Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 2,436
- 5,234
Wazee wangu nawaona huruma hivi. Pesheni vipi? au ndio mmeshalambisha asali
================
Baraza la Wazee wa Wilaya ya Namtumbo, mkoani Ruvuma, limetoa tamko rasmi likionesha uungwaji mkono wao kwa Mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan, kuelekea Uchaguzi Mkuu ujao.
Wazee hao wamesema kuwa hawana shaka na uongozi wa Samia kutokana na kazi kubwa na ya dhahiri aliyoifanya katika kipindi chake cha uongozi, hususan katika kuboresha maisha ya wakulima, wafugaji na makundi mengine ya wananchi wa kawaida.
Wakizungumza kwa kauli moja, wamesisitiza kuwa Samia amekuwa kielelezo cha uongozi wenye dira, huruma na usikivu, hivyo wanaamini kuwa kuendelea kwake na nafasi ya urais ni kwa maslahi mapana ya taifa.