Baraza La Wawakilishi Waanza Kikao.

Junius

JF-Expert Member
Mar 11, 2009
3,181
139
KIKAO cha Baraza la Wawakilishi kinaanza leo hii Maisara Mjini Zanzibar kikitarajiwa kujadili mambo mbali mbali ikiwemo jumla ya miswaada sita ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ambayo inatarajiwa kuwasilishwa katika kikao hicho.
Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyosainiwa na Mwandishi wa Habari za Baraza hilo, Talib Enzi Talib amesema matayarisho ya kikao hicho yote yameshakamilika ikiwemo takriban wajumbe wote wameshawasili kutoka kisiwani Pemba kujumuika na wenzao wa Unguja kwa lengo la kuhudhuria kikao hicho ambacho kitachukua wiki mbili.
Kikao hicho ambacho ni mkutano wa 17 kutawasilishwa mswaada sita ikiwemo maswali na majibu ambapo mapendekezo ya mswada wa sheria utaodhibiti usafirishaji fedha haramu na mapato ya uhalifu na mambo mengineyo.
Miswada mingine ambayo inatarajiwa kuwasilishwa katika kikao hicho ni pamoja na wa Sheria ya Kukuza Utalii, Sheria ya Usimamizi wa Kodi, Sheria ya Kubadili Sheria ya Bodi ya Mapato, Sheria ya Kurekebisha Sheria ya Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar na sheria ya Dawa za Kulevya na kudhibiti usafirishji haramu wa dawa hizo
kutokana na mswaada huo Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) inakusudia kuanzisha Kitengo cha taarifa za fedha na Kamati ya Kitaifa, ambayo itaweza kuwanasa wasafirishaji wa fedha haramu na mapato ya vitendo vya uhalifu, zikiwemo fedha za mitandao ya ugaidi.
Kikao hicho ambacho ni mkutano wa 17 kutawasilishwa mswaada sita na maswali na majibu ambapo mapendekezo ya mswada wa sheria utaodhibiti usafirishaji fedha haramu na mapato ya uhalifu na mambo mengineyo utajadiliwa.
Kutokana na mswaada huo Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) inakusudia kuanzisha Kitengo cha taarifa za fedha na Kamati ya Kitaifa, ambayo itaweza kuwanasa wasafirishaji wa fedha haramu na mapato ya vitendo vya uhalifu, zikiwemo fedha za mitandao ya ugaidi.
Mswada huo ambao utatambulika kwa jina la mswaada wa sheria ya usafirishaji wa fedha haramu na mapato ya uhalifu, umeainisha vipengele kadhaa vitavyoweza kuipa nguvu serikali pamoja na vyombo vya kusimamia sheria kuwabana wahusika wa vitendo hivyo pamoja na kuunda Idara hiyo.
Baadhi ya vipengele vya mapendekezo ya sheria hiyo, vinatoa kinga kwa watendaji wa Polisi, Mahakama na Idara ya Mkurugenzi wa Mashitaka katika kufuatilia watuhumiwa wataobainika kujihusisha na usafirishi wa fedha haramu na mapato ya uhalifu.
Aidha, mswada huo pia umeainisha namna sheria hiyo itavyoweza kufanya kazi katika maeneo ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, katika suala la kuwabana wahalifuhao ikiwa pamoja na mataifa ya kigeni.
Kwa mujibu wa mswada huo, katika sehemu ya kifungu cha 10 ambacho kitatoa haki ya kuundwa kwa kitengo hicho kikiwa ni Idara zaidi ya Wizara.
Kitengo hicho kitakuwa na dhamana ya kupokea, kuchambua na kusambaza taarifa zilizopokelewa juu ya suala hilo kutoka kwa watu wataotowa taarifa na vyanzo vyengine ndani na nje ya nchi.
Kifungu cha 11, kimefahamisha kuwa, kutakuwa na Kamati ya kitaifa ya kushughulikia usafirishaji fedha haramu.
Masharti ya mswada huo ambao unafuatia sheria ambayo tayari imepitishwa na Bunge ambayo inashughulikia usafirishaji wa fedha haramu yatatumika na kufanya kazi zake hapa Zanzibar, kama kwamba masharti hayo yamepitishwa chini ya sheria hiyo.
“Masharti ya sheria yalioelekezwa chini ya kijifungu cha (1) cha kifungu hiki yatalazimika kwa matumizi yake hapa Zanzibar kutokuwa yamerekebishwa moja kwa moja endapo yatafanyiwa marekebisho na Bunge” kilieleza kifungu cha (2) cha sehemu ya mswada huo.
Msawada huo umefahamisha kuwa utakuwa na uwezo wakutambua ikiwa muombaji ni mtu anayeishi au amesajiliwa katika nchi ambayo kutakuwa na msharti yanayotumika kuzuiya mtandao wa fedha kwa madhumuni ya usafirishaji haramu au kutoa fedha kusaidia ugaidi.
Eneo jengine ni mswada huo kuhusisha namna ya kuwatia hatiani kwa watu ambao watavunja sheria ya usafirishaji wa fedha haramu kwa utekelezaji wa baadhi ya vifungu vya sheria hiyo.
Adhabu ambazo zimetajwa ndani ya sheria hiyo zipo zitazohusisha faini ya shilingi milioni 100 au kifungo cha miaka isiyopungua saba kwa mtu mmoja mmoja na makampuni yakithibitika yatalazimika kulipa faini ya shilingi milioni 250 ama mara tatu ya thamani ya soko ya raslimali yoyote iliyokuwa kubwa.
Mswada huo pamoja na kufanyakazi hizo mswada huo pia utakuwa na uwezo wa kutaifisha mali chafu na utaratibu wa amri yakutaifisha mali chafu, usimamizi wa mali inayotaka kutaifishwa na ukusanjaji wa taarifa juu ya suala hilo.
Madhumi ya mswada huo imeeleza kuwa ni kutunga sheria ya kuzuiya usafirishaji wa fedha haramu na mapato ya uhalifu hapa nchini.
Mswada huo unatarajiwa kuwasilishwa na Waziri anaeshughulikia Fedha na Uchumi, Dk. Mwinyihaji Makame Mwadini leo baada ya kumalizika kwa kipindi cha maswali na majibu.
SOURCE:ZANZIBAR YETU WEB BLOG
 
pamoja na kuwa wamechelewa kutoa miswada hiyo lakini aunde sheria madhubuti kuthibiti.

Kila la heri
 
Kikao hicho ambacho ni mkutano wa 17 kutawasilishwa mswaada sita ikiwemo maswali na majibu ambapo mapendekezo ya mswada wa sheria utaodhibiti usafirishaji fedha haramu na mapato ya uhalifu na mambo mengineyo.
Miswada mingine ambayo inatarajiwa kuwasilishwa katika kikao hicho ni pamoja na wa Sheria ya Kukuza Utalii, Sheria ya Usimamizi wa Kodi, Sheria ya Kubadili Sheria ya Bodi ya Mapato, Sheria ya Kurekebisha Sheria ya Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar na sheria ya Dawa za Kulevya na kudhibiti usafirishji haramu wa dawa hizo
kutokana na mswaada huo Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) inakusudia kuanzisha Kitengo cha taarifa za fedha na Kamati ya Kitaifa, ambayo itaweza kuwanasa wasafirishaji wa fedha haramu na mapato ya vitendo vya uhalifu, zikiwemo fedha za mitandao ya ugaidi.
Kama itasimamiwa vizuri italeta tija kwa jamii.
 
Back
Top Bottom