Balozi wa Palestina nchini ampongeza Rais Magufuli

diana chumbikino

JF-Expert Member
May 29, 2018
428
368
1566467141663.png

BALOZI wa Palestina nchini Tanzania, Hamdi Mansour AbuAli amempongeza Rais John Magufuli na serikali yake kwa kuimarisha uchumi wa nchi yake. Amesema, Rais Magufuli anasimamia dhamira yake ya kuimarisha uchumi na kutekeleza miradi ya maendeleo hasa katika karne hii ya maendeleo.

Mwakilishi huyo wa Palestina akimtambua Rais Magufuli kwa jina la ‘bulldozer’, amesema kiongozi huyo wa nchini amefanikiwa kuielekeza Tanzania kwenye uchumi wa kipato cha kati kwa kuainisha sera na mazingira ya biashara.

Akitoa pongezi hizo kwa Rais Magufuli, balozi huyo amesisitiza kuwa Palestina itaendelea kuunga mkono mpango wa maendeleo wa taifa 2025, unaolenga kuwezesha uchumi thabiti na wenye ushindani kwa kuhamasisha uwekezaji. “Sote tunaona juhudi za Rais John Pombe Joseph Magufuli katika kukuza maendeleo ya kiuchumi, na kwa kasi hii Tanzania itakuwa moja ya nchi zenye uchumi mkubwa na maendeleo barani Afrika. Serikali yangu inaungana mkono na serikali ya Tanzania ili kuleta maendeleo ya kiuchumi nchini,” amesema.

Balozi Abu Ali amesisitiza, kwamba taifa lake (Palestina) imeendelea katika nyanja ya teknolojia na uvumbuzi, hususani katika sekta za afya, kilimo na ujenzi hivyo kuweza kuwa na ushirikiano kati ya nchi hizi mbili. Ameeleza, tayari kuna kampuni tatu za dawa kutoka Palestina ambazo zimeonesha nia ya kuanzisha ubia na kampuni za ndani na kwamba, Shirika la Ushirikiano wa Kimataifa wa Palestina (PICA) nchini, linaendelea na utafiti ili kuvumbua maeneo tofauti ya ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.

“Kwa maagizo kutoka kwa Rais wa Palestina, Mahmoud Abbas na Waziri wa Mambo ya nje na wahamiaji, Dk Riyad Malki, Shirika la Ushirikiano wa Kimataifa la Palestina (PICA) linafanya utafiti wa maeneo tofauti ya ushirikiano kati ya nchi zetu mbili. “Lengo ni kuleta maendeleo kwa watu wetu na nchi zetu mbili na hivyo basi, kuboresha uhusiano wetu wa kihistoria ambao ulianza tangu zama za Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na kiongozi wetu Mohammed Yasser Arafat,” amesema.

Pia Balozi AbuAli amepongeza hatua ya Rais Magufuli na serikali yake kwa msimamo wake wa kuendelea kuunga mkono na kushikamana na Palestina. Pia amepongeza hatua ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), kupitisha Lugha ya Kiswahili kuwa lugha ya nne rasmi katika jumuiya hiyo.

SOURCE: MWANAHALISI ONLINE
 
lazima ajikombe kwa serikali, wanahitaji msaada kutoka kwa kila anayeweza kuwasaidia, wanapitia magumu mno huko kwao.
 
Kwao wapi? Soma historia nchi ya Israel ilivamiwa na Waarabu kutoka Saudia Arabia na Yemen wakati Wayahudi walikuwa utumwani Misri na Babylon(Uajemi=Persia = Iran) Waarabu haohao walivamia nchi zote za Africa Kazikazini(Morocco, Mauritania, Chad Kazikazini, Tunisia, Algeria, Libya, Sudan, Misri, Sinai) ambapo mpaka leo wamezikalia!!!!!!!!!!!Jamani someni vitabu vya historia ya tangu miaka ya elfu tatu kabla ya Yesu(Isa) kuzaliwa, msiwe malimbukeni. Wote warudi kwao Saudia na Yemen!!
 
tofautisha historia na hadithi za kwenye biblia
 
Ina maana unataka kutwambia Nabii Mussa alipowakomboa Wanaisrail.kutoka utumwani walipofika the promised land walikuta pashavamiwa na Waarabu?
 
Balozi wa Palestina angemchukua na yule mwenzake wa Zanzibar ili waende kumpongeza Mtukufu Mfalme.
 
Ina maana unataka kutwambia Nabii Mussa alipowakomboa Wanaisrail.kutoka utumwani walipofika the promised land walikuta pashavamiwa na Waarabu?

Ndiyo(Yes)!! Waarabu hawakumalizia safari za Uvamizi hapo ila waliendea mpaka Morocco, Sudan etc.
 
BIG
Kwao wapi? Soma historia nchi ya Israel ilivamiwa na Waarabu kutoka Saudia Arabia na Yemen wakati Wayahudi walikuwa utumwani Misri na Babylon(Uajemi=Persia = Iran) Waarabu haohao walivamia nchi zote za Africa Kazikazini(Morocco, Mauritania, Chad Kazikazini, Tunisia, Algeria, Libya, Sudan, Misri, Sinai) ambapo mpaka leo wamezikalia!!!!!!!!!!!Jamani someni vitabu vya historia ya tangu miaka ya elfu tatu kabla ya Yesu(Isa) kuzaliwa, msiwe malimbukeni. Wote warudi kwao Saudia na Yemen!!
UP. BIG UP
 
Ndiyo(Yes)!! Waarabu hawakumalizia safari za Uvamizi hapo ila waliendea mpaka Morocco, Sudan etc.
kama nawaona vile Yaani walitamani mpaka Zanzibar chini ya mpango wa Falme za Yemen, pakawa makao makuu ya serikali ya Yemeni, kama Dodoma yetu vile ilvyo leo kwa Tanzania, bado wana amini Zenji ni mali yao mpaka leo, wanataka kurudi, pia walimega km 25 kutoka pwani ya Africa Mashariki.

Walijazana, kuzaliana ktk visiwa vya Shelisheli, ni nchi pekee ya Waarabu katikati ya weusi.

Huko Palestina kulikuwa na weusi wazawa kibao, waliuawa wote, wachache wakakimbilia Lebanon, Yemen nk, lkn hawana sauti, wala maisha mazuri, wanapitishwa haraka haraka kwenye camera za Western media. ina maana camera hazigandishwi kuwaonyesha. hasa hasa vita inayoendelea Yemen. chunguza.
 
Back
Top Bottom