Barua kwa mnyonge

Dr Mambosasa Asante

JF-Expert Member
May 10, 2012
276
250
EWE MNYONGE,


Jina lako halisi mtumwa hili mnyonge umeitwa na mtawala, kabla ya ukoloni mamboleo na mkoloni anatawala, hukufundihswa kujiajiri we ni kazi na mshahara,
Mnyonge hujui akiba maana mwisho wa mwezi una msafara,
Kabla ya unyonge baba yako alikupa uhuru,
Bila ya kumwaga damu wala bila ya kudhuru,
Mnyonge ukapata bendera safi,
Demkrrasia iko juu ila kikubwa haukuasi,
Toka sitini na moja,
We ulikuwa ni muoga,
Mnyonge ulishindwa kushindana hata kwa nguvu ya hoja,
Sio muhalifu ila ukaogopa hadi ma-soldier,
Sitini na nne mkaunganisha nguvu ndo mkawa wamoja,
Mnyonge umeanza unyonge toka kitambo,
Kipindi ya sera za ujamaa mlizoiga toka ng'ambo,
Ila tv iko baba tu
Ukibambwa tu
Una kesi na kichapo juu,
Baada ya mshua kustaafu,
Tukapumua kidogo
Mara akaja bamdgo kutoka kisiwa kidogo,
Then sera ikachange sio ujamaa tena ikawa ruksa kumiliki hata tv antenna,
Ndo kauli ya mnyonge mnyongeni ila haki yake mpeni,
Wanyonge wapinzani ikawa ruksa hadi bungeni,
Then 95 wapinzani kwa kampeni,
Ndipo rasmi mnyonge akawa haogopi hata madeni
Na mkakubali kuitwa wananchi na sio wenye nchi,
Huku wabunge ndio wawakilishi na wala hamkuhoji mbunge kuwa waziri,
Yaani mkaruhusu kipa wenu akadakie timu mbili,
Nisikize
Yaani mbunge kawa mtetezi wa wanyonge halafu mbunge pia anateuliwa kujibu hoja za wanyonge
Eti swali la mbunge toka kongwe linaenda kujibiwa na waziri ambaye ni mbunge toka songwe,
We mnyonge jimbo la waziri nani alichunge au ndo uliompa sindano ukamkataza asidunge,
Na mkaruhusu mbunge eti kuwa speaker wa bunge ukawa muhimili na kazi yao sheria wazitunge,
Mara ukoo ukaanza kufanya biashara bamdogo ben uso wa mbuzi na wala sio wa masihara,
Tra ikaanzishwa ikusanye kodi ichukue,
Hotuba za beni kila mwisho wa mwezi ili tujue
Ukoo unaenda wapi,ukoo una watu wangapi,ukoo una rasilimali nyingi tunakwama wapi,
Ghafla tukaanza na sheria ya soko huria mara mnyonge auze naye anunue anapofikiria,
Leo hii mnamuuliza mama eti mnyonge nini,
Wakati aliyetukuza unyonge wanyonge nyinyi,
Kama hamjiiti mashujaa sio unyonge nini matajiri mnakubali kuitwa nchi masikini,
We ni mnyonge na unataka connection picha ya utupu,
Sawa umekuta bamia ,bilinganya upike supu au,
Wanyonge vijiwe vimegeuka magroup..Mnakataa jina wakati maisha yenu ni ya ku-loop
Mnyonge kuna muda we ujue unatia hasira,
Shida yako unasubiria fanani aiambie hadhira,
Una ardhi haupandi mbegu unapanda hasira, we ndo mwajiri wa raisi bado unaulizia ajira

Mnyonge eti unafanya ngono zembe una michepuko minne halafu hauna hofu hata chembe,
Unafatilia ubuyu nyumbani hawana sembe,
Mnasubiria muokote tikiti tu kwenye miembe
Kuna wanyonge wana hoja za kibaguzi wanasema hupigi kura eti unashiriki tu uchaguzi,
Why now hakupinga wakati yeye ndo mkaguzi,
Wanyonge msinunue story zake za kilanguzi,
Na mnademka na hotuba kisha muhoji,
Wazito wa kupekuwa mnapigwaje ka wamefoji na
Mko radhi kuweka bando muende insta ,ofisi zipo maendeleo hayatafutwi kwenye twitter,
Wanyonge sahivi ni time ya kufanya kazi,
China wananunua mihogo bhasi na tusiwape nazi,
Soko la mahindi ya njano bhasi tusifuge panzi,
Korosho zina soko so tusiache kulima mbaazi,
Na wanaoleta magonjwa wanatuambia hawapingi ,nia yao kila watachowaeleza nyie msipinge , walioleta taharuki watakwambia ujilinde,watawashitua jibu la nape likitolewa na silinde,
Mnyonge muogope anayeandamana chumbani,sera zake zinatekelezeka akiwa jukwaani,
Sawa tunashida so,tukimbie nyumbani,we mnyonge kamwambia beberu haturudi utumwani.

CREDIT TO
CHRISTOPHER KWEKA (BAGHDAD)
 

denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
8,850
2,000
"Wananchi na wenyenchi" kweli kuna tofauti kidogo hapo, panatengenezwa tabaka kati ya watawala na watawaliwa, watawala wanarishishana madaraka wakati watawaliwa wanaishia kuwa wakulima wa jembe la mkono, machinga, na walalahoi wengine.
 

Dr Mambosasa Asante

JF-Expert Member
May 10, 2012
276
250
"Wananchi na wenyenchi" kweli kuna tofauti kidogo hapo, panatengenezwa tabaka kati ya watawala na watawaliwa, watawala wanarishishana madaraka wakati watawaliwa wanaishia kuwa wakulima wa jembe la mkono, machinga, na walalahoi wengine.
Ni kweli Tena Sana Na Tabaka sio Dogo ni kubwa
 

Dr Mambosasa Asante

JF-Expert Member
May 10, 2012
276
250
EWE MNYONGE,

......................
Huku wabunge ndio wawakilishi Na wala hamkuhoji Mbunge kuwa Waziri,
Yaani mkaruhusu Kipa wenu Akadakie Timu Mbili,
Nisikize
Yaani mbunge kawa mtetezi wa wanyonge halafu mbunge pia anateuliwa kujibu hoja za wanyonge
Eti swali la Mbunge toka Kongwe linaenda kujibiwa na waziri ambaye ni mbunge toka Songwe,
We mnyonge Jimbo la waziri nani alichunge Au ndo uliompa sindano ukamkataza asidunge,
Na mkaruhusu Mbunge eti kuwa speaker wa Bunge ukawa muhimili na kazi yao sheria wazitunge,......................................................................................................
, WE NDO MWAJIRI WA RAISI BADO UNAULIZIA AJIRA


Hii sehemu me ndo huwa inanifanya nione kuna umuhimu wa Katiba kufanyiwa marekebisho
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom