NIMESULIDE:
Painkiller, fever. Reason for ban: Liver failure.
Brand name: Nise, Nimulid
Hii nimewahi kuitumia zaidi ya mara mbili tena kwa prescription ya Daktari. ni muhimu pia kuwafikishia na wenzetu ili wafahamu hizi dawa hazifai. dah sijui kama ini langu limenusurika
Pole sana ndugu yangu. Mara nyingi sisi watumiaji wa haya madawa tunakuwa aidha si wenye kufahamu kama dawa tulizo andikiwa kuwa zina madhara au tunawaamini sana madaktari wetu au tunakuwa hatuna budi kutumia. hususan sisi raiya wa nchi daraja la tatu.
Kila dawa ina madhara yake unapoitumia kwa muda mrefu, lakini inapotokea kuwa dawa imepigwa marufuku hii inaonyesha kuwa kuna asilimia kubwa kwa mtumiaji kuathirika katika kipindi kifupi cha matumizi wa hizo dawa alizo andikiwa.
Mfano hii dawa ya Nimulid (Nimesulide) hii ni dawa kutoka marekani (USA). Lakini cha ajabu ndani ya nchi ya Amerikan dawa hii haijawa approved kutumiwa. Vile vile hairuhusiwi kutumia katika nchi zipatazo 160 zikiwemo UK, Australia, Canada n.k.
Na kwa zile nchi zenye kuruhusu matumizi ya dawa hii, wanakupa pale tu maumivu yako ni makali sana au kama una kitu kinaitwa osteoarthritis (baridi yabisi) mara nyingi maumivu haya huwapata wazee. Pia kwa wanawake wenye kupata maumivu makali wakati wa kupata hedhi. Ila hairuhusiwi kwa wenye kuwa na homa na hairuhusiwi kwa vijana chini ya umri wa miaka 12.
Pia kuna dawa nyingine inaitwa Lyrica, hii pia ni dawa ya maumivu, ila haijapigwa marufuku na inatumika sana kutibu maumivu. Dawa hii inamatatizo yake kwanza hairuhusiwi kwa mtu mwenye umri chini ya miaka 18, pia unapotumia unaweza kupata madhara kadhaa yakiwemo:
*Kuongezeka kwa hamu ya kula au kinyume chake.
*Kuhisi kuchanganyikiwa, kushindwa kufikiria vema.
*Kutokuwa na hamu ya kufanya mapenzi, na kutoweza kusimamisha vema.
*Inakufanya husiwe muangalifu.
*Kutoona vizuri, blurred vision au double vision.
*Kuvimba kwa baadhi ya viungo
*kukauka kwa midomo na macho n.k.
*Matatizo ya matumizi ya dawa hii ni mengi lakini inatumika kutibu ugonjwa wa kifafa. Sasa wataalam bado wapo katika kuiangalia. Kama matatizo yatakuwa mengi inaweza kupigwa marufuku lah kama matatizo yatakayo wapata watumiaji ni madogo itaendelea kutumika.
Tuombe Mungu tu tunapotumia haya madawa otherwise hatuna jinsi.