Barabara ya Ntyuka Dodoma inatia aibu

Barabara ya Ntyuka Dodoma inatia aibu

Joined
Dec 8, 2018
Posts
12
Reaction score
5
Hii barabara ni Km 5 tu kutoka Dodoma Mjini na inaenda katika hospitali kubwa kama DCMC na MVUMI. Imejaa vumbi na mashimo hata barabara za vijijini zina afadhali.

Viongozi wa mtaa, kata mmeshindwa hata kufukia mashimo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bado tu haijajengwa?
Yaani pamoja na kuwa inaelekea hospitali kubwa ya macho nchini ya Mvumi pamoja na Dodoma Christian Medical Centre - DCMC - hospitali ya kubwa iliyopigiwa debe sana na Mwamasika,serikali haijaona umuhimu wake kweli!?
 
Nilikuwa pale UZUNGUNI majuzi wakati nafuatilia habari Fulani hivi kuhusu Ndugu zangu Wagogo.

Nilipopata fursa ya kuelekea Mvumi Hospitali ( Hospitali kubwa kwa ajili ya tiba ya Macho ) nilishangaa sana kuona jinsi njia hiyo inayopita Ntyuka ilivyo mbaya.

Mamlaka husika zinatia aibu kiukweli.






Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni moja wapo ya barabara ambazo ziko kwenye mpango wa kuwekwa lami ingawa sijajua itawekwa lini...
 
Wajawazito tunaopenda kujifungulia DCMC cha moto huwa tunakiona
 
Hii barabara ni Km 5 tu kutoka Dodoma Mjini na inaenda katika hospitali kubwa kama DCMC na MVUMI. Imejaa vumbi na mashimo hata barabara za vijijini zina afadhali.

Viongozi wa mtaa, kata mmeshindwa hata kufukia mashimo?

Sent using Jamii Forums mobile app
Tunaishukuru serikali ya awamu ya 5 kwa hiyo barabara ya Ntyuka. Hakika hatujawahi kupata serikali yenye kujali wanyonge kama hii ya awamu ya 5 tangu tupate uhuru.

Ubovu wa hiyo barabara na uvumilivu wa wanyonge wanaoitumia ni kielelezo cha uzalendo wa wanyonge wa Ntyuka na huko Dodoma. Ni matumaini yetu mwaka huu October kwenye uchaguzi mkuu wanyonge wazalendo wa Ntyuka na Dodoma mtaichagua tena serikali ya Magufuli ili muweze kuendelea kuwa wanyonge huku yeye akijinasibu kuwatetea.

Hiyo inaitwa win-lose situation.Wao ccm na chama chao cha kutetea wanyonge wanaendelea kuneemeka huku nyie wanyonge wa Ntyuka mkiwa mtaji wao wa "kula".
 
Waziri Mkuu Mstaafu naye anapita hapo akielekea kwao Mvumi kwa miaka nenda rudi sembuse nyie ambao ni wakuja? Tuacheni Sisi Wagogo tumeizoea

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kiukweli hali inatisha na sijui kwanini serikali imekalia mambo ambayo yananufaisha mwananchi mmoja mmoja badala ya kufanya mambo yatayo nufaisha watanzania wote kitu kama barabara haswa zinazoelekea kwenye huduma za jamii zafaa zipewe kipau mbele na si kingine

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wagogo hawanufaiki na serikali za ccm lakini ni wapigakura wazuri na watiifu kwa ccm. Badilikeni
 
Umetumwa na mabeberu mwenzako aliyeripoti habari Kama hii kuhusu ngorongoro kashapewa kesi jiandae
 
Hii barabara ni Km 5 tu kutoka Dodoma Mjini na inaenda katika hospitali kubwa kama DCMC na MVUMI. Imejaa vumbi na mashimo hata barabara za vijijini zina afadhali.

Viongozi wa mtaa, kata mmeshindwa hata kufukia mashimo?

Sent using Jamii Forums mobile app
Wewe umetumwa na mabeberu huu ni uhujumu uchumi hatutakubali
 
Kesho utasikia mkuu wa mkoa,anaagiza polisi wakusake ukamatwe mala moja na kufunguliwa kesi ya uhujumu uchumi,kwani hukumsikia leo nduguyenu Gambo ametoa amri ya kumsaka aliyetoa picha na kusambaza kwenye mitandao juu ya barabala ya Ngorongoro kuwa mbovu.
 
Back
Top Bottom