Barua kwa JK na PM Pinda (Sehemu ya II)

bwegebwege

JF-Expert Member
Jul 30, 2010
1,071
185
Inaendelea……

Uwekezaji kwenye madini!
Waheshimiwa; hivi serikali ya Tanzania imelogwa? Nkumbuka sana kauli ya Hayati baba wa Taifa aliposhauri serikali isipaparike kuwapa wawekezaji wa nje madini yetu/kumiliki machimbo ya dhahabu, almasi nk, alisema "MADINI KAMA DHAHABU HAIHARIBIKI KWA KUTOKUCHIMBWA! Alishauri kwamba migodi yetu iachwe kwanza aliamini watanzania watapata elimu na uwezo mkubwa kwenye sayansi na teknolojia na kwamba watafaidika sana hapo baadaye!! Baba wa taifa aliweka bayan kwamba kuwapa makaburu na wawekezaji wa nje migodi yetu; wakati hatuna elimu ya kutosha na teknolojia husika ni sawa na kutoa kwa watu sekta muhimu kwenye uchumi wa taifa!! Kweli yule mzee aliona mbali!! Serikali ya BM haikumsikiliza yule mzee, tumeona tuliyoyaona!! Serikali yenu haikusimamia vema madini, tumeona tunayoona sasa!! NI WAZI TANZANIA HAIFAIDIKI NA SEKTA YA MADINI!! Tatizo nini nini?? MIKATABA MIBOVU!!

Wakuu kama kweli mnataka watanzania wawape support kubwa ni kwa nyie kusimamia vema sekta hii muhimu; tuache kelele za kisiasa! Mwambieni "Mami" Ngeleja akaze buti; asione haya kuomba ushauri kwa watu wenye ujuzi, elimu nk!! Tuige mfano nchi za wenzetu jinsi wanavyofaidika na madini, kama haiwezekani basin a tuyaache madini yetu hadi tutakapopata uwezo…hata kama ni miaka mingine 50 ijayo, TUTAWEZA TU!! Mbona ni miaka karibu 50 since uhuru na bado madini "HAYAJATUTOA"??

Najua nyie wote mmefika migodini! Ukifika pale Mererani unapata taswira mbili, UTAJIRI na UMASIKINI!! Zaidi ya 95% ya waliopo kule ni wale waliobeba TASWIRA YA UMASIKINI!! Hawa kucha kuchwa kazi yao ni kuwawezesha MABEPARI WACHACHE WA NDANI NA WALE WA NJE kuendelea kutajirika kwa migongo yao huku wao wakiendelea kutaabika! Wale jamaa kwa taarifa yenu wanaishi kwa kukopa hela za unga na dagaa kutoka kwa "wawekezaji wa ndani"/wa kati na wengine wanishi kwa mishahara midogo huku WAWEKEZAJI WA NJE WANAIBUKA NA MADINI YENYE THAMANI KUBWA NA KUKIMBIZA NJE YA NCHI!!

Wakuu, najua kuna "wenzenu" waliowekeza kule' lakini hebu tufumbe machi na kumkoma nyani!! Mnaonaje kama SERIKALI IKIAMUA KUTAIFISHA/KUREJESHA MIKONONI MWAKE BAADHI YA MIGODI NA KUISIMAMIA? Mkiamua inawezekana! Kuna gharama zake lakini yawezejana hebu tufanye kweli!! Kama wakuu mtaona ushauri wangu haufai basi hebu rejesheni tena mikataba yote bungeni; Mheshimiwa raisi liombe Bunge lako tukufu liwe na vikao maalum kupitia mikataba sekta ya madini na kuirekebisha!! Tupitie upya sheria, sera na sera za madini ili SEKTA HII MUHIMU IONGEZE PATO LA TAIFA NA KUKUZA UCHUMI…si kwa hela hizi za karanga za sasa tunazojisifia nazo!! Tuamue basi jamani, hii sin chi yetu?? Tuweke uzalendo mbele kwanza, LETS DO IT, PAMOJA YAWEZEKANA!! Rudisheni hili kule bungeni, waombeni waheshimiwa (ambao wengi wanatoka kwenye chama chenu) wasilale kama tunavyowaona kila siku kwenye tivii, walifanyie kazi!! Mkilifuata hili by 2015 mtaona hata digirii za heshima zinaongezeka kutoka kwa vyuo vya kueleweka, na zaidi ya yote WATANZANIA WATAWAREJESHEENI SIFA NA HESHIMA KUBWA kwa kuwa mtakuwa mmeweka uzalendo kwanza!!

