Barua kwako Eric wa CCM

 
Rudi Tu Kachunge Ng'ombe Boss, Na Magazeti Ukauzie Vitumbua.

Tuliwaambia Namba mtaanza zisoma nyie wenyewe, ila angalau wewe utasaidiana kuzisoma na OFM.
OFM hii imevunja ndoa na kuharibu maisha ya watu wengi sana. CCM hawa hawa walikuwa wanamkingia kifua. Eti mwanamke anakuwa amelala guest yuko peke yake anapigwa picha kesho front page: Jimama Lanaswa Kwenye Mtego Laivu Sinza. Mama wa watu ukimwangalia hana mbele wala nyuma. Alijua maisha ya hawa watu yalikuwaje baada ya kuwaanika hivyo? Eti mlokole tena mzee wa kanisa wakati mwenyewe anamiliki kiota cha zinaa na ngono huko Mbagala (Dar Live). Unafiki mtupu!

Wakati wa kukwepa kodi na kubebwa umeshapita. Na akileta za kuleta CCM wavifungie vigazeti vyake uchwara ajikite kwenye motivationall speaking. Malipo ni hapa hapa duniani kudadadeki!
 
Usitishwe na hili mkuu. Utashangaa hoteli yote ile ni hela ya mkopo. Kuna mtu alidhani kuwa Mbowe anaweza kuwa na madeni mpaka kutupiwa vyombo nje? Usiwaone hawa wakitamba, wengi wao wana mizigo mikubwa ya madeni. Na sasa mahoteli yanapigwa mnada na wakopeshaji kila leo. Sitashangaa!
 
Alifanya kampen mwaka jana hajapewa hela zake na ccm,na ana mikopo bank anaogopa kupigwa minada mali zake,kiufupii anaisoma namba.

Wapo "risk takers" kwa kufanya mambo yao. Wenyewe wanasema "the higher the risk the higher the return".

Tuamini kuna nyakati Shigongo alitengeneza pesa nzuri kupitia shughuli zake. Upepo umegeuka. Akubali kuwa kwenye biashara au kutafuta kuna kupata na kukosa.

Kama yaliyosemwa ni ya kweli, inaonesha bwana huyo si mjanja na hana ukomavu katika mazingira yanayomzunguka.
 
Hiyo hotel ni moja ya mali ambazo zinasubiri kupigwa mnada!!
 
Hiyo hotel ni moja ya mali ambazo zinasubiri kupigwa mnada!!
Aisee haya mahaba hataree hela zote kweli ndyo apeleke ccm sitaki kuamini, au ndyo ule usemi wa awamu hii kwamba mianya ya kupata mali na fedha kijanja janja imeminywa, lakini kuanzia Mwigulu yuko pale waliacha akaunti za ccm zipo ICU, Meghji ndyo kakwangua kabisa, sasa msukuma wa mjini alishindwa nini kugundua kuwa anafanya biashara kichaa, au kufukuzia ubunge kulimtoa ufahamu
 
Inasemekana alipewa "dili" la kusambaza tshirts na vifaa vingine kwa ajili yq uchaguzi na ilikuwa hela ndefu. Akaenda benki kuvuta hela kwa mategemeo kuwa baada ya uchaguzi hela ingerudi na faida lukuki. Ndiyo jamaa kabana na safari hii hakuna EPA
 



Mfanyabiashara kufilisika ni kama timu ya mpira kufungwa goli; One mistake one goal! Investment kubwa moja mbaya ndio kwaheri! Zikafuata kodi, mikopo, kushtakiwa, kuhonga kufunika mambo, nk nk tayari uko nje ya game; na hicho kinaweza kumtengua Erick, good riddance Erick, kiendacho hurudi!
 
Inasemekana alipewa "dili" la kusambaza tshirts na vifaa vingine kwa ajili yq uchaguzi na ilikuwa hela ndefu. Akaenda benki kuvuta hela kwa mategemeo kuwa baada ya uchaguzi hela ingerudi na faida lukuki. Ndiyo jamaa kabana na safari hii hakuna EPA
Angeomba apewe maono na kwenda mahakamani anangoja nini
 
Marehemu John Komba pamoja na kuiimbia CCM maisha yake yote shule zake zilipigwa mnada, akapata pressure, ikamuua. Siasa ni aina fulani ya usangoma, kuweni makini.
 
Ujue hii ni aibu kubwa sana kwa shigongo.hawa watu.aliwa promote sana wakati wa uchaguzi Leo wanamliza.
 

Safi sana. Huyu jamaa ni bonge la mnafiki. Magazeti yake ndio yalikuwa front kumtukama Lowassa kila siku. Ngoja aisome namba!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…