Barua toka ofisi ya waziri mkuu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Barua toka ofisi ya waziri mkuu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BRUCE LEE, Apr 14, 2011.

 1. BRUCE LEE

  BRUCE LEE JF-Expert Member

  #1
  Apr 14, 2011
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 2,089
  Likes Received: 1,158
  Trophy Points: 280
  Habari za kazi wana JF?

  Ndugu zangu nimepata barua inayoelezea kuwa inatoka ofisi ya waziri mkuu, tawala za mikoa na serikali za mitaa, barua hiyo inaelezea kua wakimbizi woote wanatakiwa kuondoka katika makambi kwenda kuishi mikoani na wananchi wengine na pindi wakifika huko baada ya kujiandikisha wao na kaya zao basi watapatiwa uraia.

  Utata unaanzia katika barua hiyo ambayo inaelezea kua kila kichwa kitapatiwa fedha laki tatu za kitanzania kwa awamu mbili laki moja na nusu kwanza halafu baada ya kupata makazi mapya then atapatiwa nyingine iliyobakia mbaya zaidi watu hao wanatakiwa kuvunja nyumba zao bila fidia yoyote na kuacha mashamba yao na kisha kutumia laki tatu kama kianzio cha kila kitu kuanzia makazi elimu pamoja na huduma za afya.

  Kiukweli nikiitazama hiyo barua naona kama imechakachuliwa kwanza haina adress ya mtumaji na pia haina muhuri wala saini ya katibu mkuu au waziri.

  Na-attach barua hiyo pia kwa heshima na taadhima naombeni msaada wenu wa mawazo na maoni kwani kuna jamaa zangu wakimbizi wamenifikia na kuniomba ushauri na ufafanuzi zaidi hivyo naaamini hapa wataalam mna uwezo mkubwa wa kutoa njia na mawazo yenu asanteni sana
   

  Attached Files:

 2. K

  Kana Amuchi Member

  #2
  Apr 14, 2011
  Joined: Jul 21, 2009
  Messages: 70
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu yangu habari hii ni ya kweli kabisa na tayari maandalizi yamepamba moto. kuna ndugu yangu yuko Newala, Mtwara aliniambia kuwa wameambiwa kuna wakimbizi watahamishiwa huko ila yeye alidai ni watu 4000 watakepelekwa kwenye vijiji mbalimbali vya huko. na hofu ya watu wa kule ilkuwa ni ujambazi na matukio mengine ya uvunjifu wa sheria ambayo wao hawajayazoea lakini wanasikia kwenye vyombo vya habari kuwa hawa ndugu zetu wageni wamekuwa wakiyafanya kila wanapoweka makazi yao. kuna mgomo unaandaliwa huko kupinga ujio wa watu hao . sielewi mikoa mingine hali ikoje.
   
 3. Kamakabuzi

  Kamakabuzi JF-Expert Member

  #3
  Apr 14, 2011
  Joined: Dec 3, 2007
  Messages: 1,499
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Haionekani kuwa barua sahihi (authentic). Mbali ya kutokuwa na sahihi na dosari nyingine ulizoona, bado kuna nyingine ambazo mtu yeyote makini asingeruhusu barua hiyo itoke tena ofisi ya waziri mkuu!
  Mazao yanayolimwa:
  Kagera: Ndizi, viazi, maharage, mahindi, kahawa na ndizi
  Shinyanga: Mchele ......
  Tabora: Mchele.....
  Mchele haulimwi kinacholimwa ni mpunga!
  Mbeya : Mpunga haukutajwa wakati mojawapo ya wilaya itakayowapokea ni mbalali nk.
  Anyway yote yanawezekana kwani nimeona kwenye website ya prime minister's office mahali pameandikwa "recently documents"
   
 4. pascaldaudi

  pascaldaudi JF-Expert Member

  #4
  Apr 14, 2011
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 534
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Jamani kama hamfahamu hii issue ni ya UN.

  UN huwa wanatoa fedha kwa ajili ya wakimbizi, sasa inapofikia suala la wakimbizi kupewa uraia, UN huwa inaruhusu nchi wanachama kuwapatia uraia wakimbizi, na pindi wanapopata uraia UN huwa inatoa fedha kila mwezi kwa wakimbizi, na hiyo laki tatu nadhani siyo kweli, wanatakiwa kupata zaidi ya hizo, kama kuna mtu anafahamiana na watu waliopo UN ajaribu kufuatilia hilo suala.

  Kuhusu wananchi wanaokataa, ni kutokana na kutokuwa na elimu tu, kwani kama nchi za ulaya zimewachukua kibao na wanaishi maisha ya ahera, na wanalipwa kila mwezi hela za kujikimu, yaani hata kama hafanyi kazi, analipwa, yaani wanauhakika wa kuishi mpaka kufa kutokana na hela za UN.
   
 5. nyengo

  nyengo JF-Expert Member

  #5
  Apr 14, 2011
  Joined: Oct 27, 2010
  Messages: 433
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Mbona hii barua iko kama imechakachuliwa. level ya uandishi naona kama ya kimbea mbea. Nina wasiwasi na barua hii kama ni genuine
   
 6. BRUCE LEE

  BRUCE LEE JF-Expert Member

  #6
  Apr 15, 2011
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 2,089
  Likes Received: 1,158
  Trophy Points: 280
  asante sana kaka pasco nimekuelewa na mpaka dakika hii naamini kabisa kuna uchakachuaji mkubwa unaotaka kufanywa mi nadhani ofisi ya waziri mkuu lazima ipatiwe barua hiyo na wao wajieleze.
   
 7. BRUCE LEE

  BRUCE LEE JF-Expert Member

  #7
  Apr 15, 2011
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 2,089
  Likes Received: 1,158
  Trophy Points: 280
  kamakabuzi upo sahihi asante kwa mchango wako ninafuatilia ili tujue ukweli wa hili jambo kwani hata leo watu huko katumba wanalazimishwa kujiandikisha habari nilizo zipata sasa ni kwamba maeneo hayo wamarekani wameuziwa na serikali na pia wamelipa pesa nyinigi sana, one more favor please who is responsible with all of these and what is to be done
   
 8. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #8
  Apr 16, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,566
  Likes Received: 18,533
  Trophy Points: 280
  Kweli hii ni process ya kawaida inayoitwa Itegration, ni moja ya fumbuzi tatu za kudumu za tatizo la wakimbizi, hii integration inahusisha wakimbizi walioridhia kwa hiyari yao, kupewa uraia wa nchi iliyowahifadhi. Solution nyingine mbili ni Repatriation-kurudi nchini kwao kwa hiyari na Relocation, kuhamishiwa nchi nyingine, -ulaya etc. Mpango wote unagharimiwa na UNHCR, ni kweli wanatoa hela kiduchu za kujikimu, ili fedha zisitumike kama kishawishi.

  Pamoja na fedha hizo kiduchu, wanaendelea kupewa ration ya chakula na kusaidiwa ujenzi wa makazi mapya.
   
 9. M

  MWANANCHI WA MZ Member

  #9
  Apr 16, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 9
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndo nchi ilikofikia wana JF,bt muda wa CCM kutawala nchi hii unahesabika
   
 10. G

  GJ Mwanakatwe JF-Expert Member

  #10
  Apr 16, 2011
  Joined: Mar 26, 2011
  Messages: 241
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Siyo kwa utaratibu huo, hata kama wamepewa uraia wanahamishwa kwa fidia ipi? hizo laki tatu? watajenga vipi makazi mapya na kujikimu? Nafikiri aliyesema eneo limeuzwa yupo sahihi, lakini huo utaratibu wa serikali kuuza ardhi ya nchi kwa nchi tena marekani ni hatari sana, huko ni kuuza nchi. Cuba walifanya hivyo kwa marekani miaka ya nyuma pale gwantanamo bay leo hii inawatokea puani.Serikali iache mzaha kabisa na ardhi yetu, imeanza kurudisha ukoloni tz kwa kuuza ardhi, madini, gas,mafuta nk wanajichukulia , hata ardhi tena? tutalima wapi? mbona watatufanya maskini wa kudumu?
   
 11. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #11
  Apr 16, 2011
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,591
  Likes Received: 797
  Trophy Points: 280
  No comment about authenticity of that letter!
  Lakini mpango huo upo, na umewalenga sana wakimbizi wa muda mrefu, walikuwa kwenye makambi yaliyoko Kigoma, Mpanda na Tabora! Waliomba uraia, instead ya kuwaacha wakae sehemu moja, wanasambazwa sehemu mbali2 za nchi!

  Naomba tusiwaite wezi au kuwaona nusu binadamu, coz ni watu kama sisi, na hatuombi ila nasi twaweza kuwa wakimbizi!
   
 12. BRUCE LEE

  BRUCE LEE JF-Expert Member

  #12
  Apr 16, 2011
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 2,089
  Likes Received: 1,158
  Trophy Points: 280
  nashukuru kwa michango yenu ya kitaalam, tatizo moja na hayo malipo kwa watu hao inaonekana waziwazi yamechakachuliwa kwani hata ofisi ya waziri mkuu wamesema hawaitambui barua hiyo pamoja na uchanganuzi wake. nahitaji msaada zaidi wa nini kifanyike baadhi ya watu hao wamechanganyikiwa na kuniomba nijaribu kuwasaidia kutafuta ufumbuzi asanteni sana
   
Loading...