Barabara yaweka rehani ubunge wa Dr. Mwakyembe 2015... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Barabara yaweka rehani ubunge wa Dr. Mwakyembe 2015...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwakiluma, Mar 24, 2012.

 1. Mwakiluma

  Mwakiluma Senior Member

  #1
  Mar 24, 2012
  Joined: Jan 23, 2012
  Messages: 120
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Katika analysis yangu katika jimbo la kyela wananchi wanasema huenda ukawadia mwisho wa ccm katika jimbo la kyela mara itapofika mwaka 2015 huku barabara ya kyela-ipinda-matema haitakuwa imejengwa kwa kiwango cha lami...tangu kuanza kwa mfumo wa vyama vingi na uchaguzi wa kwanza mwaka 95 wabunge wa CCM wamekuwa wakiahidi kuijenga barabara hiyo lakini hakuna kilichofanyika.
  Mbunge wa kwanza alikuwa Kasyupa, akaja akaja mwakipesile na sasa Mwakyembe wote wametoa ahadi hizohizo...
  Katika kampeni zake Mwakyembe aliwaambia wananchi wa kyela kuwa wampigie kura Kikwete kwa sababu amemwahidi kuijenga barabara hiyo.
  Katika maelezo yake bungeni Mwakyembe alisema hawezi kudai ujenzi wa barabara ya wilaya wakati barabara za mikoa katika mikoa mingine bado hazijajengwa kauli ambayo ilileta minong'ono mingi miongoni mwa wananchi wa kyela...
  Katika kata za Talatala, Ipinda, Lusungo, Makwale na Matema wamesema watalazimika kufanya mabadiliko iwapo barabara hiyo haitajengwa.
  Hata baada ya kupewa unaibu waziri wa ujenzi wananchi wengi wa kyela wamekuwa wakiweka matumaini mengi kwa Mwakyembe lakini hadi hivi sasa ikiwa imebakia takribani miaka mitatu ya ubunge wake hakuna kilichofanyika.
  CCM haina ushawishi wa kichama katika jimbo lolote lile bali kimebaki na ushawashi wa mtu binafsi tu,hivyo iwapo wananchi wa kyela wataamua kuachana na mwakyembe jimbo hilo litakwenda kwa upinzani maramoja...mathalani katika kata ya ipinda tayari chadema kilishapata diwani katika uchaguzi wa 2010 na katika kata nyingi kama ile ya makwale ccm ilipata upinzani mkubwa...vijiji vingi vya talatala, tenende, ipinda, kafundo, ikulu, bwato, lupaso, lukama, mpanda lusungo, kisale, mpunguti, makwale na matema vinapata usumbufu mkubwa wa usafiri ikiwemo gharama kubwa za usafiri kutokana na ubovu wa barabara....Mwakyembe itambidi afanye jithada kubwa kuweza kujenga barabara ile ili kuongeza ushawishi..HAKUNA MAENDELEO KATIKA JIMBO LA KYELA NA MWAKYEMBE AMEKUWA MTU WA KYENYE MAGAZETI TU NA SIO MAENDELEO YA JIMBO LA KYELA...HAELEWANI NA WATENDAJI WENGI WA JIMBO HILO.
   
 2. kookolikoo

  kookolikoo JF-Expert Member

  #2
  Mar 24, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 2,537
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Chochote chawezekana. Miaka mitatu ni mingi.
   
 3. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #3
  Mar 24, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Mwaka Gellete! Ni nouma!
   
 4. Malafyale

  Malafyale JF-Expert Member

  #4
  Mar 24, 2012
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 11,214
  Likes Received: 3,626
  Trophy Points: 280
  Mwakyembe amekwisha tangaza kuwa HATAGOMBEA TENA JIMBO LA KYELA MWAKA 2015 na aliyasema haya mbele yetu alipokuja KASUMULU mwaka jana na kukumbana na upinzani mkali wa watu kumpigia mayowe kuwa HATUKUTAKI na yeye kuwajibu wapiga kura kuwa MM NI MTU MKUBWA SERIKALINI NA ANGALIENI MNAONIZOMEA MTAISHIA JELA!

  Jimbo nalichukua kiurahisi kabisa mwaka 2015 na kila mwana Kyela analijua hilo!Mwakilama njoo kijijini kwangu Butangali uone mikakati!
   
