Barabara ya Kibada - Vijibweni serikali itupie macho

vngenge

JF-Expert Member
Apr 19, 2011
539
270
Sisi wakazi kigambo, kibada, toangoma mikwambe Na maeneo mbalimbali tumechoshwa Na hali mbaya ya Barbara hii muhimu ya kilomita 3.9.

Barbara hii ni muhimu kwani ni kiunganishi kati ya hospital ya kisiwani na wakazi wa kibada Na maeneo mengine tajwa kuelekea daraja la Nyerere. Pia kiuchumi malori mengi yanachukua mafuta toka depots hutumia Barabara hii kuzungukia kongowe. Barabara imekuwa na mashimo mengi, vumbi na kusabisha uharibifu wa magari na kuhatarisha usalama.

Kutokana na umuhimu wake na kwakuzingatia kauli mbiu ya serikali yetu ya HAPA KAZI TU tunaziomba mamlaka husika kutekeleza kaulimbiu hii kwa vitendo katika kutatua kero zinazotukabili sisi wananchi walipa kodi Na wapiga kura. Kwakweli hali ni mbaya sana hasa unapohitaji kumuwahisha mgonjwa au mjamzito hospitality ya kisiwani.
 
WANA MPANGO WA KUHAMIA DODOMA UNAFIKILI WATAKUSIKILIZA? Jibu utakalopewa tunahamia Dodoma; watu hawana barabara nyie mnahama Kwa bajeti ipi? Yaani Tanzania ukiitafakali waweza patwa na wendawazimu.
 
Naunga mkono hoja, na ikifika Kibada ujenzi uendelee mpaka Tundwi-Songani.
Mkurugenzi na mkuu wa wilaya mpya ya Kigamboni, miundo-mbinu ya barabara na usambazaji wa umeme viwe kipaumbele chenu tafadhali.
 
Sisi wakazi kigambo, kibada, toangoma mikwambe Na maeneo mbalimbali tumechoshwa Na hali mbaya ya Barbara hii muhimu ya kilomita 3.9.

Barbara hii ni muhimu kwani ni kiunganishi kati ya hospital ya kisiwani na wakazi wa kibada Na maeneo mengine tajwa kuelekea daraja la Nyerere. Pia kiuchumi malori mengi yanachukua mafuta toka depots hutumia Barabara hii kuzungukia kongowe. Barabara imekuwa na mashimo mengi, vumbi na kusabisha uharibifu wa magari na kuhatarisha usalama.

Kutokana na umuhimu wake na kwakuzingatia kauli mbiu ya serikali yetu ya HAPA KAZI TU tunaziomba mamlaka husika kutekeleza kaulimbiu hii kwa vitendo katika kutatua kero zinazotukabili sisi wananchi walipa kodi Na wapiga kura. Kwakweli hali ni mbaya sana hasa unapohitaji kumuwahisha mgonjwa au mjamzito hospitality ya kisiwani.
Ni kweli mkuu hii barabara Ni shida Sana wiki iliyopita nilipo ingia Tu pale kutokea Kibada stand nikaona mshale wa kuonyesha speed umelala haufanyi kazi nilipoenda kwa Fundi nikakuta ABS spare zimedondoka. Siku hizi napita asbh kwenda kazini kurudi nazungukia feri
 
Back
Top Bottom