Baraza la Madiwani Manispaa ya Bukoba livunjwe

Baraza la Madiwani Manispaa ya Bukoba livunjwe

Field Mashal

Member
Joined
Jan 16, 2013
Posts
36
Reaction score
13
Kuvunjwa kwa baraza hilo la madiwani kumependekezwa na wananchi wa manispaa kupitia vi-redio vya Bukoba, baada ya kuona kila kitu kinaenda mchafu koge, na kupelekea ongezeko ugumu wa maisha kutokana na wawakilishi wa wananchi kwenye kata kutozungumzia yanayowagusa kwenye halmashauri hiyo.

Leo Baraza limefunguliwa na Meya Aman, lakini wakabadili kanuni makusudi ili waandishi waondolewe kwenye kikao na kumpa Meya nafasi ya kujitanua na kupokea taarifa za utekelezaji wa kila kata ambapo saizi kinachoendelea ni agenda ya Mugambo wanaotumika kunyanyasa wananchi kwa kuvunja nyumba zao eti ni chafu, kupiga watu eti hawajalipa faini baada ya kukutwa hawana shimo la taka, pamoja na kubeba watoto na kuzunguka nao wanaokutwa kwenye nyumba ambayo mzazi pengine ameenda kazini badala ya kuchukua jina la mhusika ili kama nifaini akalipe kwa mujibu wa sheria.

Jambo hilo limekwishafikishwa kwa mkurugezi na waandishi wa habari lakini anashindwa kutoa majibu kwa kisingizio cha kusubiri Meya alizungumzie, kwasababu yeye ndiyo aliyeweka wanamgambo, ambapo kinachofanyika ni kusakama kata ambazo madiwani wake hawamuungi Meya mkono.

Sazi baraza linaendelea lakini waalikwa, na wanahabari wametolewa nje, je kunani zaidi ambacho hawataki wananchi wakijue?
 
Ni bora livunjwe ili wananchi wapewe nafasi ya kuchagu wengine kwani wamevurunda hadi mbunge amekuja kuwabumburua katika manyanga waliokuwa wamekubali kuyapitisha.

Saizi wamepanga kupitisha milioni 200 kulipa mthamini wa soko wakati tume inaendelea na uchunguzi wa taratibu zilizotumika huo huoni kama utakuwa ni wizi kwa wananchi?
 
Back
Top Bottom