 5. Mwakiluma

  Mwakiluma Senior Member

  #5
  Mar 24, 2012
  Joined: Jan 23, 2012
  Messages: 120
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  unagombea kwa chama gani?...niambie chama ili nikuunge mkono na nikuombee kura katika kata za ipinda, lusungo na matema..
   
 6. wwww

  wwww JF-Expert Member

  #6
  Mar 24, 2012
  Joined: Mar 20, 2012
  Messages: 350
  Likes Received: 204
  Trophy Points: 60
  Ingawa ni Kweli kuwa Kyela wananchi hawaoni maendeleo kipindi cha Mwakyembe na hasa barabara ya njia panda - Ipinda - Matema Beach. Lakini nawatahadharisha wananchi wasikurupuke kushawishiwa kirahisi ila wafanye maamuzi ya busara.


  Si lazima Mwakyembe agombee, lakini wawe makini kumpata mtu wa kumbadili Mwakyembe. Kuna vijana wengi wazuri na wenye uchungu wa maendeleo ya Kyela mfano mdogo; ni kijana mmoja anaitwa Africar T Kagema anaishi Dar-es-Salaam.


  Huyu kijana nilikutana naye mwezi Desemba, 2011 alichonieleza kuhusu mikakati ya kuiendeleza Kyela kwa kweli inatia matumaini ingawa alikuwa anasimulia tu. Aliongeza kuwa ili kuhakikisha anawasaidia wananchi wake wa Kyela yuko mbioni kutoa kitabu kinachoitwa ''KYELA YA LEO NA MAGEUZI YA KESHO''

  Hivyo nawasihi wakyela kutafuta mtu makini na mzalendo.
   
 7. l

  lijumbete Member

  #7
  Mar 24, 2012
  Joined: Jan 22, 2011
  Messages: 52
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 15
  MANENO hayasaidii kutekeleza mikakati ya kuikomboa kyl, maana kuna changamoto nyingi kukubwa msianze kupigiana debe mara oh AFRICA anafaa oh mara kijana, huyo africa anakaaa dar na anaona uchungu wa kyl akiwa dar na kuandika vitabu ambavyo ataviuza na kujineemesha yeye maana hawezi kuvitoa bure, KUNA mambo msifanye kama mnakurupuka lazima mbunge wa kyl awe na stamina ya kutetea jimbo lake.PERSONAL NIMEWAH SIKIA TAARIFA ZA AFRICA NI MTU anayependa madaraka mno kila kikundi akianzisha anapenda sana kuwa kiongozi mtu wa namna hiyo hafai maana yeye shida yake ni kutawala tuu kama ilivyo kwa mwakyembe. NAwashauri kama kweli mna nia ya dhadi fanyen mambo ya maana jitoleeni kufundisha, kaeni vijiji mjue shida za wananchi sio mnaandika vitabu wakati hata nyie wavivu kusoma, kyela is NO LONGER SHAMBA LA BIBI
   
 8. wwww

  wwww JF-Expert Member

  #8
  Mar 24, 2012
  Joined: Mar 20, 2012
  Messages: 350
  Likes Received: 204
  Trophy Points: 60
  Kwani kama ana vision, uwezo wa kuongoza watu kiakili, kiubunifu, kizalendo na ana uchungu kuna ubaya gani akiwa mbunge?

  Tambua kuwa Kyl inakabiliwa na matatizo na changamoto nyingi, hivyo inahitaji mtu mwenye fikira, ubunifu na mikakati mipya ili kukabiliana na changamoto zilizopo.

  Kyl haikabiliwi na tatizo la barabara ya Njia panda - Ipinda - Matema Beach tu, bali kuna matatizo kama;

