Baraza la Mawaziri halifanyi vikao siku hizi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Baraza la Mawaziri halifanyi vikao siku hizi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Gurtu, Jan 15, 2011.

 1. G

  Gurtu JF-Expert Member

  #1
  Jan 15, 2011
  Joined: May 15, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kauli zinazotolewa na mawaziri na hasa kuhusu Dowans linaiaibisha serikali. Ngeleja ameshasema vya kwake, Sitta tumeshamsikia na hatimaye Chikawe naye amezungumza hivi karibuni. Katika suala la Dowans kumejitokeza pande mbili zinazopingana katika hoja ya kuilipa Dowans. Mh. Sitta alituambia kuwa hawajazungumza suala la kuilipa Dowans katika baraza la mawaziri.

  Jk uko wapi? kwanini huitishi kikao cha baraza la mawaziri na suala la Dowans likawa moja ya ajenda za kikao? Au ndiyo kusema sasa hivi upo likizo? Mawaziri wa serikali moja wanapopingana hadharani ni aibu ya aina yake. Siku hizo kumeibuka aina mpya ya viongozi wa serikali ambao hujitetea pale wanapoona mambo yanawageuka kwa kusema "yale yalikuwa maoni yangu binafsi". Tunaomba maoni ya serikali kwani majukumu yenu kufanya hivyo.
   
 2. The Hunter

  The Hunter JF-Expert Member

  #2
  Jan 15, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 1,049
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Hii inaitwa mwanzo mwisho! Ndani ya muda mfupi serikali itaparaganyika.
   
Loading...