Baraza la mitihani latangaza Matokeo ya kidato cha sita, Kibaha sekondari yaongoza

Ahsante Tabora Boys kwa kutoa Tanzania One (Best Student) kwa mara ya tatu mfululizo.
Kimbiza kina Mzumbe, Feza, Marian hao
 
Kibaha wamejitahidi sana ila pamoja na kufaulu sana hamna I ya point 3
Yote kwa yote hongera kwao na walimu wao!!
 
Baraza la mitihani nchini(NECTA)limetangaza Matokeo ya kidato Cha sita ambapo shule ya sekondari Kibaha imeongoza.

Kuangalia matokeo, Bofya

Tumeyapokea ila kwa akili ya kawaida tu na isiyotaka sana utumie nguvu nyingi inawezekana vipi Shule za Serikali kwa takribani miaka nenda rudi zinashika tu mikia ( zinakuwa za mwisho ) Kiufaulu halafu ghafla tu leo nazo zinaibuka na Kuongoza.

Kwa mtazamo wangu tu kama GENTAMYCINE na naruhusu nipingwe kwa ' Hoja ' ni kwamba haya ni ' matokeo ' ya Kisiasa zaidi kuliko Uhalisia wake hasa baada ya Wizara husika pamoja na Watendaji wake kuonekana kwamba bado hawajaweza kusimamia Elimu ya nchi hii ambayo kama ' Mwanataaluma ' sioni aibu wala haya kusema kwamba kwa sasa ipo ICU.

Ni matokeo ya kutaka kumuonyesha Mheshimiwa Rais kuwa Wizara inafanya Kazi yake vyema kabisa na kwamba ' Bwana Mkubwa ' asiwe na wasiwasi na wala pengine asiwaze ' Kuwatumbua ' katika nafasi zao. Sina shida na hiyo Shule ya Kibaha Kuongoza au Kufanya vyema katika matokeo ila Kilio changu Kikuu ni kwamba ' Kitaaluma ' ufaulu wa Mtu huwa hauji kwa haraka hivyo na nimeshikwa na butwaa kwakuwa kwa Historia ya miaka 10 iliyopita Shule za Serikali zilikuwa ' chali ' kabisa kimatokeo hivyo leo hii Mimi kuamini kuwa kuna ' improvement ' huko tena ya ghafla hivi itakuwa ngumu.

Tuacheni Siasa na ukweli utabaki pale pale kwamba Elimu ya Tanzania kwa sasa ipo ICU na 90% ya Shule za Serikali zina matatizo makubwa ya Kimsingi yanayojumuisha Taaluma yenyewe. Watendaji wengi wa Serikalini kwa sasa wanafanya Kazi kwa Sifa Kuu mbili 1. UWOGA, na 2. KUJIPENDEKEZA ili mradi tu ' Vitumbua ' vyao visiingie ' mchanga '.

Haina shida tuendeleeni tu ' Kudanganyana ' hivi hivi ila chezeeni vitu vyote lakini siyo Elimu kwani tutakuja Kujuta mbeleni.

Nawapongeza wale wote waliofaulu ' Kimazingaombwe ' na naomba haya ' Mazingaombwe ' yazidi kuendelea hata katika matokeo yajayo ya kuanzia Darasa la Saba, Kidato cha Pili, Kidato cha Nne na Kidato cha Sita. Tutafika tu!
 
Hivi mwaka huu minimum qualification ya kusoma degree ya kwanza ya sheria pale Open Universty ni ufaulu upi?
 
Precious precious Kibaha... Daah . Struggle for success is our school motto... nafurahi kupit a KSS, hongera sana madogo, ndo special school iliyobaki Tanzania kwasasa
Precious precious Kibaha an honoured special school... Special school located in the coast region....


Hahaha mimi sijasoma hapo lakini
 
Back
Top Bottom