kanisa. Ni wakati wa kuwa na viongozi wa kiroho na viongozi wa parokia kwa maana ya mtunza fedha na uongozi. Watu hawa waandaliwe, au waajiriwe kufuatana na masomo ya uongozi na fedha. Mapadre wawe viongozi wa kiroho. Wahudumie sakramenti. Lakini ujenzi na miradi na mambo mengine ya utawala na fedha yafanywe na watu wengine, waumini, lakini waliosomea mambo hayo na waajiriwe. Ni wakati wa kutambua kwamba Kanisa ni la watu wote na wala si la kundi dogo la wapakwa mafuta.

Sikuwa na lengo la kuandika point 7, imejitokeza tu!

Ni lazima kuwa mjanja kama nyoka na mpole kama njiwa. Hasa wakati huu ambapo suala la ukabila linachipuka. Nimeona watu wanalalamika kwamba kanisa sasa hivi linaongozwa na Wachaga. Hii ni hatari, inahitaji busara kubwa. Wewe ukiwa hapa ni lazima uwe mwangalifu. Dar-es-salaam ina wachaga wengi, na wengi wao wana nafasi na fedha na ushawishi mkubwa, hivyo jaribu kuwa mwangalifu. Usiwapatie watu faida ya kusema kwamba hawa ni Wachaga!

Usipojibu, nitaelewa tu! La msingi upate nafasi ya kusoma na kusikiliza na ukibahatiwa kuwa na watu wa kukwambia ukweli bila unafiki, umshukuru Mungu.

Ulipoteuliwa kuja Dar-es-salaam, vyombo vingi vya habari vilitaka kujua mengi juu yako. Nilipopigiwa simu nilisema; “Ninamfahamu, tulisoma pamoja, ni mtu mwenye uwezo mkubwa, muadilifu, mcha Mungu na ni Mfransikani”.

Jaribu kwa nguvu zote kushinda kiburi cha madaraka. Unyenyekevu, utakusaidia zaidi na watu watakukubali na kukupokea ukiwa mnyenyekevu.

Ubarikiwe sana na karibu Dar-es-salaam.

Ndugu yako,

Padre Privatus Karugendo.
 
Barua ya Wazi kwa Askofu Mkuu Yuda Thaddeus Ruwaichi
View attachment 1185093

Karugendo wa watu!Naamin bado ana PTOD!Askofu Christopher Mwoleka,mjomba ake alimdanganya sana kwamba atakuja kuwa askofu!Akafanya mambo mengi kinyume cha kanisa katoriki!Pumzika Karugendo,kanisa limeshakuweka pembeni.Tulia jenga ndoa yako!
 
Padre Karugendo? Tuambie kidogo kuhusu maisha ya ndoa na utawa manake umebahatika kuwepo kote kote.
Hayo ya Jimbo Askofu Mkuu atayamaliza kwa nafasi. Nawe toa kaushauri kajinsi ya kuendesha hizi jumuia, anzia na jumuia yako basi!!!!
 
.
Observe the following rules of intellectual engagement:

1. Avoid argumentum adhominem
2. Avoid fallacy of association
3. Avoid genetic fallacy
4.....
 
Pamoja na kua ujumbe huu umetoka kwa mtu anaechukuliwa kwa namna tofauti na jamii ya watu, ukweli ni kwamba huyu ndugu kaongea ukweli iwa uhalisia wa hali ya juu sana.

Alioyasema kuhusu jumuia za kikatoliki nami nikiwa kama mwana jumuiya ni kweli tena ni kweli, kuhusu mashirika ya kitawa nami nikiwa kwenye parokia inaongozwa na shirika la kitawa ni kweli. Na mambo mengi mengi sana yenye kuhitaji mtu mwenye kuyabadilisha bila athari ya katika kanisa.

Huyu askofu kusema ukweli Mungu amuongoze sana kwa sababu sasa watu wengi wamekatishwa tamaa na mapadre na abaadhi ya maaskofu kiasi cha kupelekea kutokuwa na haja ya mambo ya kikanisa na Mungu kwa ujumla.

Ujumbe huu kama utamfikia askofu Ruwaichi basi na aupokee na kuufanyia kazi.
 
