Balozi wa Libya na danadana ya bendera mbili tata

KIGENE

JF-Expert Member
Joined
Jan 22, 2011
Messages
1,164
Points
1,500

KIGENE

JF-Expert Member
Joined Jan 22, 2011
1,164 1,500
Balozi wa Libya nchini Tanzania Prof.Ahmed A El Ash'hal ametuma ujumbe mwingine tata kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe kuwa hayuko tayari kupeperusha bendera ya utawala uliosambaratika wa Gadhafi baada yakuamua kutopeperusha bendera yeyote kwenye ubalozi wa nchi yake.

Picha zilizopigwa jana na gazeti la Majira zinaonyesha milingoti miwili ikiwa haina bendera yeyote.

Je kwa kudhalau na kupuuza maelekezo ya Membe kunaipa sababu tosha serikali kumtimua balozi huyo na Vienna Convetion inasemaje kwa kitendo kama hiki.
 
TzPride

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2006
Messages
2,586
Points
2,000

TzPride

JF-Expert Member
Joined Nov 2, 2006
2,586 2,000
anajua tuna serikali legelege ndio maana hajali. Ole wake angefanya kwenye awamu ya kwanza, zamaníii angekuwa anashuhudi milio ya bunduki huko kwao.
 
Jituoriginal

JF-Expert Member
Joined
Feb 8, 2010
Messages
362
Points
195

Jituoriginal

JF-Expert Member
Joined Feb 8, 2010
362 195
Balozi uko sahihi, Libya serikali ya Mshenzi Gadafi imeingia msituni na kutokomea baada ya wanamapinduzi kumtimua .Viva Ntc, Pole Alhaj Membe !mradi wa Kiwanda cha Sementi kimeota mbawa.
 
Kiranga

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2009
Messages
47,525
Points
2,000

Kiranga

JF-Expert Member
Joined Jan 29, 2009
47,525 2,000
Balozi uko sahihi, Libya serikali ya Mshenzi Gadafi imeingia msituni na kutokomea baada ya wanamapinduzi kumtimua .Viva Ntc, Pole Alhaj Membe !mradi wa Kiwanda cha Sementi kimeota mbawa.
Labda Membe anataka ahadi ya mradi wa kiwanda cha sementi kuwa guaranteed na serikali mpya kabla ya kuitambua, tehe tehe tehe.
 
Arafat

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2009
Messages
2,581
Points
0

Arafat

JF-Expert Member
Joined Nov 17, 2009
2,581 0
Barazi yupo sawa, membe ni ndio mpuuzi!

Hatuwezi kuwachagulia bendera, ila tunaweza kuvunja nao ubalozi hakuna option ya yingine zaidi ya hizo mbili, amatuwatambue au tusiwatambue. Kama hatuwatambui basi ina maana tunavunja nao ubalozi automatically hakuna bendera itapeperuka pale, au tuwatambue na bendara ni mali yao haituhusu lazima ipeperuke.
 
Feedback

JF-Expert Member
Joined
Mar 14, 2011
Messages
7,995
Points
1,500

Feedback

JF-Expert Member
Joined Mar 14, 2011
7,995 1,500
Juzi balozi wa Libya nchini Bulgaria aliyeteuliwa na Gaddafi katimuliwa baada ya serikali ya waasi kupeleza balozi mpya.
SOFIA (Reuters) - Bulgarian police stormed the Libyan embassy in Sofia on Friday and forced out diplomats of Muammar Gaddafi's regime after a new ambassador appointed by Libya's interim authority arrived in the Balkan country, the foreign ministry said.
 
Kiranga

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2009
Messages
47,525
Points
2,000

Kiranga

JF-Expert Member
Joined Jan 29, 2009
47,525 2,000
Barazi yupo sawa, membe ni ndio mpuuzi!

Hatuwezi kuwachagulia bendera, ila tunaweza kuvunja nao ubalozi hakuna option ya yingine zaidi ya hizo mbili, amatuwatambue au tusiwatambue. Kama hatuwatambui basi ina maana tunavunja nao ubalozi automatically hakuna bendera itapeperuka pale, au tuwatambue na bendara ni mali yao haituhusu lazima ipeperuke.
1. Tanzania haiwatambui waasi.
2. Balozi alikuja Tanzania kama balozi wa serikali ya Gaddafi, katoa credentials zake Ikulu kama balozi wa Gaddafi.
3. Balozi hakupeleka credentials mpya za serikali mpya ya Libya, in fact hawezi kwa sababu serikali ya NTC haitambuliwi na serikali ya Tanzania.
4. Balozi kapandisha bendera ya NTC kihuni bila ku coordinate na MOFA.
5. Kwa sababu serikali ya Tanzania haiitambui serikali ya NTC, Membe yuko sawa kumkataza balozi kupeperusha bendera ya waasi.

Serikali ya Tanzania haiwezi kuulazimisha ubalozi wa Libya kupeperusha bendera, lakini ubalozi wa Libya hauwezi kupeperusha bendera ya serikali ambayo haitambuliki na serikali ya Tanzania.

Sasa hivi Libya haina ubalozi Tanzania, kwa sababu ubalozi uliokubalika (wa serikali ya Gaddafi) umejivua uwakilishi wa ubalozi huo, na ume ji affiliate na serikali isiyotambuliwa na serikali ya Tanzania.

Sio tu ni sawa kusema kwamba kutopeperusha bendera yoyote ni sawa, ni sawa pia kusema kuwa Libya haina ubalozi Tanzania.
 
