Balozi Seif Alli Idd adaiwa kukosa sifa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Balozi Seif Alli Idd adaiwa kukosa sifa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by bagwell, Sep 24, 2012.

 1. b

  bagwell Senior Member

  #1
  Sep 24, 2012
  Joined: Sep 19, 2012
  Messages: 113
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  NAIBU Katibu Mkuu wa CUF, Ismail Jussa amemuelezea Makamo wa pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd kuwa ni kiongozi aliyepoteza sifa katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa, Zanzibar.

  Jussa akizumgumza katika mkutano mkubwa wa hadhara wa CUF uliyofanyika jana katika Jimbo la Bububu, alimtaka Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein na Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharifu Hamad, kulielewa hilo.

  Aidha, akionekana kukerwa na utendaji wa kiongozi huyo Jussa, alisema Balozi Seif Ali Idd amepoteza sifa za kuwa kiongozi katika Serikali hiyo na utendaji wake wa kazi unaelekea kuwa wa uwakilishi wa Tanganyika:

  "Sitaki kumung'unya maneno hapa Dk Shein na mwenzako Maalim Seif…Balozi Seif amepoteza sifa ya kuwa kiongozi katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa na wala sitafuni tena maneno huyu ni Balozi mkaazi wa Serikali ya Tanganyika ndani ya Zanzibar huyu sio Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar huyu ni Balozi mkaazi," alisema na kuongeza:

  "huyu…huyu…huyu ameletwa hapa kwa lengo maalumu la kuvuruga Serikali ya umoja na kuvuruga umoja wa Wazanzibari…nasema umoja wetu ndio silaha kubwa," alisema Jussa.

  Jussa ambaye pia ni Mwakilishi wa Mji Mkongwe, aliwatahadharisha wananchi wa Zanzibar, na mitego ya baadhi ya viongozi wa CCM kama Balozi Seif Ali Idd:

  "Tukiingia katika mtego tutakuwa tumeingia katika mtego wa Balozi Seif Idd, nataka kumhakikishia Balozi Seif Ali Idd kwamba sisi hata siku moja hatutaondoka katika mstari huu ataondoka yeye na vibaraka vyao," alisema Jussa.

  Kuhusu kauli yake hiyo Naibu Katibu Mkuu huyo wa CUF Zanzibar, alisema ng'oo hawezi kubadilisha matamshi yake dhidi ya kiongozi huyo mwenye dhamana ya shughuli za kila siku za Serikali na Baraza la Wawakilishi:

  "Ati Waziri wa nchi Mohamed Aboud, anasema tumtake radhi Balozi Seif Idd…nasema hatumtaki radhi hadi kiama lakini mimi kwa niaba ya Wazanzibari wote namwambia Balozi Seif Ali Idd jiuzulu," alisisistiza Jussa.

  Alisema Wawakilishi wa CUF, ndani ya Baraza la Wawakilishi, hawatamtambua Mwakilishi huyo mpya wa Jimbo la Bububu, kutoka CCM, kama Mwakilishi halali wa kuchaguliwa na wananchi:

  "Jukumu letu ni kuirejesha Zanzibar katika mamlaka kamili, nasema na sisi Wajumbe wa CUF ndani ya Baraza la wawakilishi hatutamtambua kama ni mwakilishi wa jimbo la BUBUBU na hatutampa mashirikiano kama ni mwakilishi halali bali tutamtambua Issa Khamis Issa kuwa ndio Mwakilishi halali wa Jimbo hili la Bububu", alisema Jussa..
   
 2. N

  NnyaMbwate JF-Expert Member

  #2
  Sep 24, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,410
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Taabu Hii. Lakini Mwalimu Nyerere alishatabiri haya. Ukishaonja nyama ya Binadamu, hutaiacha!
   
 3. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #3
  Sep 24, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,355
  Trophy Points: 280
  hawa jamaa si competent kweli including Jusa mwenyewe.Wazenj sijui ni watoto wa mama mmoja.
   
 4. KOMBAJR

  KOMBAJR JF-Expert Member

  #4
  Sep 24, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 5,848
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  dugu moja kwisha chokana sasa!huku mwendo ni:rockon:power! power!
   