Karugendo wa watu!Naamin bado ana PTOD!Askofu Christopher Mwoleka,mjomba ake alimdanganya sana kwamba atakuja kuwa askofu!Akafanya mambo mengi kinyume cha kanisa katoriki!Pumzika Karugendo,kanisa limeshakuweka pembeni.Tulia jenga ndoa yako!
 
Hizi ni hofu tu kwa wale waliozoea aina utawala wa Baba Askofu Pengo na sasa hawajui dira ya Baba Askofu wa sasa.
Kama una dukuduku na hufati utaratibu itashughulikiwa vipi? Na kama sio majungu wa TZ kwanini utumie platform hii.
Unafiki hauwezi kutuacha huru wala kuleta mabadiliko chanya!!
 
nampongeza karugendo kufungua moyo wake na kuongea na baba kupitia jukwaa hili pendwa. Kasema wazi kwamba imebidi atumie njia hii kwa sababu ni ngumu kwake kumfikia baba askofu.lakini imekuwa faida kubwa kwa wakatoliki wa DSM mmejua nini alichosema angeenda kimyakimya hayo ndiyo majungu. Ni nafasi nzuri sasa kwenu kumshauri baba askofu kwani naamini atasoma huu Uzi. Sasa badala ya kupoteza muda kuitana majina jadilini kwa hoja ana za kupinga au kukubaliana kwa sababu sioni kama karugendo analenga kujinufaisha yeye binafsi.a
 
Vitu vya kiimani biblia,rozari vitabu vya watakatifu, ni ghali mnonkwa waumini. Kanisa sio biashara , binafsi nachukia sana japo sio mpakwa. Hivi, kwanini Manisa lisikusanye hela , likatengeneza idara ya uchapshaji biblia ikauzwa 5,000/ mpaka 25,000/ etc .
 
Nimebahatika kuwa chini ya Uchungaji wa Baba Askofu Yuda Thaddeus Ruwa'ichi.....ngoja niheshimu sakramenti yangu ya Kipaimara maana niliapa kuwa "askari" wa imani yangu ila kwa huyu baba mh!

"7. Kanisa lianze kutafakari upya mfumo wa utawala wa kanisa. Ni wakati wa kuwa na viongozi wa kiroho na viongozi wa parokia kwa maana ya mtunza fedha na uongozi. Watu hawa waandaliwe, au waajiriwe kufuatana na masomo ya uongozi na fedha. Mapadre wawe viongozi wa kiroho. Wahudumie sakramenti. Lakini ujenzi na miradi na mambo mengine ya utawala na fedha yafanywe na watu wengine, waumini, lakini waliosomea mambo hayo na waajiriwe. Ni wakati wa kutambua kwamba Kanisa ni la watu wote na wala si la kundi dogo la wapakwa mafuta."
 
Karugendo wa watu!Naamin bado ana PTOD!Askofu Christopher Mwoleka,mjomba ake alimdanganya sana kwamba atakuja kuwa askofu!Akafanya mambo mengi kinyume cha kanisa katoriki!Pumzika Karugendo,kanisa limeshakuweka pembeni.Tulia jenga ndoa yako!

Bado ana haki ya kutoa maoni yake Kama muumini.

Mimi maoni yake nimeyapenda mengi, yana msingi sana.
 
Padre Karugendo? Tuambie kidogo kuhusu maisha ya ndoa na utawa manake umebahatika kuwepo kote kote.
Hayo ya Jimbo Askofu Mkuu atayamaliza kwa nafasi. Nawe toa kaushauri kajinsi ya kuendesha hizi jumuia, anzia na jumuia yako basi!!!!

Watu hamna akili kabisa.
 
Hizi ni hofu tu kwa wale waliozoea aina utawala wa Baba Askofu Pengo na sasa hawajui dira ya Baba Askofu wa sasa.
Kama una dukuduku na hufati utaratibu itashughulikiwa vipi? Na kama sio majungu wa TZ kwanini utumie platform hii.
Unafiki hauwezi kutuacha huru wala kuleta mabadiliko chanya!!

Wewe ndio mnafiki.

Kina kuuma nini Padre kutoa maoni yake humu??

Au ni mmoja wa Wala michango ya waumini kanisani?.
 
Back
Top Bottom