Balbu hizi ni hatari | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Balbu hizi ni hatari

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by GM7, May 17, 2010.

 1. GM7

  GM7 JF-Expert Member

  #1
  May 17, 2010
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 492
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Balbu hizi ni hatari
  Monday, 17 May 2010 12:22

  LONDON, Uingereza

  WAKATI teknolojia ya matumizi ya nishati ya umeme yakizidi kukua, Wizara ya Afya nchini Uingereza imehadharisha kuhusu aina ya balbu mbalimbali zinazotumika majumbani kwa kile ilichodai kuwa zinaweza kusababisha madhara mbalimbali kiafya pindi zinapopasuka.

  Kwa mujibu wa Wizara hiyo, mtu anapaswa kuondoka chumbani kwa angalau dakika 15 mara balbu hizo zinazoitwa Energy Saving au Low Energy zinapopasuka kutokana na kuwa zina sumu aina ya Mercury ambayo inasababisha maradhi mbalimbali kiafya.

  Maradhi ambayo yametajwa na Wizara hiyo ni pamoja na maumivu ya kichwa, kurukwa na akili, kizunguzungu na matatizo mengine mengi kiafya.

  Mbali na maradhi hayo, kwa mujibu wa Wizara hiyo pia kwa watu wenye mzio (allergy), balbu hizo zinaweza kuwasababishia madhara ya ngozi na maradhi mengine baada ya kugusa mabaki ya balbu hizo.

  Wizara hiyo pia imehadharisha kutosafisha mabaki ya balbu hizo kwa kutumia mashine za kufanyia usafi zinazotumia upepo kwa kile ilichodai kuwa zinaweza kusambaza sumu hiyo katika vyumba vingine.

  Imeeleza kuwa ili kuepukana na madhara yanayoweza kusababishwa na mabaki ya balbu hizo ni bora ukasafisha kwa kutumia brashi ya kawaida na kisha kuyahifadhi mabaki hayo kwenye mfuko uliofungwa vyema na kuyaweka mbali na nyumba.

  Katika ushauri huo Wizara imeelekeza kuwa ni bora kutonunua ama kutumia balbu hizo kwa ajili ya kuokoa afya na mazingira.

  Source: Dar Leo
   
Loading...