Barack Obama aonya dhidi ya viongozi wababe,

radika

JF-Expert Member
Jul 15, 2014
20,427
32,196
_102561103_hi048213786.jpg

Image captionBarack Obama ndiye rais wa pili wa zamani wa Marekani kutoa mhadhara huo, baada ya Bill Clinton

Rais mstaafu wa Marekani Barack Obama amesema ulimwengu umo kwenye njia panda na kwamba kuna mitazamo miwili tofauti kuhusu ubinadamu.

Amesema hayo akihutubu katika mhadhara wa kila mwaka wa Nelson Mandela nchini Afrika Kusini ambao huandaliwa kila mwaka kama sehemu ya maadhimisho ya kukumbuka kuzaliwa kwa kiongozi huyo wa zamani wa Afrika Kusini.

Bw Obama amesema enzi hizi ni za watawala walio na ubabe na kwamba demokrasia haitiliwi uzito sana.

Huku akionekana kumkosoa mrithi wake Donald trump, Bw Obama amesema watawala wenye nguvu wanahujumu karibu kila taasisi ya serikali ambayo huleta maana kwa demokrasia.

Bw Mandela alizaliwa 18 Julai mwaka 1918 na mwaka huu ni karne moja tangu kuzaliwa kwake.

Obama amesema kiongozi huyo aliyepambana dhidi ya utawala wa ubaguzi wa rangi Afrika Kusini alikuwa mtu shujaa kweli na anayefaa kukumbukwa katika historia.

Ametoa wito kwa watu kujifunza mengi zaidi kutoka kwa uongozi wake na kujenga jamii ya kuvumiliana ambapo demokrasia na tofauti baina ya jamii tofauti vinathaminiwa na kusema kwamba vijana wanafaa kutekeleza mchango muhimu katika kuangusha watawala wa kiimla.
Bw Obama amesema kuna kizazi kizima cha watu ambao wamekulia na kulelewa katika ulimwengu uliojaa uhuru zaidi na wa kuvumiliana.

"Hili linafaa kutupatia matumaini," ameongeza.

"Lakini ulimwengu unakabiliwa na tishio la kurejea katika mtindo wa zamani na hatari zaidi na katili wa kufanya mambo.

"Ni lazima tuanze kwa kukubali kwamba sheria zote ambazo huenda zilikuwepo kwenye vitabu …. Miundo ya zamani ya hadhi na mamlaka na unyanyasaji vyote viliangamizwa, lakini havikuangamizwa kabisa," amesema.

Uongozi wa kiimla
Bw Obama amesema kwamba Marekani changamoto dhidi ya utandawazi mwanzoni zilitoka kwa wanasiasa wa mrengo wa kushoto na kisha zikaanza kutokea kwa wanasiasa wa mrengo wa kulia.

Amesema madhara ya kudorora kwa uchumi wa dunia mwaka 2008 - na kutomakinika kwa wasomi na watawala - vilizifanya ahadi zilizotolewa kwa watu kuwa hewa tu.

"Siasa za kuwatia watu hofu na kutoridhika na kuwa na misimamo mikali zilianza kuwavutia watu. Na siasa za aina hiyo sasa zinashika kasi," Bw Obama amesema.

_102561101_hi048209622.jpg
Haki miliki ya pichaAFP
Image captionInakadiriwa watu 15,000 wamehudhuria mhadhara hu
Ameongeza kwamba hawatii watu wasiwasi lakini anaeleza ukweli uliopo.

Amesema katika enzi za viongozi wa kisiasa wenye mamlaka makuu, demokrasia huwa ni kivuli tu.

"Viongozi wenye nguvu kuu kisiasa wameanza kuchipuka...wale walio mamlakani hujaribu kuhujumu kila taasisi au utamaduni unaoipatia demokrasia maana.

Wakuu:

Sasa mmepeta jibu kwa nini huyu jamaa hakuja kuonana na mheshimiwa.
 
Ila siasa za dunia zimepiga U Turn ya nguvu miaka ya hivi karibuni. Leo hii Kiongozi kutoka Marekani nchi iliyokua mstari wa mbele kutoa support kwa serikali ya kibaguzi ya Makaburu leo ndie anakua mgeni mashuhuri kwenye sherehe za kuadhimisha kumbukumbu ya Mpigania Uhuru mashuhuri zaidi duniani akiwapinga Makaburu na haohao Marekani
 
Ila siasa za dunia zimepiga U Turn ya nguvu miaka ya hivi karibuni. Leo hii Kiongozi kutoka Marekani nchi iliyokua mstari wa mbele kutoa support kwa serikali ya kibaguzi ya Makaburu leo ndie anakua mgeni mashuhuri kwenye sherehe za kuadhimisha kumbukumbu ya Mpigania Uhuru mashuhuri zaidi duniani akiwapinga Makaburu na haohao Marekani
Utakua umesahau kuwa alipofariki Mandela,Obama alihudhuria na kutoa maneno kuwa bila wakina Mandela kuupinga ubaguzi wa rangi hata yeye asingekua Rais wa USA enzi hizo akiwa Rais
 
Mwacheni Obama apumuzike. Musije mkamygombanisha na akina JPM.Trump. Putin.Jyping na wenzake. Dunia ya saivi imebadilika sana inahitaji ubabe ubabe.
 
Hayo ni MANENO yake ya kila siku tangu alivyokuwa rais!
Na anawapa na ushoga juu !
Dadadeki!
 
Marekani hofu yao kubwa kwenye siasa ni kudukuana kwenye taarifa...


Africa hofu yetu kubwa kwenye siasa ni kukosoana...


Cc: mahondaw
 
Siasa za Africa.

Mtu anafunga wapinzani wake wote halafu anashangilia ushindi mnono aliopata.

Mtu anazuia wapinzani wake wote kufanya siasa kwa uhuru,halafu anashangilia kukubalika.

Ujinga!
Hata huyo Obama siasa kaja kufanyia huku Africa. Akirudi kwakwe US anasubiri uchaguzi
 
Back
Top Bottom