Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 48,671
- 149,843
Habari wadau,
Kwa muda mrefu sana hapa maeneo ya Sinza kuna msikiti mmoja (jina nalihifadhi) ambao umefungwa loudspeaker kwa nje hivyo wakianza Ibada zao basi inakuwa ni kero sana kwa sisi tunaoishi jirani na msikiti huu.
Kwa mfano,kila siku ikifika saa 2 kamili usiku wakati wa taarifa ya habari nao huanza ibada na kutulazimisha tuongeze sauti za tv ili tuweze kusikiliza taarifa ya habari vinginevyo haiwezekani.
Pia, ikifika Ijumaa muda kama huu hali ni hiyo hiyo ila bahati tu leo muda huu umeme umekatika ghafla nao imewabidi wasali bila kutumia hizo loudspeaker ingawa walishaanza kuzitumia.
Ukiacha misikiti,hata kuna makanisa ambayo nayo yako katika makazi ya watu na yamefungwa vipaza sauti ambavyo hugeuka kero kwa watu wanaoishi jirani na makanisa hayo pale waumini husika wanapokuwa kwenye ibada zao au wanapopiga nyimbo za Injili.
Nachojuiliza hivi sheria za mipango miji na sheria za nchi kwa ujumla zinaruhusu mambo haya yote?
Hii noise polution katika makazi ya watu mpaka lini?Kuna wagonjwa na watu wenye matatizo mbalimbali ambao hizi kelele ni mateso makubwa kwao hivyo tubadili huu utaratibu wa kufanya ibada kwa kutumia vipaza sauti.
Serikali tazameni upya jambo hili ambalo pengine ni kero kama ilivyo mziki wa bar.