Barua pepe za Clinton kuchunguzwa

Barua pepe za Clinton kuchunguzwa

kbm

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
5,224
Reaction score
1,686
Maelfu ya kurasa za barua pepe binafsi za aliyekuwa Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani Hillary Clinton zilizotumwa kwa anuani binafsi ya Waziri huyo, zimewekwa wazi hii leo na idara za Usalama nchini humo.

Wizara ya Mambo ya nje ya Marekani imesema kati ya barua pepe hizo, 150 kati yake ni zile zinazodaiwa kuwa na taarifa muhimu na za siri za serikali. Hata hivyo, Clinton mwenyewe amesema kuwa barua pepe hizo alizituma kimakosa, kwa kutumia anuani binafsi kwa shughuli rasmi za kikazi.

Shirika la Ujasusi la Marekani FBI linachunguza ili kubaini kama ni kweli barua pepe hizo zilitumwa kimakosa.

Tukio hili limekuwa gumzo nchini Marekani hasa wakati huu ambapo Hillary Clinton anatafuta ridhaa ya chama chake kuwania urais wa taifa hilo kubwa katika uchaguzi wa mwaka 2016.



Chanzo: BBC
 
USA hakuna waziri.cheo cha mwisho kwenye wizara USA ni katibu Mkuu .Hillary alikuwa katibu Mkuu wa wizara hiyo.Waziri wanaitwa chairman kuepuka siasa kwenye wizara.Chairman wao nahisi ni ISSA
 
Hillary alitumia cheo chake Kufanya biashara clinton foundation .
 
Back
Top Bottom