Barabara ya mandela | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Barabara ya mandela

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Raia Fulani, Nov 28, 2009.

 1. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #1
  Nov 28, 2009
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Kumekuwa na ubabaishaji mkubwa wa matrafiki katika hii njia hasa kama unaenda ubungo. Trafiki wamekuwa wanapendelea sana njia zingine kuliko hii. Unaweza kuwa uko hapo landmark lakini ikakuchukua nusu saa kufika mataa. Hii ni kero. Afande kombe ongea na vijana wako ili wawe fair katika kuruhusu magari kwani wote tunahitaji kuwahi tuendako
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Nov 28, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Kuna mtaalamu mmoja wa Saikolojia anasema kwamba ukienda benki, basi foleni utakayochagua kusimama utaona kama vile haiendi, imesahaulika.

  Ukihamia inayoenda, basi ghafla nayo inakwama kabisa, na teller anatoka kabisa kibandani pale, na unatamani usingehama!

  Angalia isije ikawa haraka zako zikawa zinakuadhibu kisaikolojia, kumbe mambo yote yako sawa!
   
 3. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #3
  Nov 28, 2009
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  hapana. Ile njia inabaniwa sana. Ya morogoro inapendelewa zaidi
   
 4. Serendipity

  Serendipity JF-Expert Member

  #4
  Nov 29, 2009
  Joined: Jan 24, 2009
  Messages: 475
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Hivi huwa najiuliza zile taa kazi yake ni nini? maana utakuta kuna taa za kuongozea magari lakini kuna trafiki amesimama anaongoza magari! hivii hii kitu inatokea kwenye nchi nyingine au ndo utamaduni wetu wabongo?
   
 5. paesulta

  paesulta JF-Expert Member

  #5
  Nov 29, 2009
  Joined: Mar 13, 2009
  Messages: 227
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  inatokea sehemu nyingi tu,kwani mantiki nzima ni kuwa say kama Morogoro road haina msululu basi kama ingekuwa taa pekee ingechelewesha wa Mandela rd.lkn akiwa traffic hapo angeruhusu magari mengi ya Mandela ambako say kuna foleni kubwa zaidi.........
   
 6. Mlango wa gunia

  Mlango wa gunia Senior Member

  #6
  Nov 29, 2009
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 123
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Tutalaumu matrafiki bure,suluhisho la foleni ni madaraja au mahandaki ili gari zinazotoka opposite direction zisiwe zina interfere,suala la foleni halijapewa kipaumbele na wizara ya miundo mbinu na hivyo kuwaongezea kazi wizara ya mambo ya ndani na ndio maana tunalalamikia traffic police sasa
   
 7. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #7
  Nov 29, 2009
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  In actual fact tatizo lipo pale junction ya ubungo.
  Junction hii imekuwa overloaded na trafficpande zote.(traffic kwa maana ya magari-technical term).
  Junction hii ilipokuwa designed ilikuwa kwa ajili ya magari machache tu toka pande zote.
  Sasa hivi junction ya Ubungo si ajabu ndio the busiest nchini Tanzania, na sasa inahitaji redesign ilitraffic flow iweze kuwa contained.
  Tetesi zilizopo ni kuwa kuna mradi utakaofadhiliwa na Serikali ya Japan ili ijengwe flyover kwa junctions za Ubungo, Tazara,Temeke -Machinjioni, na hata Magomeni.
  Pengine mifumo hii itapunguza jammimg ya junctions jizi.
   
Loading...