Barabara za umeme Tanzania zanukia

Barabara za umeme Tanzania zanukia

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2016
Posts
757
Reaction score
1,822
Wizara ya Ujenzi ,Uchukuzi na Mawasiliano nchini kwa kushirikiana na shirikisho la Barabara Duniani (PIARC) limeandaa Mkutano wa Kimataifa utatakaohusia na miundombinu ya Barabara na usafirishaji utakaofanyika jijini Arusha kesho.

Akiongea na waandishi wa habari mapema Leo, katibu Mkuu wizara ya Ujenzi ,Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Joseph Nyamhanga amesema mkutano huo utazishirikisha nchi 25 wanachama wa shirikisho hilo na kufunguliwa na Mhandisi Isack Aloyce Kamwelwe Waziri wa Ujenzi ,Uchukuzi na Mawasiliano.

Aidha amesema lengo la mkutano huo ni kuangalia matokeo ya uwekezaji katika Miundo Mbinu ya Usafirishaji , kubadilishana uzoefu na matumizi ya teknolojia za kisasa katika Ujenzi wa Barabara kwa nchi zinazoendelea.

Akiongelea mpango wa serikali katika Ujenzi wa Barabara za Lami hapa nchini amesema serikali IPO katika hatua ya kukamilisha mtandao wa Barabara za Lami kwa kuunganisha Majiji yote na baadhi ya nchi jirani.

Naye Mwenyekiti wa chama cha Barabara Tanzania(TARA),Joseph Haule Amesema mkutano huo utajadili teknolojia za kisasa kuhusu matumizi ya umeme katika Barabara ili kuondokana na matumizi ya magari ya Mafuta ambayo yamekuwa chanzo cha uharibifu wa mazingira.

Amesema katika mkutano huo watapata fursa kwa Mataifa mbalimbali kubadilishana uzoefu namna ya Ujenzi wa Barabara za kisasa zitakazoweza kuondoa msongamano katika miji Mikubwa na inayokua .

Amesema moja ya Mipango ya Kisasa hapa nchini ni pamoja na Ujenzi wa Barabara ya kimataifa iliyojengwa Arusha kutoka Sakina hadi Tengeru ikiwa na urefu wa kilometa 14 na Ujenzi wa Barabara ya Afrika Mashariki inayoendelea kujengwa kwa lengo la kupitisha magari makubwa na kupunguza Masongamano Mjini.

Mkutano huo wa kimataifa ni wa kwanza kufanyika hapa nchini na utawashirikisha washiriki zaidi ya 200 kutoka nchi zaidi ya 25 Duniani .

Ends...........
 
Back
Top Bottom