Charles Mkubya
JF-Expert Member
- Aug 27, 2009
- 206
- 161
Jana nilipokea simu toka kwa Milard Ayo wa Clouds Media akinitaarifu nimekua mshindi katika moja ya michezo ya kubahatisha....TZS bilioni 1.
Akaniuliza swali moja “utaifanyia nini hii pesa??” Nikamwambia kwa adha ya barabara ninayopata, najitolea pesa yote hii itumike kwa ujenzi wa barabara ya Kitunda mpaka Magole mwisho. Kwa kuwa nilikua live clouds fm, zikapigwa simu nyingi kudhibitisha adha ya wakazi wa Magole na Bonge wa kipindi cha PB nae akadhibitisha hili..
Ukazuka mjadala mrefu na kizuri zaidi simu zikandelea kupigwa na katika watu wachache naokumbuka walipiga simu alikua mkuu wa Toyota Tanzania akisema nimetumia pesa nyingi kununua vipuli vya gari yangu (spare) sababu ya ubovu wa barabara hivyo anachangia kiasi cha pesa...., Mh mkuu wa mkoa, kaka yangu Makonda akachangia sehemu ya fedha huku akitoa maelekezo kwa wizara husika....Mh Lukuvi akajitolea kuchangia akisema itasaidia kuboresha makazi ya watu wa Magole, tukapata baadhi ya wakandarasi waliojitolea vifusi na kokoto na ndani ya dakika 30 tukawa na kiasi cha Bilioni 5.
Dakika za mwisho mkuu mwenyewe akapiga simu kushukuru kuona wananchi wanajitolea kusaidia serikali katika utatuzi wa kero zinazowazunguka na akauliza kama nina ombi lingine zaidi. Nikamwambia, “Mheshimiwa kwa sasa natamani hii barabara tu ikamilike na kama itakupendeza, hii kazi na pesa zote zilizopatikana apewe Kamanda Charles Mbuge, Brig Generali yule mahiri wa kusimamia ujenzi aisimamie...” wakati nasubiri mkuu atajibu nini, nikihisi labda nimekosea protocal........alarm ya simu ikaniamsha....kumbe nilikua naota tu usingizini🤦🏽♂️🤦🏽♂️🤦🏽♂️.
Natamani ndoto hii iwe kweli siku moja. Mungu ibariki Tanzania.