Barabara ya 12, Tanga: Inadaiwa Polisi na Zimamoto wamempiga mtu mmoja aliyesaidia kuzima moto

pye Chang shen

JF-Expert Member
Jul 11, 2016
11,038
5,259
Inasemekana nyumba ya jirani ilikuwa inaungua, na huyu jamaa nyumbani kwao kuna kisima cha maji so akajitolea pamoja na wasamaria wengine kuchota maji na kuzima moto huo, huku wakipiga simu taasisi ya zima moto kwa ajili ya msaada zaidi.

Bahati mbaya fire brigade wakachelewa kufika hadi moto umezimwa, kwa hiyo walipofika wananchi wakaanza kuwapopoa kwa mawe, na wao wakaanza kupiga wanachi labda kwa kujihami.

Ila kilichowakera wengi ni kwenda kumpiga mtu ambaye hakuwepo kwenye kundi linalorusha mawe na ni mtu ambaye ametoa mchango mkubwa sana wa mali na nguvu zake katika kuuzima moto huo.

Inasemekana ameumia sanaa ndani kwa ndani na baadhi ya wakubwa na viongozi waliopo hapo wamempa 30,000/= tsh ili akajitibie huku wakimuomba msamaha.

Sasa swali je, hii ni haki?

Na inasemekana kuna waliosema watamrudia wamkomeshe yaani maisha yake yapo hatarini
Sijui tumsidieje huyu mtu mwema
Msaada tafadhali wa maoni tu
 
Kichwani mzima kweli?? Mbona heading umetaja Polisi na wanajeshi ila ktk contents haujawataja hao watu umetaja askari wa fire???
 
Umesema alikua hausiki kwenye kurusha mawe na hausiki kwenye ugomvi na kisima kipo nyumbani kwake inamaanisha alikua kwake kwahiyo polisi wamemfata kwake ndio nimeuliza hapo
Ndio hahusiki kwa namna yeyote kwenye kurusha mawe ila alikuwa anhusika kwenye kuzima moto, maji yanatokea kwao yaani oppisite ya nyumba inayoungua so ndio kisanga kikamkuta
 
Ndio hahusiki kwa namna yeyote kwenye kurusha mawe ila alikuwa anhusika kwenye kuzima moto, maji yanatokea kwao yaani oppisite ya nyumba inayoungua so ndio kisanga kikamkuta
Asee vitu kama hivyo inatakiwa wananchi mmalizane na hao npolisi hapo hapo ikiwezekana pigeni ila mkiwaacha kama hivyo polisi wanabebana sana kesi itaisha juu juu tu Mkuu.
 
Kichwani mzima kweli?? Mbona heading umetaja Polisi na wanajeshi ila ktk contents haujawataja hao watu umetaja askari wa fire???
Akikujibu ni tag na mimi yawezekana kuna mengine amesahau kuandika.
 
Kichwani mzima kweli?? Mbona heading umetaja Polisi na wanajeshi ila ktk contents haujawataja hao watu umetaja askari wa fire???
Mkuu tulia kwanza,
Kwenye uzi kasema anasikia, kwahiyo taarifa sio rasmi na bado sio kamili.
 
Hivi moderators yaani mnaacha mada kama hizi kweli! Wakati mtu ameandika kabisa neno "naskia" kwa maana hana uhakika wala hajashuhudia tukio.
 
Umesema "unasikia" hivyo taarifa yako haina ushahidi.
Tafuta kwanza ushahidi wa kutosha ndo uilete taarifa yako ikiwa na ushahidi ulio kamilika
 
Hivi moderators yaani mnaacha mada kama hizi kweli! Wakati mtu ameandika kabisa neno "naskia" kwa maana hana uhakika wala hajashuhudia tukio.
Tukio lipo, ushahidi upo, ni suala la muda tu,
Ni kwa kuwa mpaka sasa
Ila uhakika utwepo hapa
 
Back
Top Bottom