Balile kwa hili umekurupuka


true joh msamehe ni uelewa mdogo na masuala ya chuo ni kukosa ustaarabu tu angeuliza kwanza na siyo kuongea uongo na sio kila kitu uchangie
 
Kaka mwaka wa chuo sio miezi12, ni miezi8 tu! 230,000X8=1,840,000
Alivosema 1,800,000 hakukosea ila alichokosea ni kusema miezi3. Badala ya mwaka mzima(alimezeshwa vibaya) 60,000 kwa mwezi chakula cha aina gani? Kwa sababu hata usema unakula mkate na maji ya uhai kila siku hiyo 60,000 sidhan kama inatosha.
Ilo swala la ipad na tv amefanya generalization ambayo sio realistic!

Sent from my BlackBerry 9360 using JamiiForums
 

Si ndo huyu mmoja wa wahariri wa Jamhuri? Hawa jamaa wakiambiwa ni makanjanja wanakasirika na kuchukia baadhi ya watu,huwezi jua labda anawaonea wivu wanaolipiwa na bodi yeye pengine hata Bachelor degree haijui Jamaa yake Manyerere aje atuambie hapa huyu jamaa kama sio Kanjanja!
 

Aaah!ndo maana kama nilivyosema huyu hata bodi ya mikopo haijui, muda wote amekuwa akifadhiliwa mara na kanisa mara scholarship Ulaya,ndo tatizo aulize watu tulivyotaabika, watu wengine huwa wanatia hasira sana basi tu!
 

Nafikiri umeangalia upande mmoja wa shilingi, nilimsikia Balile zaidi alitumia lugha ya picha ambayo kwako imekuwa ngumu kuielewa! Upande wa pili aw shilingi, Balile alisema enzi zao hawakuwa wakishika hela jambo ambalo ni la kweli; walisafiri kwa warrant na kula walikula cafeteria. Kizazi cha leo, kinapewa hela hela ambayo ni kweli kuwa imechangia kwa kiasi kikubwa wanafunzi kufeli. Niko kwenye taasisi ya elimu, kweli sasa hivi wanafunzi wengi mburula. Usibishe Ndg yangu.
 

Ndo walewale kina Balile! Ni Tsh 7500 kwa siku piga kwa miezi mitatu,na wengine hiyohiyo ndo akate alipe ada na hiyo ada inategemea na asilimia yako sasa kama % yako ni ndogo hapo ndo utakapojuta na hasa kama wazazi ndo hivy o ungaunga mwana ni kazi. Nashurukur bwana mdogo anamaliza mwez ujao japo nipumzike kidogo. Waulize vijana upate data za kutosha huko vyuon. Wanaofanya Luxury kwa kias kikubwa ni michango toka kwa wazaz/walezi.
 

Ukimwita Balile kanjanja, utakuwa si tu humtendei haki Bali pia utakuwa humpendi tu kwa kusikia watu wengine wakimsema na humfamu. Tusikurupuke kuwasema watu tusiowafahamu!
 
Ukimwita Balile kanjanja, utakuwa si tu humtendei haki Bali pia utakuwa humpendi tu kwa kusikia watu wengine wakimsema na humfamu. Tusikurupuke kuwasema watu tusiowafahamu!

Tueleweshane basi ukweli ni upi,maanake yeye alitakiwa na ushahid wa kutosha kwa kila anachokisema kuliko kupotosha! Mtu akimwambia anatumika au ni Kanjanja atakosea?
 

Unakula chakula gani hicho ambacho unatumia 60, 000TSH kwa mwezi?
 
Kifikra na kiuhalisia Ndugu Byabato unamuunga mkono mtoa hoja kuwa alichokisema Balile (Mwandishi mwenzio) ni UONGO wa mchana kweupe. Waandishi wa namna hii ndiyo wanaoaminisha wananchi na ndugu zetu huko uraiani kuwa tunaishi maisha ya anasa vyuoni alhali mkumbuke vyuoni wanakuja watu wa familia tofauti na wote tunapata MKOPO ila wengine wazazi wao wankipato na kwao vitu kama I-Pad, I-phones, LCD etc kuwa navyo ni jambo la kawaida. Kwa taarifa yako na hyake kuna wazazi wanawalipa watoto wao mishahara wakiwa vyuoni alimradi tu mwanae asome kama motisha maana wengine huwa hawana nia na shule. Sasa ukimkuta huyu anaspendi kwa anasa utasema wote ni watu wa anasa. Hii ni FALLACY. Hii ndiyo inasababisha tukirudi vijijini tuambiwe WANACHUO HATUJENGI KWETU wakati tunalipwa!!! Waandishi kama hawa ni hatari badala ya kueleza UMMA uhalisia wa mambo wanachochea uhasama na chuki kati ya wanavyuo na wananchi wengine.
Kwa taarifa yake huyo Ndg. Balile hapo Hall 6 watu wanalala watatu kwenye kitanda kimoja...akaandike hili ili Mukandara azingatie umuhimu wa makazi kwa WANACHUO...
 
ama kweli "no research no right to talk",hv wanajua kua mahesabu yapigwayo ya kulipia rumu kwa semister na kwa chuo cha udsm ni tofauti na vyou vinginevyo vya mikoani?bei ya chumba ni sh 78,000/= na laki unusu kwa semister na kwa vyuo vya ndani ya chuo na nnje ya chuo. je wanaosoma Iringa, mbeya Arusha n.k nako wanapata yumba kwa bei hiyo? tusipende kufanya jambo pasipo kufanyia utafiti. na usidhani kila mwanachuo ana akili mbovu na isiyo na uvumilivu na busara kama yake.
 

Majibu mepesi kwa maswali magumu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…