Baraza la mitihani hili lina ukweli? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Baraza la mitihani hili lina ukweli?

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by jeremiah michael, Sep 28, 2012.

 1. j

  jeremiah michael Member

  #1
  Sep 28, 2012
  Joined: Sep 5, 2012
  Messages: 14
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 5
  Jamani tuwekane sawa wadau wa elimu,ni kweli kwamba form six wameongezewa muda,hadi mwez wa tano?na nini sababu?
   
 2. l

  leonard ngobole Member

  #2
  Oct 1, 2012
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 12
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Ndio jeremiah, ni kweli kabisa baraza la mtihani limesogeza mbele muda wa kufanya mtihani wa mwisho kwa watahiniwa wa kidato cha sita. Badala ya kufanya mtihani mwezi wa pili kama ilivyozoeleka sasa watafanya mwezi wa tano na ratiba ya mtihani tayari wamekwishaitoa.Sina uhakika sana na hili lakini ninafikiri penginepo wamefanya hivi ili likizo zote ziwe pamoja yaani ile ya o'level na advance, pia wamefikiri kwamba wakifanya hivi watawapa muda wa kutosha kwa wanafunzi wa advance kujiandaa na mtihani tofauti na ilivyokuwa mwanzo ambapo kidato cha 5&6 wanafunzi walikuwa wakisoma kwa miaka miwili kasoro sasa watasoma kwa miaka miwili kwani kuna uwezekano mkubwa wanafunzi wa kidato cha nne kwenda cha tano wakaanza shule mapema zaidi tofauti na ilivyokuwa hapo awali.
   
 3. Kamakabuzi

  Kamakabuzi JF-Expert Member

  #3
  Oct 2, 2012
  Joined: Dec 3, 2007
  Messages: 1,499
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Wana ajenda tofauti na walivyoeleza kuwa ni kuoanisha suala la muhula na likizo. Ebu jiulize je wakifanya mtihani mwezi may vyuo vikuu wataenda lini? si ni mpaka 2014! je mwaka mzima na miezi mitano (may 2013 to sept 2014)watakuwa wanafanya nini. Suala la kidato cha tano kuanza mapema nalo siliafiki kwani ukiangalia ratiba mitihani ya form 4 nayo imesogezwambele kwa mwezi mmoja hadi wiki ya kwanza ya nov. (WEF 2013)
  Nahisi kuna ajenda ya JKT au kuna watoto wa wakubwa hawakufaulu vizuri kuingia vyuo vikuu sasa wanafikiri wakipata mwaka mzima ambao hapatakuwepo form six wapya, itakuwa ndio nafasi yao.
  Hayo ndiyo mapya ya Kawambwa na wenzake - mara std seven multiple choice tupu, sasa mihula, baadae turudishe std 8, baadae tuondoe michezo mashuleni nk ali mradi kila waziri akiingia anafanya vyake.
   
Loading...