Bamakita limeunga mkono kauli ya Samuel Sitta, | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bamakita limeunga mkono kauli ya Samuel Sitta,

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by bagwell, Sep 24, 2012.

 1. b

  bagwell Senior Member

  #1
  Sep 24, 2012
  Joined: Sep 19, 2012
  Messages: 113
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Baraza la Maadili la Kiislamu Tanzania (Bamakita) limeunga mkono kauli ya Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, ya kuwataka wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwang’oa watuhumiwa wa ufisadi katika uchaguzi unaoendelea ndani ya chama hicho, kwa kuwa watu hao ndio wanaochafua sifa nzuri ya chama.

  Mwenyekiti wa Bamakita, Sheikh Athumani Mkambaku, alisema jijini Dar es Salaam jana kuwa baraza linaamini kwamba, CCM ni chama kikubwa chenye viongozi wengi makini na wazoefu wa kuendesha serikali kuliko chama kingine chochote cha siasa nchini na kwamba, wananchi walio wengi bado wanakiamini.

  Hata hivyo, Sheikh Mkambaku alisema chama hicho kimekuwa kikichafuliwa na baadhi ya viongozi wake wakuu, ambao wamekuwa wakijihusisha na vitendo vya kifisadi vya kuhujumu uchumi wa taifa.

  “Ndio maana tunaunga mkono kauli ya Mheshimiwa Sitta na tunaomba wanachama wa CCM waifanyie kazi kauli hiyo ili waweze kukinusuru chama chao dhidi ya wapinzani na pia watakuwa wamerudisha heshima ambayo imeanza kupungua kutokana na kashfa mbalimbali za ufisadi zinazowaandama baadhi ya viongozi wakuu wa chama hicho,” alisema Sheikh Mkambaku.

  Kutokana na hali hiyo, aliwataka wana CCM kuutumia vyema uchaguzi wa chama wa mwaka huu kuchagua viongozi waadilifu na kuondoa dhana kuwa watu wazuri na wachapakazi wanaowajibika kwa wananchi hawatakiwi katika chama hicho, bali mafisadi ndio wanaopendeza.

  Alisema dhana hiyo ndio imesababisha CCM kuitwa ‘chama cha mafisadi’, wakati haiko hivyo.

  Aliwaomba wana CCM watakaopiga kura kuchagua viongozi katika ngazi ya wilaya, mkoa na taifa, kuiga mfano wa Yesu alipoingia katika hekalu la Yerusalemu na kuzipindua meza za wabadilisha fedha na walanguzi na kuwaambia ‘nyumba yangu itaitwa nyumba ya salama na ibada, nyinyi mnaigeuza kuwa pango la wezi na wanyang’anyi?’.

  Hivyo, Sheikh Mkambaku amewataka wana CCM kuwaambia mafisadi kuwa lengo la CCM ni kuwakomboa wanyonge na siyo kuwakandamiza na kuwafanya kuwa maskini kwa kuwapandishia gharama za maisha kwa kulipa madeni ya ujanjaujanja.

  “Leo IPTL, kesho Richmond, keshokutwa Dowans na hatujui itafuta kampuni gani, mambo kama hayo ni kikwazo cha maisha bora kwa kila Mtanzania,” alisema Sheikh Mkambaku.

  Sheikh huyo alisema njia pekee ya kukomesha wizi aliouita ‘wa mchana’ kama huo, ni kuwatoa mafisadi na vibaraka wao kupitia uchaguzi huo na kusema kwa kufanya hivyo watakuwa wameudhibiti pia upinzani.

  Alisema kinyume cha hapo, watakuwa wameimarisha upinzani kwa mikono yao na watashuhudia CCM ikiporomoka kwa kupoteza majimbo na hata nafasi ya urais na kusema hakuna kitu kisichowezekana kwani Watanzania wa leo siyo wa jana.

  “Hivyo, hakuna haja ya kuchagua viongozi wachafu ili baadaye mjipe kazi ya kuwasafisha wakati chama kinao watu wengi wasafi, wasomi na wachapa kazi. Kwanini mjipe kazi isiyokuwa ya lazima?” alihoji Sheikh Mkambaku.

  Mwishoni mwa wiki iliyopita, akizungumza katika mahafali ya 11 ya Shule ya Msingi ya Mchapuo wa Kiingereza ya Kwema, Wilaya ya Kahama, mkoani Shinyanga, Sitta alisema CCM inatia aibu kutokana na kujiimarisha kwa kikundi cha wasiokuwa waadilifu, wanaokifanya kizomewe na kukosolewa na wapinzani.

  Alisema hali hiyo imeathiri mashiko ya CCM kwa umma, na kukwamisha jitihada za serikali kuharakisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo na ustawishaji huduma za jamii nchini.
   
 2. Jiwejeusi

  Jiwejeusi JF-Expert Member

  #2
  Sep 24, 2012
  Joined: May 3, 2011
  Messages: 755
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  hawa bahakita na wao ni ccm? Kwa nini washabikie mambo ya ccm? Wananikumbusha enzi zile za tamko la maaskofu, kikwete ni chaguo la mungu.
   
 3. Amiliki

  Amiliki JF-Expert Member

  #3
  Sep 24, 2012
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 2,087
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Ndio vikundi vinavyolelewa na CCM, baadae vinavimba mkia kama ilivyo kwa akina Ponda. Na vinajua kwamba vikundi vyote vya Kibabaishaji, nje ya CCM havitakuwepo.
   
 4. Nyalotsi

  Nyalotsi JF-Expert Member

  #4
  Sep 24, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 5,104
  Likes Received: 551
  Trophy Points: 280
  wangeongea maaskofu kuirekebisha cdm kusingekalika humu. Kila mtu angekuja na utumbo wake. Lakini kwa kuwa serikali ina wadini kuanzia juu, huwezi kushangaa. Hii ni kawaida kwao, kwani wanaishi kwa misaada ni lazima wamtumikie bwana wao.
   
 5. p

  politiki JF-Expert Member

  #5
  Sep 24, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  Bamakita limemuunga mkono fisadi kutaka mafisadi wenzake wangolewe, jamani mfanyieni research mtu mwenyewe kabla hamjaamua kumuunga mkono. Kumbukeni ni nani alikuwa anazuia kuundwa kwa tume ya bunge kuchunguza issue za deepgreen,wizi wa mabilioni ya kagoda na meremeta wakati dr.slaa alipowashikia bango bungeni. Please grow up
   
 6. D

  Deo JF-Expert Member

  #6
  Sep 24, 2012
  Joined: Nov 10, 2008
  Messages: 1,190
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Je huyu shekh ana ubavu kama wa Ponda.? Ingekuwa Ponda kasema tungesubiri utekelezaji, asingesubiri sisemu fisadi iafanye hivyo
   
Loading...