  1. Elimu - Kidato cha Tano na sita shule moja ya binafsi (Dennob High School), lakini sekondari kama za Ipinda, Matema Beach, Kyela ambayo inasuasua na hata Itope zinaweza kuanzisha High level. Hakuna chuo hata kimoja, hata cha ualimu au ufundi tu.
  2. Maji - Kuna Mamlaka mbili tu za maji (Kyela Mjini na Kasumulu)ambazo hazitoshi kuhudumia vijiji zaidi ya 100 vilivyopo Kyela
  3. Afya - Kuna Hospitali moja tu (Chakavu) ya Serikali Kyl mjini ambayo haina vifaa vya kutosha vya kutolea huduma kwa madaktari, Wananchi wanalazimika kwenye Matema Beach kwenye Hospitali ya Mission au Tukuyu.
  4. Kilimo - Kilimo chenyewe ni cha msimu tu, hakuna mikakati ya kuanzisha kilimo cha Umwagiliaji kwa kutumia mito ya Kiwira, Songwe, Mbaka, Lufilyo na hata Ziwa Nyasa.
  5. Miundombinu - Bandari ya Itungi imetelekezwa, Ofisi za Halmashauri na Mkuu wa Wilaya ni chakavu zote.
  6. Ardhi - Ardhi yenyewe ya Kyl ni ndogo lakini imetekwa na walowezi.
  7. Watoto - Wanakosa haki zao za msingi kama Elimu, Afya na Maji kwavile wengi wanaishi kwenye mazingira magumu.
  8. Vijana - Hawana ajira, biashara zao za Malawi hazina tija kwa sasa, hawana pa kukopea mikopo kwa ajili ya biashara zao na hata kilimo kwa vile wanategema benki moja tu (NMB),pia hawana soko la uhakika. Wanatangatanga tu.
  9. Wazee - Utadhani hawana watoto, kwani kila mzee anaishi kivyake, hakuna anayeweza kuwaunganisha ili kuwatafutia misaada inayowafaa.
   
 9. Cha Moto

  Cha Moto JF-Expert Member

  #9
  Mar 24, 2012
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 945
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Nimeamua kuachana na ubebaji maboksi huku ughaibuni nakuja KYELA kugombea ubunge 2015.
  Kaja ketu tyesa, natangaza nia mapema mwakani narudi kuishi Kikusya!
   
 10. l

  lijumbete Member

  #10
  Mar 24, 2012
  Joined: Jan 22, 2011
  Messages: 52
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 15
  MMHHH haya bwana siasa wote mnaziendesha kwa kulalamika, but I can assure u matatizo hayo yaliyopo hayahitaji mtu mjanja mjanja katika kuyashughulikia msije mkazaa mtu anayepinga ufisadi mwingine, Haitoshi kuhitaji A level school wakati O level hawafaulu nani atakuja kusoma hizo shle. Mimi msimamo wangu ni kuwa wana kyl wote tuungane kuzikabili hizi changamoto hata ukiwa nje ya uwanja, Baadhi tunafanya baadh ya research huko tukiwa likizo na kuja na vijisuluhisho kwa pale tunapoweza, huyo africa anasubili ubunge ndo ajue kwanini watoto wanafel??? si atajipanga mwaka mzima. Unajua kwanini kuna failure rate kubwwaa?? sasa watu tumepiga tempo huko na kukaa na madent na kujua ubovu ni nini . Kama mnataka kuikomboa kyl sio kila kitu kukimbila siasa we can even discus those issues hata kama sio wabunge na tukafanya yaliyo ndani ya uwezo na yaliyo nje tusubili hizo siasa za JOPE AKAGELEPOOOO,, njoo kyela member fb u welcome au mnaweza kuwa mpo but mnaogopa chngamoto kule msipinge ufisadi tutawarushia mawe we need kaziiii
   
 11. tindikalikali

  tindikalikali JF-Expert Member

  #11
  Mar 25, 2012
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,883
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 135
  embombo jilipo!
   
 12. Teacher1

  Teacher1 JF-Expert Member

  #12
  Mar 25, 2012
  Joined: Jan 29, 2011
  Messages: 313
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Uvivu, ubishi na kupenda vya bure ndo tatizo lenu ninyi watu wa kyela hata akija malaika Gabreil kuwa mbunge wenu bado hataweza kuwafaa.Hadi sasa nadhani ni moja ya wilaya inayoongoza kwa kubadili wabunge mara nyingi kuliko wilaya nyingi nchini lakini bado mnalalamika. Hiyo barabara ijengwe kiwango cha lami ikiwa na manufaa gani kiuchumi au mnataka iwe barabara nzuri muendeshee vibaskeli vyenu vya mitumba? Ni kweli mnahitaji mabadiliko lakini anzeni kubadilika tabia zenu wenyewe mnaongoza kwa majungu Tanzania wanawake wenu kila siku ni sikukuu kutwa wameulamba watafanya kazi saa ngapi za kuwaletea maendeleo? Mnaomboleza msiba mwezi mzima sasa ikitokea misiba mitatu kijijini ina maana mwaka huo hamtavuna vimpunga vyenu maana mtalala msibani miezi yote.

