McLaren
JF-Expert Member
- Feb 19, 2025
- 889
- 2,863
Baada ya Chama cha Wananchi (CUF), kuitisha mkutano wa waandishi wa habari katika ofisi za makao makuu Buguruni jijini Dar es Salaam Februari 17, umeibuka mzozo kati ya viongozi na makada walioshitaki kwa msajili, hali iliyowafanya polisi kuvamia mkutano huo kabla haujaanza.
Chanzo cha mgawanyiko huo ni barua ya Msajili wa Vyama vya Siasa iliyobatilisha uchaguzi uliofanyika mwaka 2024, uliomweka Profesa Ibrahim Lipumba katika nafasi ya Mwenyekiti wa chama hicho pamoja na wenzake watano.
Kwa mujibu wa uamuzi huo, Profesa Lipumba na wenzake hawakupata zaidi ya nusu ya kura zilizopigwa, hivyo ushindi wao ukatajwa kuwa batili na uchaguzi huo ulipaswa kurudiwa