Bank ya Finca Haipeleki Mafao ya Wafanyakazi wake

KISHINDO

JF-Expert Member
Jun 23, 2013
2,147
1,883
Kama kichwa cha habari kinavyosema, kampuni ya finca inayojiita bank haipeleki mafao ya wafanyakazi wake.

Uchunguzi uliofanyika unaonyesha kuwa mara ya mwisho mafao ya wafanyakazi wa finca yalipelekwa mwezi wa nane (8) mwaka jana 2015.

Kuanzia mwezi huo wa nane hadi leo January 30, 2016 hakuna kitu kilichopelekwa katika mifuko mbalimbali ya kijamii ambayo wafanyakazi wake wamejiunga nayo.


Hii kampuni nayo ni jipu kwani imekuwa ikilalamikiwa sana na wateja (kwa kuambiwa hawajalipa marejesho yote wakati wanakuwa wamelipa, hili hutokea kwa wateja wanaotaka mkopo mwingine baada ya kumaliza mkopo wa awali-ukiwauliza maofisa wao wanakwambia system ndo inasema kuwa wanadaiwa) pia malalamiko mengine mengi yako kwa wafanyakazi dhidi ya menejiment ya kampuni hiyo-wafanyakazi wanailalamika kwa kunyanyaswa sana na Mablanch managers pamoja na HR department.

Naiomba Serikali iamke kwa hivi vibenki vibenki kwa sababu kuna mengi sana yamejificha yanayofanyika kuwaibia wateja.



Nawasilisha
 
Back
Top Bottom