Miundombinu
Seikali ya awamu ya tatu ilifanya kazi kubwa sana kwenye barabara!! Miundombinu ni eneo muhimu kwa uchumi!! Lakini haitoshi kuwepo na barabara za lami tu; hebu simamieni pia "VIWANGO VYA UJENZI WA HIZO BARABARA"!! Mamlaka husika na zihakikishe kwa mfano KUNA KU-OVERLOAD…Si mnaona kila siku, magari yamezidisha mizigo, wanafika mizani pale Chalinze au Kibaha kwa mfano…unatoa senti kidogo unaruhusiwa kupita!! Kwa nini tusiwashughulikie wahusika? Niwape njia rahis? Kwa mfano; chukua watu wako wa geti jeusi pale (usalama) mpe roli limezidisha mzigo, anaendesha na akifika hizi sehemu anatoa rushwa at the same time anarekodi yanayojiri kule!! Haitachukua muda utaona mabadiliko…!! Kwa nini msiige kwa Kagame? Mwenzenu amefanya mambo makubwa sana; hakuna upuuzi huo kule Rwanda, na anawashughulikia kweli!! Tatizo letu sisi tunawachekea sana hawa watu kwa kuwa SERIKALI IMEKAMATWA/IKO KIBINDONI MWA WAFANYABIASHARA (Tena wengine ni wanachama maarufu wa chama chenu na wengine ni viongozi)!! Matokeo yake mtu anakamatwa amezidisha mzigo afisa muhusika anaishia kupigiwa simu na Waziri au Wakurugenzi…au hata mkuu wa Polisi etc kwamba huyo mtu aachiliwe!! UNATEGEMEA NINI??

Jambo jingine wakuu; hivi sisi mchawi wetu amefariki? Mbona tunakuwa wapole kuliko maelezo?? Inakuwaje serikali inatoa tenda kujenga barabara, mabilioni yanapotea halafu chini ya mwaka baada ya kukabidhiwa barabara mnaanza kuona vituko?? Si mmeona ile barabara ya Kilwa? Yaani hata kuisha bado tayari imeanza kubomoka?? Au kwa kuwa hampiti kule kuelekea home?? Mkiwa wakali, mkikemea waziwazi upuuzi ule hauwezi kufanyika tena!! Yote inafanyika kwa kuwa aliyepewa tenda naye anatoa tenda kwa sub-contructors, nao sijui wanafanya nini na nini…then wana-outsource na kadhalika!! Mnataka kujua zaidi?? Kuna viongozi wenye vijikampuni hivi vya ujenzi…wanafaidika na hizo tenda, kwa hiyo hawaangalii maslahi ya taifa, wanajiangalia kwanza!!! MKITAKA WATANZANIA WAWAKUBALI SIMAMIENI HILI….Wanaovurunda wawajibishwe, wasihamishwe wizara!!

Katika hili kuna suala la MSONGAMANO WA MAGARI DAR-ES-SALAAM!! Nasubiri kwa hamu kuiona Dar yenye "Flyovers" !! Lakini tatizo si hilo tu; tatizo ni kwamba kuna feeder roads nyingi jijini hazijaendelezwa!! Kwa mfano ile barabara ya Mbezi (Morogoro road) kupitia Goba hadi Maeneo ya Tangi bovu; Barabara ya kutokea External kupitia kigogo- Jangwani hadi Karikaoo; Barabara ya kutoka Sinza (Afrika Sana) kupitia Kijitonyama – Kinondoni; Barabara ya kutoka Segerea hadi Morogoro Road (Mbezi) na nyingine nyiiingi!! Mkizijenga hizi kwa kiwango cha lami, ongeza na hizo flyovers mtakuwa mmesaidia!!
Lakini kingine pia ni kurundikana kwa ofisi zote za serikali na amshirika binafsi yote kule mitaa ya Posta!! Hebu anzisheni juhudi za makusudi, wanaotaka kujenga "Supermarkets au Shopping Malls", Maofisi makubwa ya serikali na kadhalika wahamasishwe kutafuta maeneo kwingineko!! Wajenge Goba, Tegeta, Mbezi, Segerea etc…..hii itapunguza suala la kila mtu kuamka na kuelekea kariakoo au posta!! MSIOGOPE KUTHUBUTU!!

Tena mmenikumbusha; ILE ISSUE YA SERIKALI KWENDA DODOMA NI SIASA TU?? WIZARA NGAPI ZIPO DODOMA TANGU SERIKALI YA CCM ILIPOAMUA KUHAMISHIA MAKAO MAKUU KULE DOM?? Naona siisikii tena habari hii,naamini mkiamua yawezekana!! Hebu miaka hii mitano pelekeni Wizara zifuatazo Dodoma!! Kilimo, Mifugo na Maendeleo ya Mifugo; Ujenzi, Miundombinu, Nishati na Madini, East Africa, Sheria na Katiba pamoja na Makamu wa Rais na Mawaziri wake wote (kwani wanafanya nini Dar es Salaam hawa?)

Waheshimiwa; endeleeni kutafakari haya, najua ninawachosha nab ado mna majukumu mengi (hasa kupokea wageni wanaokuja kuwapongeza) nitaendelea na barua hii….
 
Back
Top Bottom