Rose Mayemba
JF-Expert Member
- May 7, 2012
- 721
- 1,017
Salaam.
Mhe waziri, kwa mamlaka uliyopewa na mhe Rais kuwa waziri wa maliasili na utalii,nakuandikia barua hii uisome,uitafakari kwa makini bila kupuuza hata herufi moja iliyoandikwa kwenye barua hii.
Mhe Waziri, mimi ni mmoja wa wale wananchi waliojitoa mhanga kuhangaikia riziki zao kwa hali na mali bila kuvunja kanuni wala sheria yoyote iliyowekwa na mamlaka zinazotuongoza.
mhe Waziri.
mimi, kwa niaba ya wenzangu wote wanaojishughulisha na biashara haramu ya kuchoma na kuuza zao la mkaa wa miti ya kupandwa katika maeneo mbalimbali ya nchi yetu nimesikitishwa sana na tamko lako nililoliona kwenye vyombo vya habari na mitandao mingine ya kijamii la kuzuia kusafirisha mkaa kutoka wilaya moja kwenda wilaya nyingine.
Mhe waziri,sababu ulizozitoa za kuzuia kusafirisha zao la mkaa kutoka wilaya moja kwenda wilaya nyingine hazijitoshelezi,zina ukakasi,zinaacha maswali mengi kwa kila mwenye akili zisizo na hitilafu.
Mhe waziri,umesema unazuia kusafirisha zao la mkaa kwa sababu ukatwaji wa miti unasababisha uhaba wa mvua na wakati mwingine mvua kutokunyesha kwa wakati, sababu hii haina mashiko Mhe waziri kwani kama hivi ndivyo basi ungezuia pia ukatwaji wa miti ya mbao ambayo hii inavunwa kwa wingi kuliko miti ya mkaa.
Mhe waziri,zoezi la uvunwaji wa zao la miti ya mkaa haujaanza leo, hili ni zoezi endelevu,wakulima huvuna na kupanda miti hii kila mwaka na haijawahi kutokea athari yoyote inayofanana na ulizozitoa kwenye tamko lako.
Mhe waziri, kukosekana kwa mvua kwa wakati mwaka huu si kwa sababu ya uvunwaji wa zao la miti ya mkaa la hasha, ifike hatua serikali wa wananchi kwa ujumla waamini kwamba mabadiliko ya tabia nchi hayazuiliki wa kuepukika isipokuwa kukabiliana nayo.
Mhe waziri, inawezekana kuna jambo hulijui kuhusu zao hili la miti ya mkaa.Miti ya mkaa ni zao la biashara kama ilivyo kwa viazi,miti ya mbao,mahindi na mazao mengine. Zao hili hupandwa na baadae huvunwa kama mazao mengine, wewe na serikali yako mnalazimika kubuni namna nyingine ya kuhifadhi hali ya hewa wala si kwa kuzuia uvunwaji wa miti ambayo ilipandwa kwa kusudi la kibiashara.
Mhe waziri, mimi na wafanyabiashara wenzangu ni walipa kodi halali wa serikali yako kupitia zao hili,tunaishi kwa biashara hii na hatuhitaji kujutia maamuzi ya kufanya biashara hii kwani inatambulika katika wizara yako na inaliingizia taifa mapato.
Mhe waziri,samahani kwa barua yangu ndefu lakini ni muhimu ukanivumilia,haya ninayoyaandika hapa yasiposaidia leo basi yanaweza kufaa kwa wakati mwingine.
Mhe waziri,tamko lako la kuzuia kusafirisha mkaa kutoka wilaya moja kwenda wilaya nyingine halitofautiani kabisa na tamko la kuzuia uvunwaji wa miti hii jambo ambalo ni kinyume kabisa za taratibu za kibiashara ambazo zinawataka watu waangalie namna ya upatikanaji wa fursa za bidhaa zao.
Mhe waziri, mimi ni mkazi wa mkoa wa Njombe ambako ni maarufu kwa utengenezaji wa mkaa wa miti aina ya miwati, watu wengi wa mkoani kwangu hutumia kuni kupikia wakiwemo wachache ambao hutumia mkaa, Miti hii imepandwa kwa wingi sana mkoani kwangu huku matumizi yake yakiwa kidogo sana kufuatia idadi ya watu wa mkoa huu ambao kwa takwimu za sensa iliyopita unakadiriwa kuwa na wakazi laki tano tu(500000).
Mhe waziri, mimi kama mfanya biashara wa zao hili,nikiwa natambua kwamba biashara hii ni huria, ninasafirisha zao hili la mkaa kupeleka jijini dar es salaam ambako ninaamini kuna wakazi wengi na hawana eneo la kutosha kuendeshea shughuli hizi za upandwaji na uvunwaji wa zao hili.
Mhe waziri,kwa tamko lako ambalo ninaamini ukipata nafasi ya kulitathmini utalibatilisha mara moja,unaathiri maeneo mengi sana ya kiutendaji na maisha ya watu kwa ujumla.
Kwanza unatuathiri sisi wafanya biashara wa zao hili ambao tumewekeza pesa zetu nyingi kwenye zao hili,hii inakwenda kuathiri familia zetu moja kwa moja na shughuli zetu za kiuchumi kusimama.
Sisi kama wafanyabiashara kuna watu wamechukua mikopo kwenye mabenki mbalimbali kupitia biashara hii, kwa tamko lako mabenki mengi yaliyokopesha pesa zao kwa wafanya biashara wa zao hili unayatia hasara maana wateja wao hawatakuwa na uwezo tena wa kurejesha pesa hizo.
Mhe waziri, kwa wananchi wa mikoa kama ya Dar es salaam ambao kwa siku hutumia zaidi ta tani za mkaa 300-600 kwa siku watakuwa na mtihani mkubwa sana wa kukabiliana na mabadiliko haya ukizingatia hali halisi ya uchumi ambayo kwa makadirio kila mtanzania anaishi kwa kutumia chini ya dola moja kwa siku.
Mhe waziri,kuna tetesi kwamba mmeingia ubia wa watu wanaoingiza gesi nchini hivyo mmeamua ku discourage matumizi ya mkaa kwa lazima ili kuneemesha matumbo yenu,taarifa hizi kama ni za kweli basi mtakuwa mna dhambi kubwa kwa mwenyezi Mungu na hasa kwa wapiga kura wenu waliowaamini.
Mhe waziri, kabla hamjafikiria kuneemesha matumbo yenu fikirini kwanza juu ya wananchi wa kitanzania ambao chakula chao kikuu ni ugali na maharage, ambao familia zao huanzia watu 5-15, ambao makusanyo yao ya fedha kwa siku ku sh 500-5000. ukifikiri juu ya hayo mhe waziri utalaani tamko lako lakuzuia zao la mkaa lisisafirishwe.
Mwisho kabisa Mhe waziri nikuombe,wakati mwingine wewe na serikali yako kabla hamjafanya maamuzi yoyote mtoe muda wa kutosha wa watu kujiandaa kwa biashara zingine kama mlivyofanya mlipozuia matumizi ya viloba.
Pia naishauri serikali kupitia wizara yako ione namna ya kuhamasisha wananchi kupanda na kuvuna misitu wala si kuzuia uvunwaji wa miti hiyo
Niombe radhi kwa popote nitakapokuwa nimetumia lugha ya maudhi,najua siwezi kumfurahisha kila mmoja lakini hakuna namna WENGINE MTANIPENDAGA NIKIFA...
By Mayemba The Ion..