Ban Ki-Moon aisifu Tanzania kwa mageuzi

Mtu wa Pwani

JF-Expert Member
Dec 26, 2006
4,184
671
wapinzani huku wakisema lolote hawa wao wanaona kuna maendeleo yupi kati ya hawa ana makengeza?
Ban Ki-Moon aisifu Tanzania kwa mageuzi
na Assah Mwambene, New YorkKATIBU Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, ameimwagia sifa Tanzania kwa hatua ilizopiga katika kuleta mapinduzi ya kilimo na elimu nchini.
Ripoti ya kazi ya Katibu Mkuu huyo iliyotolewa hapa hivi karibuni, imeisifia Tanzania kuwa ni moja ya nchi nne za Afrika ambazo zimefanikiwa kuinua kiwango cha wanafunzi wanaoandikishwa kuanza shule na kuboresha kilimo.

“Ninafurahishwa na mafanikio ya nchi za Afrika, hasa katika kuinua kilimo na kuinua uzalishaji katika kilimo,” alisema katika ripoti yake yenye kurasa 70.

Nchi nyingine ambazo Ki-Moon amezimwagia sifa ni pamoja na Ghana, Uganda na Kenya.

Alisema uamuzi wa Tanzania kuanzisha kijiji cha milenia, umeonyesha jinsi nchi inavyothamni na kutekeleza uongozi tangu ngazi ya jamii na kuunganisha mikakati ya ngazi za chini na za juu katika kutekelesa malengo ya milenia.

Kijiji hicho cha milenia, kipo Mbola katika wilaya ya Uyui, mkoani Tabora na kingine kipo katika wilaya ya Micheweni katika Mmkoa wa Kaskazini kisiwani Pemba.

Ripoti hiyo pia inazilaumu nchi tajiri kwa kushindwa kwao kutekeleza ahadi zao kuongeza maradufu misaada ya kimaendeleo inayoelekezwa Afrika ifikapo mwaka 2010.

“Pamoja na ahadi hizi, ukiondoa msamaha wa madeni na misaada ya kibinadamu, miasaada mingine haijaongezeka sana tangu mwaka 2004,” alisema.
 
Hajui anachoongea, labda hata hicho kijiji anachokiongea hakiwezi kufanana na hata Dorasan korea kusini
 
Nadhani Ban ki moon (Bank ya Mwezini) anatamani kuichana chana hiyo report yake... kwa hali halisi ya Sasa
 
Back
Top Bottom