sammosses
JF-Expert Member
- Jan 24, 2011
- 1,745
- 1,171
Ule msemo wa wahenga usemao baniani mbaya kiatu chake dawa umendelea kujidhihirisha siku za hivi karibuni mara baada CCM kumpendekeza Dr. Salim Ahmed Salim kuteuliwa mjumbe wa Central Committee wa CCM na kuungana na majeruhi mwingine wa siasa za ndani ya CCM mh.Philip Mangula.
Bila hata ya kuujulisha umma ambao uliaminishwa kuwa Dr. Salim alikuwa muuaji wa kifo cha mwana mapinduzi na mwasisi wa taifa la Zanzibar hayati Abed Aman Karume kama tuhuma zile zilikuwa ni matokeo ya siasa za majitaka na mpango mkakati wa kumwezesha kuingia madarakani bwana mkubwa.
Dr.Salim ndiye yule aliyewahi kuteuliwa kuwa balozi wa Tanzania nchini Misri akiwa kijana mdogo na ndiye yule yule aliyechaguliwa kuwa katibu mkuu wa O.A.U lakini haikujalisha sifa ya utukuka ya uongozi aliyotunukiwa na kuiletea sifa nchi yetu kwa kuchafuliwa na kuitwa muaji.
Watanzania wanashangaa leo hii kuona Dr. Salim pamoja na tuhuma zile mbaya kabisa za kumshushia heshima kwa kiwango kikubwa kwa tamaa ya madaraka wametumia kigezo gani kumsafisha ndani ya jamii husika ilihali jamii ilishaaminishwa.Yuko wapi mzee Hassan Moyo aliyediriki kutumika katika mkakati wa kumchafua mzee huyu Dr. Salim na kuruhusu uteuzi wa mjumbe wa kamati yenye kutoa maamuz makuu ndani ya chama.
Mbona M/Kiti wa CCM taifa hajauweleza umma kuwa tuhuma zile hazikuwa za kweli ilhali Watanzania walikwisha aminishwa kuwa Dr. Salim ni muuaji!Tunataka kuuelezwa kama tuhuma zile zilikuwa ni kwa ajili ya fitina za uchaguzi tu ila kwa kuwa chama kimechafuka kwa kupoteza dira na mwelekeo sasa ni msafi katika mandhali ya kukiokoa chama.
Dr. Salim ni msikivu,mvumuilivu na asiye na visasi je ameupokeaje ujumbe huo bila kuombwa radhi hadharani kama ilivyotumika kumchafua hadharani kupitia vyombo vya habari.Watanzania tuache unafiki, ifike mahali tuhoji na kuacha nidhamu za uoga kwa malengo ya matakwa ya wakubwa kutekelezwa.Akigombea urais ana kuwa muuaji lakini akiwa hagombei ana stahili kuwa mjumbe wa kamati kuu,chombo cha maamuzi ndani ya chama,wapi tunakwenda?
Mwisho,kuchamba kwingi mwisho kushika mavi,yaliyotokea kwa mzee wetu Dr, Salim iwe fundisho kwa watawala wetu,yatupasa tushindane kwa hoja na kuacha tabia ya siasa za majitaka ilihali uwezo wa kuongoza hatuna,na baniani mbaya hapasi kiatu chake kuwa dawa.Naomba kuwakilisha