 5. i

  iseesa JF-Expert Member

  #5
  Sep 24, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 944
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hawa apana dugu moja. iko wazanzibari, tena iko wamatumbi, vile vile iko wazanzibara, afu tena iko washirazi, ama iko nakosea?
   
 6. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #6
  Sep 24, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,745
  Likes Received: 1,459
  Trophy Points: 280
  Huyo Jussa nadhani ni tatizo jingine ktk ndoa ya CCM na CUF. Haishi maneno ya ubaguzi, uchochezi, kebehi na matusi.

  Yeye hastahili kuwa hata balozi wa nyumba kumi kumi
   
 7. a

  abdul 28 JF-Expert Member

  #7
  Sep 24, 2012
  Joined: May 29, 2012
  Messages: 325
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  seif aliy idi anaumbuka wazanzibar wauovu wet lazima tuwatajee
   
 8. p

  politiki JF-Expert Member

  #8
  Sep 24, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  kaanza na wabara sasa kahamia kwa wanzanzibar wenzake ndiyo inavyokwenda wakimaliza waunguja watahamia wapemba wenyewe kwa wenyewe.
   
 9. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #9
  Sep 24, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  "Talaka ndani ya GNU inanukia," hawafiki 2015 salama, na kama watafika hapo ndio mwisho wa ndoa yao.
   
 10. a

  afwe JF-Expert Member

  #10
  Sep 24, 2012
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 4,087
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  Niliwahi kusikia watu wanasema ya Ngoswe mwachieni Ngoswe! Mkimaliza kumnanga huyu sijui atafuata nani tena!
   
 11. Wamunzengo

  Wamunzengo JF-Expert Member

  #11
  Sep 24, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 810
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 60
  Ningependa sana kama Jussa angetaja mambo ambayo Balozi kayafanya mpaka kufikia kumtaka ajihudhuru. Mleta maada mbona habari yako haija-balance??? Lete hayo makosa anayotuhumiwa nayo Balozi ili tupime nani anachafua hali ya hewa huko kwenye harufu nzuri ya marashi ya Karfuu. Ni vizuri tukazijua tuhuma za pande zote mbili ili tujiaminishe kama ni Jussa au Balozi???
   
 12. a

  abdul 28 JF-Expert Member

  #12
  Sep 24, 2012
  Joined: May 29, 2012
  Messages: 325
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  wewe ni mtu ****** kweli hujuwi kama huyu balozi wenu nchini zanzibar ndie alie tumia nguvu kubwa kwa uchaguzi wa jimbo na kusababisha kifo cha kijana mmoja
  pili ni mtu ane wambia wananchi kukataa serekali ya umoja wa kitaifa

  tatu huwambia watu watowe maoni ya mfumo huu huuj wa muungano watu hawapati aliandaa vipeperushi kupeleka kwa tumee huyu ni ****** mwenziyoooo
   
 13. Wamunzengo

  Wamunzengo JF-Expert Member

  #13
  Sep 25, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 810
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 60
  Mkuu abdul 28, naona umenichana kisharishari ile mbaya. nashukuru nilielimishwa kwamba kutukanwa ni sehemu ya changamoto. ahsante kwa kunitusi, ila ni kweli mi sikujua uharo aliokuwa kautapika huyo Balozi, na kwa namna ulivyonielewesha hapo, nimeona kweli Jussa yupo sahihi. Huyu Balozi ni mpuuzi na kwa kweli hastahili kuwa kiongozi wa umma. Tatizo ccm, huwa hawana kipimo cha kujua kama mtu anastahili kuongoza umma au familia yake tu ya watu 4. Uongozi wa umma ni tofauti na uongozi wa familia. Balozi hafai kabisa.
   
 14. F

  Fitinamwiko JF-Expert Member

  #14
  Sep 25, 2012
  Joined: Aug 13, 2012
  Messages: 4,810
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 180
  Mh Jussa ni mkweli, anasema anachoamini kwa maslahi ya Wazanzibari. Tunahitaji viongozi kama huyu, kwa maendeleo
   
Loading...