Mbunge wa Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo akimkabidhi zawadi Balozi wa China Mhe. Dr. Lu Youqing wakati wa tafrija ya kumuaga Balozi huyo, anayemaliza muda wa utumishi Kama Balozi wa China nchini Tanzania. Aidha, Mhe. Muhongo alipata nafasi ya kufanya mazungumzo kwa Lengo la kusaidia wananchi wa Jimbo la Musoma Vijijini na kumpongeza kwa misaada aliyokuwa akiitoa kwenye jimbo la Musoma vijijini kama vile kutoa michango ya Ujenzi wa vyumba vya madarasa, Ujenzi wa maabara, Libeary za kusomea na huduma ya matibabu ya bure kutoka kwa timu ya madakrari bingwa wa china. Mwisho Mhe. Muhongo alimtakia Mhe. Balozi mafanikio mema huko aendako.
Mbunge wa Musoma vijijini Mhe. Prof. Muhongo akisalikiana na Balozi China Dr. Lu wakati wa hafla ya kumuaga Balozi huyo iliyofanyika Leo 5/9/2017