Edson

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2009
Messages
9,329
Points
2,000

Edson

JF-Expert Member
Joined Mar 7, 2009
9,329 2,000
ndio maana serikali haieleweki.....kwan yeye balzi ni mjinga kutundika bendera ya waas? wao(MoFA) hawakusema lolote wakati waasi wanapambana kule libya wala kutoa tamko.maana yake hawafungamani na upande wowote.leo mtu wao(qaddaffi) ameondoshwa ndo wanakuja na matamko yasiyo na tija?!!

kesho atundike bendera ya waasi huyo balozi
 
Concrete

JF-Expert Member
Joined
Mar 12, 2011
Messages
3,607
Points
0

Concrete

JF-Expert Member
Joined Mar 12, 2011
3,607 0
@Hakuna cha kuuma maneno hapa, Serikali ya Tanzania inatakiwa kuchukua moja ya hatua zifuatazo: 1/Kuvunja rasmi uhusiano wa Kibalozi na Libya (Kwani Tanzania imetamka wazi kutokuutambua utawala wa sasa wa Libya). Automatically Ubalozi wa Libya uliopo nchini unafungwa na balozi wa Libya anarudi kwao mara moja. Kinyume na hivyo ni; 2/Kuutambua rasmi utawala mpya wa Libya (Ili kuendelea na uhusiano wa kibalozi na nchi ya Libya). @Kumbuka Ubalozi wowote Unawakilisha nchi (Watu na Serikali yao) bila kuangalia nani ni mtawala. Hivyo balozi wa Libya aliyeko nchini ni mwakilishi wa nchi ya Libya (Watu&Serikali ya Libya) na siyo Ghadafi kama Ghadafi, japokuwa aliyemteua alikuwa ni Ghadafi. @Kuendelea au kubadilishwa kwa balozi wa Libya aliyepo sasa Tz ambaye aliteuriwa na Ghadafi, kunategemea maamuzi ya serikali mpya ya Libya ya sasa, Na siyo jukumu la Serikali ya Tz kuwapangia. Mambo ya bendera siyo issue ya msingi sana kwa sasa, hizo ni Diplomatic protocal za kawaida sana.
 
REBEL

Senior Member
Joined
Dec 15, 2010
Messages
166
Points
195

REBEL

Senior Member
Joined Dec 15, 2010
166 195
nimesoma International Law,sema na swali dogo tu,nyumba ya ubalozi wa Libya inatambulika kama jamhuri ya libya au tanzania?nijibuni kisomi na tumieni sheria husika kwe jibu lenu.sitaki bla blah.
 
Unaposema "serikali ya Tanzania inatakiwa..." inatakiwa na nani? Nchi gani? Watu gani? Principle gani? Serikali ya Tanzania ni a sovereign entity na haitakiwi na mtu yeyote kuitambua serikali nyingine yeyote. Itatambua tu serikali inayotaka kuitambua, hii ni basic tenet ya sovereignty. Sasa wewe unapossema "inatakiwa" inatakiwa na nani/nini?

Hakuna sababu ya Tanzania kuvunja uhusiano wa kibalozi uliokuwapo kabla ya hii melee ya waasi kuanza, not so much kwa sababu Gaddafi alikuwa mzuri sana but especially kwa sababu hatujui kama hao rebels watakuwa any better. Especially if you consider Tanzanian interests.

Kuitambua serikali katika international diplomacy ni "bargaining chip". Kuna watu wa visiwa vya Pacific hawana hata influence zaidi ya kuwa na kura UN wanalipwa dola nzuri na Taiwan kwa sababu tu wanaitambua Taiwan na kui support katika lobbying zake UN. Kwa nini tutake kuwatambua watu kirahisi rahisi tu bila hata ya kupata nafasi ya kuzungumza nao kujua wanataka nini, wana mpango gani kuhusu Libya na wananchi wake na watasaidiaje interests za Tanzania ?

Pia, Tanzania inaweza kuweka viwango vyake vyovyote inavyotaka ili kitambua serikali ya Libya. Mathalani, inaweza kusema inataka kujua misimamo katika mambo fulani fulani, inaweza kutaka kujua muundo wa serikali, inaweza kusema inataka uchaguzi ufanyike kwanza etc.
 
Kiranga

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2009
Messages
47,525
Points
2,000

Kiranga

JF-Expert Member
Joined Jan 29, 2009
47,525 2,000
nimesoma International Law,sema na swali dogo tu,nyumba ya ubalozi wa Libya inatambulika kama jamhuri ya libya au tanzania?nijibuni kisomi na tumieni sheria husika kwe jibu lenu.sitaki bla blah.
Ni Jamhuri ya Tanzania iliyo nje ya jurisdiction ya Jamhuri ya Tanzania katika mambo ya kidiplomasia.

Ndiyo maana ukiandamwa kisiasa na kukimbilia ubalozi wa Marekani/ nchi nyingine inayoclaim kutetea demokrasia, polisi wakaja kukufuata hawawezi kuingia ndani kwa nguvu za dola kisheria bila idhini ya ubalozi.

This raises a very delicate point, kama ni hivyo kwa nini kuwalazimisha bendera gani wasipandishe?

Kwa sababu mkataba uliowapa hiyo haki umetiwa sahihi na serikali ya Libya ya Gaddafi, sio rebels.

Gaddafi angeamua kubadili bendera yake wala kusingekuwa na issue, tatizo linakuja, balozi huyu kidiplomasia si yule tuliyemkubali, ingawa ni mtu mmoja.

Hajawahi kuleta credentials zake Ikulu kwa niaba ya NTC. Hawezi. Hatuitambui NTC.
 
Forum statistics

Threads 1,356,250
Members 518,868
Posts 33,128,588
Top