Ban ya Google kwa Huawei inaifundisha nini dunia, hasa wewe mtanzania?

Kibosho1

JF-Expert Member
Dec 12, 2017
2,491
3,998
Ule msemo wa mtegemea cha nduguye hufa masikini ndio uliopo akilini mwa watengenezaji wa simu za Huawei na serekali ya Uchina kwa sasa.

Kwa nini Karibu 3/4 ya teknolojia inayotumika duniani inatoka Marekani. Mataifa mengine yanajifunza nini? Pamoja na kuwa na chuki na Mmarekani lakini kumbe bado ni mtu muhimu kwako. Kwa miaka sasa China imekua ikipiga marufuku huduma za Google (upande wa apps sio OS) Lengo lao kuu ni kukuza apps zao na kuhofia kuchunguzwa kupitia hizo apps.

Tangazo rasmi ni kuwa Huawei haitapata tena huduma ya mfumo endeshi wa Android,je wamejipanga vya kutosha kuwa na mfumo wao? Jibu ni hakuna. Je hata kama watakuwa na mfumo wao je soko lao litakidhi mahitaji kama ilivyo kwa Android na iOs? Kumbukeni Windows OS ilivyokufa!!.

Mf.Funzo kwetu: vipi ikijatokea wamepiga marufuku apps zao kama instagram,wasap, facebook na youtube? Tuna mbadala au ndio kutegemea kwa jirani mwingine???

Upande wa mtandao wa kijamii angalau tuna JF vipi kwa huduma zingine???
 
Nani kakwambia Africa hizo Apps ni muhimu ?

Huku Africa zipo kwa kulazimisha lazimisha tu, hata ambazo zimeanzishwa huku kama BLOGS tu za watu, YouTube Chanel na JF waulize waanzilishi wao wanavyopata tabu kwa #MadiktetaYaAfrika.

Ikitokea Marekani wakazima hizo Apps mbona yatachekelea sana.
 
China imekua ikitumia pesa nyingi sana kusomesha vijana wake US ilimradi tu kuja kuisaidia nchi yao lakini sasa hivi sijui wataanzia wapi?

Mana kazi sio kutengeneza apps kazi ni kusuka mfumo utakaokuwa wazi kama android ili kila developer aweze kuongeza maujanja yake. Itachukua muda sana.

Hasara kubwa kwa Huawei ipo kwenye soko la nje tu,mana ndani walikua hawataki huduma Google muda sana.
 
Mkuu wapo ila sasa una kuta mwamko upo chini .
Ikitokea shida watatoka mafichoni huko waliko kuja kupiga fursa hakuna kinachoshindikana .
Tuna programmers and coders kibao sema wengi wanafanya for fun na wako low key

Product zao ni competitive mkuu ?
 
Bongo inawezekana kabjsa kuna vijana kibao sana wanatengeneza apps

Labda kwa hio OS
Bongo njaa kali,hawana mitaji na uvumilivu sokoni,ndio maana wao wanatengeneza na kuanza kuweka matangazo ya kukera watu kabla hawapata watumiaji wengi
 
Mkuu wapo ila sasa una kuta mwamko upo chini .

Ikitokea shida watatoka mafichoni huko waliko kuja kupiga fursa hakuna kinachoshindikana .

Tuna programmers and coders kibao sema wengi wanafanya for fun na wako low key
Kipi wamewahi kufanya ambacho hakikuwepo?
 
Wachina ni copycats wa teknolojia ya Marekani huku wakijiwekea bonge la protectionism kujiboost.

Wameshajijua hata wao vichwa panzi wameweka R&D centers zao Israel ili angalau wajitafute.
 
Ukatili ambao umefanywa na marekani Kwa Huawei/china ni janga la kubwa,
Kuna makampuni kama Qualcomm,intel,micron na Google hawa wote wamekata mguu na Huawei sielewi atajiendesha vipi..

Leo hii ukitaka kutengeneza simu lazima utumie chipset(ambazo nyingi zinamilikiwa na marekani au memory ya simu zinafanywa na micron.
Akirudi Kwenye upande wa computer utakubidi utumie bits za intel yaani kila upande kuna marekani na technology yake.

Huawei wamesema wamejiandaa na Os Yao lakini ni vigumu sana leo hii kuja kuzipiku android na iOS
 
Kipi wamewahi kufanya ambacho hakikuwepo?
Hujanielewa naona unataka kuleta ushindani hapa

Jamaa kauliza juu kama wakifungia Na Tanzania itakuwa ikiwa sisi tuna tegemea apps na OS za watu .

Nikajibu kwamba Hata TZ developers,coders,na programmers wapo ila wamejificha sababu ya ushidani uliopo na kwamba hawana mwamko sababu watu wengi wanatumia App na OS za mtoni

Ila sasa shida ikazuka hapa Tz mfano na sisi tukapigwa ban na hao Google na wenye apps zao huko majuu basi hawa developers wetu wataibuka huko walipo .

Wanachokihitaji tu ni financiers tu was kuwawezesha na strategists

Long time kukikuwa na The grid ,darhotwire ,and the like ila walipotea sababu ya ushindani na pesa ya uendeshaji hawakuwa nayo.

So shida ikizuka na fursa itazuka pia watu wataonyesha vipaji vyao vya coding to the maximum

Dhana potofu tuache
 
Huyo jamaa kauliza kuhusu innovators ukajibu wapo.Ndio nimekuuliza kipi walichowahi kufanya ambacho hakikuwepo.Tofautisha developers/programmers na innovators
 
Back
Top Bottom