  Hamtaki mabadiliko pamoja na kuwa na mpunga mzuri kuliko mwingine nchini lakini mnaendeleza kilimo cha kumwaga mbegu kilichoandikwa katika biblia enzi za Yesu kristo. Anzeni kubadilika wenyewe na muombeeni mbunge wenu apone maana amepigana sana kwaniaba ya watanzania, mshaulini atoke huko kwa magamba aende kwenye upande wanaoelewa athali za ufisadi.
   
 13. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #13
  Mar 25, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,327
  Likes Received: 1,793
  Trophy Points: 280
  Ingawa ubwana mkubwa pamoja na system za u chief ziliondolewa Tanzani watu wa Kyela kama bado wanaziendekeza sana. Hakuna mtu wa kupeleka maendeleo kule kama wao wenyewe hawaoni sababu ya kufanya hivyo. Mbunge ajaye lazima ahakikishe anafikiria nje ya mstari huo.
   
 14. tindikalikali

  tindikalikali JF-Expert Member

  #14
  Mar 25, 2012
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,883
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 135
  kumbe tunaongoza kwa majungu na ubishi? Sikulijua hili...
   
 15. Mwakiluma

  Mwakiluma Senior Member

  #15
  Mar 25, 2012
  Joined: Jan 23, 2012
  Messages: 120
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Ninamashaka kama wewe umeishi kyela muda mrefu na ninawasiwasi kama wewe unaijua vizuri barabara hiyo ambayo unasema haina manufaa.
  Kwa ufupi mimi ni mwandisi kwa elimu katika mambo ya ujenzi wa barabara...moja ya kazi kubwa ya barabara ni usafirishaji wa mazao na watu. Kyela kuna kilimo kikubwa cha mpunga bei ya zao hilo ni chini na haliwakomboi wananchi kutokana na ubovu wa barabara hiyo inayoongeza gharama kubwa za usafirishaji, Matema beach ni eneo zuri sana la utalii lakini kutokana na ubovu ya barabara hiyo utalii umedorola kwa kiasi kikubwa. Huduma za umeme zinadolora kutokana na ubovu wa barabara hiyo, maendeleo sehemu yoyote ile duniani hutegemea sana ubora mzuri wa barabara...kipimo kimojawapo cha maendeleo sehemu yoyote ile hupimwa kwa barabara....tungekuwa na barabara nzuri kungekuwa na maendeleo na tungevutia sana walimu kwenda kufundisha katika shule zetu na kuongeza ufaulu katika shule zetu.mimi nadhani kwa jimbo la kyela "BARABARA KWANZA"
   
 16. Malafyale

  Malafyale JF-Expert Member

  #16
  Mar 25, 2012
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 11,214
  Likes Received: 3,626
  Trophy Points: 280
  Nitagombea kwakupitia upinzani!Mm siwezi kuwa CCM kamwe chenye sera zilizoshindwa!Kwa sasa nipo nje ya TZ kikazi lkn nashuka Ngonga hivi karibuni;CCM ipende isipende Kyela inachapwa mwaka 2015!
   
 17. Gwankaja Gwakilingo

  Gwankaja Gwakilingo JF-Expert Member

  #17
  Mar 25, 2012
  Joined: Jan 26, 2012
  Messages: 1,963
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Nitakuja huko kutoka masoko ili nikupigie kura endapo tu utagombea kwa tiket ya CDM,nijulishe mapema Comrade
   
 18. Malafyale

  Malafyale JF-Expert Member

  #18
  Mar 25, 2012
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 11,214
  Likes Received: 3,626
  Trophy Points: 280
  Afrikar Kagema nilisoma nae Itope katikati ya miaka ya 90 na kwa mara ya mwisho niliambiwa yupo jeshini;tafadhali www kama una mawasiliano na mtu huyu niandikie chemba namba yake niongee nae;Kagema ni mmoja wa wanamapinduzi wa awali kushtukia utapeli wa CCM-Kyela!
   
 19. Mwakiluma

  Mwakiluma Senior Member

  #19
  Mar 25, 2012
  Joined: Jan 23, 2012
  Messages: 120
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Gombea kupitia CDM Ili nikuunge mkono..naamini kabisa kuwa ukombozi wa kweli ndani ya kyela hautatoka ndani ya ccm..
   
 20. trachomatis

  trachomatis JF-Expert Member

  #20
  Mar 25, 2012
  Joined: Jun 7, 2011
  Messages: 3,653
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 145
  Watabadilisha sana Wabunge,na wala barabara hiyo haitajengwa!

  Mark my words..
   
Loading...