Balozi wa Uingereza nchini Tanzania amtembelea Makonda

TataMadiba

JF-Expert Member
Feb 7, 2014
9,866
5,747
Balozi wa Uingereza nchini Tanzania *Bi. SARAH COOKE,* amemtembelea Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam *Mhe PAUL MAKONDA* na kufanya nae mazungumzo yenye lengo la kuongeza na kuimarisha Ushirikiano uliopo baina ya jiji la Dar es salaam na London, nchini Uingereza.

Katika mazungumzo yao, *Mhe MAKONDA* na *Bi. COOKE* wamekubaliana kuongeza kasi ya Ushirikiano baina ya majiji makubwa mawili *Dar es salaam* Tanzania na *London* nchini Uingereza, makubaliano ambayo yatasaidia kupatikana kwa vifaa vya kisasa vya kuzuia na kupambana na majanga kama vile moto na mafuriko, ambapo *Mhe MAKONDA* ameomba kupatiwa magari ya kisasa ya shughuli za kuzima moto na uokoaji.

*Mhe MAKONDA* pia ameomba kusaidiwa vifaa maalum vya *UTAMBUZ*I wa mifumo ya teknolojia ya kamera za kisasa zitakazofungwa *barabarani* kwa ajili ya kusaidia *USALAMA* wa magari, raia na mali zao mifumo ambayo inafanya kazi katika jiji la London nchini Uingereza, hatua itakayokwenda sambamba na ujengewaji *UWEZO* kwa maofisa wa *polisi* wa Mkoa wa Dar es salaam katika matumizi ya mifumo hii.

Katika kukabiliana na changamoto ya *MIGOGORO ya ARDHI* mkoani Dar es salaam, *Mhe MAKONDA* ameomba kusaidiwa kuwajengea uwezo *maafisa ARDHI* na *Mipango miji* wa Mkoa wa Dar es salaam katika matumizi ya kisasa ya upimaji na upangaji ardhi, mafunzo ambayo yatakwenda sambamba na upatikanaji wa vifaa vya kisasa vya kupima ardhi, jambo litakalosaidia *kuondoa KERO* ya upatikanaji wa *HATI* pamoja na *vibali vya UJENZI* Mkoa wa Dar es salaam.

Katika mazungumzo hayo, *Mhe MAKONDA* na *Bi. COOKE* wamejadili suala la uanzishwaji wa *JIJI la FIKRA* (brain storming center ) kwa ajili ya kuwakutanisha vijana wabunifu kama ilivyo kwa *Tech City Uingereza.*

Katika kuhitimisha mazungumzo yao, *Mhe MAKONDA* na *Bi. COOKE* kwa pamoja wamekubaliana kuzikutanisha timu za wataalamu kutoka London na Dar es salaam za kukabiliana na Majanga haraka iwezekanovyo.

*Bi. COOKE,* kwa upande wake *amefurahishwa* na jinsi Mkuu wa Mkoa anavyopambana na *vita ya dawa za kulevya* ambayo imeathiri nguvu kazi kubwa sana katika jiji la Dar es salaam na kumuhakikishia kuwa *Serikali ya Uingereza inaunga mkono jitihada zote* zinazofanywa katika kuwaletea maendeleo wananchi wa Mkoa wa Dar es salaam.

*Imetolewa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam.*
*23/05/2017.*
 
Watanzania tunatiana aibu , yani mtu anakutembelea labda kusalimia halafu mara moja unakuwa ombaomba wa adabu ! Unatokea na litania ya vitu vya kusaidiwa .
Ptuuu!
 
Ikiwa yeye bashite kaomba vyoote hivyo,
Yeye anatoa nini?
Maana hawa jamaa hawakawii kuombaaa wapewe ndo.......
 
Back
Top Bottom