Barabara za Arusha na kero zake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Barabara za Arusha na kero zake

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mary Chuwa, Mar 21, 2011.

 1. M

  Mary Chuwa Senior Member

  #1
  Mar 21, 2011
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 178
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Kwa kweli sijui kama hii inaweza kuwa kero kwa wengi lakini,kwangu mimi ni kero sana.
  Pamoja na uduni wa barabara za Arusha.

  Kitu kinachonikera ni alama za waendao kwa miguu,katika Manispaa ya Arusha barabara ya Uhuru ina alama tatu moja ipo pale karibu na Naaz Hotel,nyingine Metro na nyingine Friends' Corner,pamoja na alama za pundamlia kutoonesha vizuri kutokana na wahusika kutorjeza alama hizo pindi zinapochakaa.

  barabara nyingine hazina kabisa,barabara ya Wachaga amabayo ndiyo barabara inayotoka stendi ya vifodi kueleke Njiro,Majengo,Mbauda,na hata mabasi ya Abiria wa Mikoani kama Mara,Mwanza na Dodoma,ina kivuko cha waendao kwa miguu hapo karibu na Idara ya Maji lakini napo ni kmaa hakijulikanai kwani huwa alama hiyo inapofutika inachukua muda sana kuirejesha.

  Barabara nyingine ni ile inayotoka Mianzini kuja Stendi ya Mkoa,haina alama ya waendao kwa miguu(pundamilia) ni hatarai sana kwa wavukao barabara hii kwenda upande wa pili na hapo magari hupita kwa kasi bila kujali na wahusika wanaliona jambo hili na wala hawajishughlishi.

  Barabara nyingine ni inayoelekea kwa Iddi,Ngaramtoni na nchi jirani ya Kenya,hii ndiyo kabisa ni balaa,kwani haina kivuko ukiachilia mbali mataa ya Mianzini,na hii barabara kuna shule mbali mbali ,St Patric,Secondary lakini ndiyo wala hakuna kivuko,kituo cha kusimama vifodi,pale Triple A, Sakina ,na Raskazoni hakuna usalama wa watu katika hili.

  Barabara nyingine ni hiyo ya Dodoma, hakuna kabisa maana kuna shule mbili za Msingi pale Mwangaza na Ngarenaro,ila kivuko ndiyo hivyo tena hakuna

  Na barabara ya Maromboso Mahakamani,na ya Kilombero sokoni kuelekea kwa Babu kanisani ni maeneo ambayo kuna mkusanyiko wa watu kama hapo Kilombero sokoni, na kanisa la Lutheran na Kwa Babu.

  Kwa ujumla naweza sema maamlaka husika haijali usalama wa waendao kwa miguu na zaidi hata alama zilizopo hazitoshi kwa barabara za Arusha na hat zilizopo hakuna anayezirekebisha kwa wakati.

  Mamlaka husika isifumbie macho kwenye hili kwani watu wengi wamepoteza maisha wengine nikiwashuhudia kwa macho yangu mawili,watekeleze wajibu wao.
   
 2. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #2
  May 6, 2011
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Best! Hata nami inaniboa sana!!
   
 3. M

  Mary Chuwa Senior Member

  #3
  May 7, 2011
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 178
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Ni kweli Liverpoolfc,hizo barabara za Arusha wahusika wala hawaoni umuhimu wa waendao kwa miguu kabisa.
  Wahusika wao sababu ni kujikalia tu huko maofisini hawana wanachofanya ukaona matokeo yake,barabara za katikati ya mji zina mashimo utadhani wanataka kuvuna maji ya mvua.
  Kwa kweli inanikera sana.
  Halafu ndiyo unaitwa mji wa Kitalii pamoja na vivutio vyote hivyo Barabara zake ni hovyo kabisa
   
 4. Bushbaby

  Bushbaby JF-Expert Member

  #4
  May 7, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 1,577
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 145
  Hivi mhandisi wa barabara Arusha akili yake ipo kichwani? Wanaweka zebra cross juu ya tuta..... kwa ufahamu wangu mdogo nafikiri zebra cross inatakiwa ikae katikati ta matuta mawili moja kushoto na jingine kulia
   
 5. S

  Stuxnet JF-Expert Member

  #5
  May 7, 2011
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,016
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Arusha kwa barabara bado haiko vizuri. Pamoja na ubora wa majjengo na uchumi unaotegemea utalii na madini bado Jiji la Arusha liko sawa na Manispaa za Sumbawanga, Morogoro na Jiji la Mbeya. Tanga na Kilimanjaro ziko mbali kwa hili
   
 6. Ciril

  Ciril JF-Expert Member

  #6
  May 7, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 5,536
  Likes Received: 1,468
  Trophy Points: 280
  Mpaka watu wagongwe wafe ndio Serikali itaamka
  kama kawaida yao lazima wakurupuke,watendaji wa Manispaa ya Arusha ni wazembe sn na waweza kwenda kuulizia vp ukaambiwa pesa zilishatoka na zilipoelekea hawajui....go to he'll ccm
   
Loading...