Baraza jipya la Mawaziri latangazwa Libya

TUMBIRI

JF-Expert Member
May 7, 2011
1,933
1,199
Hatimaye watawala wapya wa Libya wametangaza baraza lao la mawaziri baada ya wiki sita tangu kuanguka kwa utawala wa Muammar Gaddafi, huku mapigano yakiendelea katika mji wa Sirte alikozaliwa Gaddafi

Mahmoud Jibril, ambaye ni mtaalamu wa mipango na mikakati aliyesomea Chuo Kikuu cha Pittsburgh, nchini Marekani, anabakia na nafasi yake ya uwaziri mkuu na anachukuwa pia nafasi ya uwaziri wa mambo ya nje, jambo linalomaamisha kuwa, naibu wake na aliyekuwa akishikilia wadhifa huo, Ali al-Issawi ametupwa nje.

Mwanauchumi aliyesomea Marekani pia, Ali al-Tarhouni, anaendelea na wadhifa wake wa uwaziri wa mafuta hadi hapo Shirika la Mafuta la Taifa litakapokuwa tayari kuchukuwa nafasi hii.

Mwansheria aliyewahi kujeruhiwa katika vita vya kumuondoa Gaddafi, Abdil-Rahman Al-Keissah, ameteuliwa kuwa waziri wa maafa na Hamza Abu Fas anachukuwa nafasi iliyokuwa ikishikiliwa na Sheikh Salim al-Sheikh kama waziri wa masuala ya dini.

Viongozi hawa wapya wamesema kuwa wataendelea kubakia kwenye nyadhifa zao hadi hapo nchi ikombolewe na iwe na utulivu kamili, ambalo serikali mpya ya mpito itaundwa ndani ya kipindi cha mwezi mmoja.

Source:
http://www.dw-world.de/dw/article/0,,15434755,00.html
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom