Akitoa uamuzi wa kesi hiyo, Jaji Mussa alisema malalamiko ya Benandys ni ya msingi hivyo alimuamuru Balozi Nkya na mkewe kulipa kampuni hiyo Sh500,000 kila siku kuanzia Februari 24,2005 alipovunja mkataba hadi siku ya hukumu hiyo.Kimahesabu tangu kipindi hicho hadi sasa ni karibu siku 2,300 ambazo zinafanya kuwa malipo hayo ya hasara ya kibiashara yafikie Sh1.15 bilioni.Mgahawa huo ulikuwa ukitoa huduma kwa watalii na Watanzania, Internet na uuzaji wa vitabu.