Wadau serikali kivuli duniani kote hupaswa kuonesha kiwango cha juu cha uwezo kuliko serikali. Hii ni moja ya changamoto kubwa ninaiona katika mwenendo wa mpambano kati ya baraza la jk na baraza kivuli.
Ukweli baraza la JK ni dhaifu lakini kiwango cha shadow cabinet kuonesha uwezo mbadala bado ni changamoto iliyo wazi. Naomba tujaribu kupitia wizara moja hadi nyingine tupime kama msemaji wa kambi ya upinzani anaonesha uwezo kiasi gani ukilinganisha na waziri husika, naibu wake na hata mwenyekiti wa kamati ukizingatia kuwa kamati zote za kisekta zinaongozwa na wabunge wa ccm. Kwa mfano linganisha wizara ya fedha, nenda nishati na madini, kilimo, miundombinu, mifugo, makazi, miundombinu, uchukuzi, tamisemi, elimu, afya. Nk.
Je, pamoja na udhaifu wa vilaza walioshika uwaziri katika wizara hizi nikweli kuwa mawaziri vivuli wanaonekana kufunika? Huwa naona aibu sana kuona wenyeviti wa kamati wanakuwa visible kuliko wasemaji wa upinzani. Hii ni aibu. Kwasababu mwenyekiti wa kamati ana mipaka ya mapambano kwakuwa serikali ni ya chama chake lakini msemaji wa upinzani hafungwi na mpaka wowote kwani lengo lake hasa kuhakikisha serikali iliyopo inaondoka na serikali ya chama chake inaongoza. Hii ni changamoto.
Mimi najitahidi kufuatilia bunge lakini ukinipa mtihani wa hata kutaja mawaziri vivuli kumi na wizara wanazongoza napata shida kidogo, inanichukua muda na wakati mwingine nachanganya. Hii ni kwasababu mawaziri vivuli hawakati madaraka yao vilivyo. Kuna haja ya training ya kutosha kwa shadow cabinet na kusuka upya kama itaonekana ina tija.