TRA NA BANDARI LAZIMA WAFANYE KAZI KWA SAA 24.
Katika kuunga mkono jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr.John Pombe Magufuli katika kuongeza mapato ya nchi na kubana Matumizi ili kama taifa tuweze kujitegemea,huu ni ushauri wangu kwa Waziri wa Fedha pamoja na Serikali kwa Ujumla.
Hakuna shaka kuwa eneo muhimu kuliko yote katika vyanzo vya mapato kwa taifa lolote ni kulipa Kodi.
TRA inapaswa kutobweteka na kile wabachokusanya bali wanapaswa kubadilika kuendana na wakati.
Ukienda Bandarini ukaangalia jinsi bandari inavyofanya kazi.
Bado kuna mambo yanatakiwa kufanyiwa mabadiliko ya haraka hasa katika kipindi hiki cha kuelekea Mwaka Mpya wa Fedha 2016/2017.
TRA kwa mara ya mwisho (Mwezi Desemba 2014 waliruhusu wateja wanaotaka kutoa mizigo Bandarini kulipia mizigo yao kupitua Benki kuu au Benki M.
Hili linachelewesha ukusanyaji wa Mapato (accumulation)
Foleni inakuwa kubwa kiasi cha kuwazidia wahudumu.
Kuna kipindi nilienda Bandarini kufuatilia mzigo,yaani wateja wa ndani na nje ya nchi walikuwa na vifurushi vya fedha wakitamani kulipia lkn kasi ndogo ya upokeaji fedha iliwafanya wateja kukaa na vifurushi vyao kati ya siku tatu hadi siku kumi wakiwa hawajapatiwa hata ushuru wanaodaiwa.
Hivyo kwa taifa ambao tumeweka malengo ya kujitegemea ili kuepuka misaada inayoweza kuhatarisha uhuru wetu.
Ni lazima serikali kupitia TRA waweke utaratibu wa kufanya kazi kwa Saa 24,
Yaani wawepo wafanyakazi wa muda wa mchana na wengine waingie Jioni mpaka saa saba usiku na wengine waanzie hiyo saa saba hadi saa moja asubuhi.
Tunatakiwa kukusanya fedha kwa kasi itakayosaidia kufikia malengo ya taifa kujitegemea na kuachana na utegemezi wa wahisani.
Pamoja na hayo,TRA iruhusu wateja kulipia kupitia Mabenki mengine na sio kutegemea malipo kufanyika kupitia Benki Kuu na Benki M.
Mabenki Mengine ya Tanzania hasa yale yaliyopo mikoani yaruhusiwe ili kuondoa usumbufu na hatari ya kutembea na fedha kutoka Benki moja kwenda benki zilizopendekezwa.
Kiukweli ni kuwa Asilimi 80 ya wateja wa Bandari hawana account kwenye Benk Kuu au Benk M,bali utawakuta wakiwa wateja wa NMB,CRDB,ACCESS,KCB,EXIM n.k hivyo benki hizo zitumike sambamba na Benk M.
Pamoja na hayo TRA waanzishe haraka mfumo wa computer ambao utawezesha mteja kujua jumla ya ushuru anaotakiwa kulipia katika vitu kama Magari.
Pia wawe wanatoa taarifa (updates) za Exchange rate kila siku ili kuruhusu ulipaji kodi kirahisi kama ambavyo wateja wanajua madeni ya magari yao kupitia simu za mkononi.
Pamoja na TRA kufanya kazi masaa 24 haiwezi kusaidi kama Bandari na ICDs (Bandari kavu)wao watafanta kazi kwa saa 12 tu.
Ni muhimu pia Bandari na ICDs wafanye kazi ya kutoa mizigo kwa masaa 24.
Hakuna namna yoyote ya kujitegemea kama tutafanya kazi nusu siku huku kukiwepo idadi kubwa ya vijana ambao wanalilia ajira.
(Mbona Zipo petrol station zinakesha zikitoa huduma iweje eneo nyeti kama Bandari na TRA?
Mbona Vodacom,Airtel ,Tigo na Halotel wanawahudumua wateja kwa masaa 24?
Mbona Madaktari na Askari wetu wa Polisi,JWTZ na Magereza wanafanya kazi madaa 24 kwa kupokezana?
Kwanini Moyo wa Nchi yaani Bandari na TRA wanafunga ofisi wakati kuna maelfu ya wateja wanalilia kulipia mizigo yao?
Wapo watakao dai kuwa wanafanya kazi masaa 24 lkn kiukweli hizo ni porojo,wakati wa Mwakyembe alitangazika kuwa wanafanya kazi masaa 24 lkn kiukweli hilo halipo,mimi niliteseka katikati ya tamko hilo la masaa 24.
2.Mashine za EFDs Kugawiwa bure
Hapa wawepo watakaolipia kwa VAT ,Wengine walipie kwa makadirio kama ilivyo sasa
Ziwepo mashine Maalum ambazo mtu akifanya malipo basi angalau asilimia 2% iwe kodi moja kwa moja.
Hapa namaanisha EFDs zipelekwe Kwenye Mabasi yote ya Mikoani ,
kumbi za Starehe (Clubs)
,Dalala zote za Mijini na vijijini,
Tax
,Bajaji,
Saloon
,Na nyumba za kupangisha(Zote za biashara na Makazi)
Harambee
mbalimbali
Harusi zote zitakofanyika kwenye kumbi.
Kila maalipo yatakayo fanyika kwenye maeneo bainifu basi yalipiwe kodi walau asilimia 2% hadi 5% kadri wadau watakavyoona Inafaa.
Tutavuna zaidi Trillion moja kwa kila mwezi kama hayo maeneo nayo yatatozwa kodi.
Na kwa hili wananchi tusinung'unike bali tujivunie kuchangia fedha za kuendesha nchi yetu.
Na ili kusimamia haya serikaki isiogope kuanzisha Jeshi maalumu la kodi kama yalivyo majeshi ya Zimamoto,tutawalipa fedha ndogo sana vijana watakaoajiriwa kufuatilia kuhakikisha kila manunuzi yana rusiti.
Hata ile michezo ya wafanya biashara kuandika elfu tano badala ya elfu hamsini itapungua sana kama si kukoma kabisa.
Pia Jeshi la la kodi itakuwa fursa nyungine ya ajira kwa vijana hasa wanaomaliza vyuo na kukosa Ajira.
Haiwezekani nchi yenye fursa nyingi za kukusanya kodi eti walipa kodi ni 22% na kati ya hao watumishi wa sekta ya Umma na ile ya binafsi ni 18% eti waliosalia ni 4% tu.
Naomba kwa yeyote mwenye Access na Dr Mpango (Wazari wa Fedha wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anifikishie huu ujumbe.)
Jashia Khamisi Maarufu.
0765733718/0714276818